Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,436
- 4,151
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.
Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.
View attachment 1932327
Clowns at their best.
Acha waendelee kuifisidi nchi. Wanadai wanaimarisha uchumi huku wamekataa katakata kuhakikisha uwepo wa misingi imara ya usimamizi wa serikali.
Ndugai na bunge lake si chochote mbele ya Rais na mawaziri.