Spika Ndugai amewafukuza Bungeni mara kadhaa Halima Mdee na Esther Bulaya kwa utovu wa nidhamu. Je, aliwaonea?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Kuwatetea Halima James Mdee na Esther Bulaya kuhusiana na utovu wa nidhamu ni lazima ujitoe ufahamu kidogo.

Tukitaka kujenga jamii ya watu waadilifu ni lazima tuwe wakweli.

Halima James Mdee mara kadhaa amefukuzwa Bungeni na Spika Ndugai kwa utovu wa nidhamu.

Halima James Mdee amewahi kutupwa rumande kwa saa 48 na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi kwa makosa ya kinidhamu. Mkuu wa Wilaya ni mwakilishi wa Rais Wilayani.

Sasa kama Halima Mdee ameweza kuadhibiwa na Bunge, akaadhibiwa na Serikali, Mahakama pia ilimhukumu kifungo/faini, kwanini inakuwa nongwa akiadhibiwa na chama chake kwa makosa ya aina hiyo hiyo?

Tunaweza kudhani tumejificha lakini Mungu anatuona.

Maendeleo hayana vyama!
 
Naona umeanza kufanyia kazi mahubiri ya Askofu Mtetemela mkuu

Ila kumsikiliza anachozungumza KAZI ni kupoteza muda maana hana maamuzi ambayo anaweza kuyasimamia mfano mdogo kwenye sakata la wabunge wa CUF walipofukuzwa tu Prof. kwa kasi ya mwanga akawa kashapata taarifa zao na akawatambua siyo wabunge tena na kwa kasi ileile akapata wapya akawatambua.

Leo wale ambao wamefukuzwa na Chadema anasema hao bado ni wabunge sasa mtu wa design hii unamsikiliza wa nini!?
 
Kuwatetea Halima James Mdee na Esther Bulaya kuhusiana na utovu wa nidhamu ni lazima ujitoe ufahamu kidogo.

Tukitaka kujenga jamii ya watu waadilifu ni lazima tuwe wakweli...
Halima na wenzake wameadhibiwa na Mbowe sababu ya wivu.

Wewe unafikiri kina Mbowe wangepata ubunge wangesusia huo ubunge kisa hawatambui uchguzi?

Tangu enzi za Slaa wanalia kuibiwa lakini hawajawahi kususa kuwa wabunge!

Nasema spika awakinde hao kina dada.
 
Kuwatetea Halima James Mdee na Esther Bulaya kuhusiana na utovu wa nidhamu ni lazima ujitoe ufahamu kidogo.

Tukitaka kujenga jamii ya watu waadilifu ni lazima tuwe wakweli...
Kwani shida yenu ni nn?
Uanachama si tayari Mmewavua?
Sasa mbona makelele meeeengi
Au mlitaka na ubunge wakose, then nyie mnapata faida gani?
 
Halima na wenzake wameadhibiwa na Mbowe sababu ya wivu.

Wewe unafikiri kina Mbowe wangepata ubunge wangesusia huo ubunge kisa hawatambui uchguzi?

Tangu enzi za Slaa wanalia kuibiwa lakini hawajawahi kususa kuwa wabunge!

Nasema spika awakinde hao kina dada.
Nauliza tu ile sheria ya kwamba mbunge akivuliwa uanachama na chama chake no matter how ili mradi amevuliwa bado anaendelea kuwa mbunge kwa amri ya spika?

Unajua kuna wakati baadhi ya viongozi wa CCM wanaifanya ccm ionekane chama cha kidikteta rasmi kwa kukiuka katiba wazi wazi.

Katiba imezungumza wazi wazi mbunge yeyote akivuliwa uanachama basi hapo hapo anakosa sifa ya kuwa mbunge lakini kwa ccm hii mpya katiba sio chochote.
 
Halima na wenzake wameadhibiwa na Mbowe sababu ya wivu.

Wewe unafikiri kina Mbowe wangepata ubunge wangesusia huo ubunge kisa hawatambui uchguzi?

Tangu enzi za Slaa wanalia kuibiwa lakini hawajawahi kususa kuwa wabunge!

Nasema spika awakinde hao kina dada.
Yaani Spika anasimama hadharani nakusema atawalinda. Huo ni uvunjifu wa katiba waziwazi.
 
Nauliza tu ile sheria ya kwamba mbunge akivuliwa uanachama na chama chake no matter how ili mradi amevuliwa bado anaendelea kuwa mbunge kwa amri ya spika?..
Shida ni kwamba wamevuliwa uanachama kwa wivu.

Alafu katiba ni makaratasi tu ndio maana hata hapo chadema yakichanwa yakaandikwa upya ili Mbowe awe mwenyekiti wa kudumu
 
Mlijua fika haki haitotendeka lakini mkashiriki uchaguzi!
Ndio mnaamka sasa? Toka lini wezi wa kura wakawa waadilifu? Kama ni mkweli anzia kwenye zoezi zima lilitoa hao wabunge, mchakato ule haukuwa wa kiadilifu, unategemea spika wa bunge kama hilo awe muadilifu?
 
Back
Top Bottom