Spika ndo tatizo

Gwisya boy

Member
Nov 13, 2011
8
1
Mbunge la Mh. Sita lilikuwa na mvuto kwa sababu alikuwa hajali masilahi ya ccm, lakini huyu mama hana lolote, anakataa hoja ya upinzani halafu anaruhusu wabunge kuacha kujadili katiba na kuanza kumjadili Lisu, kafulila na wapenda nchi wote.
 
Alichaguliwa kuwa speaker purposely hivyo anatekeleza jinsi alivyoagizwa na waliomuweka kwenye hicho kiti
 
kwanza naomba nikupe pole kwa mambo mazito ambayo yanakuzunguka kwa sasa, jambo la katiba ni jambo zito kabisa ambalo kwa sasa lipo mezani, ukiachia mambo mengine madogo madogo kama jairo na mengineyo.

Mama mimi binafsi nakushauri mapema kabisa kwamba usome alama za nyakati ili kuliepusha taifa kuingia katika janga kuu ambalo chanzo kikuu kitakuwa ni wewe na msimamo wako egemezi katika chama chako.

Ukiwa kama spika unapaswakuwa msikivu wa hoja za wabunge wote na sio
Kupuuza hoja zinazoonekana ni chungu kwa chama chako.
Jaribu kuulizia joto la wenye nchi katika maamuzi yako na ya wabunge wa chama chako limepanda kiasi gani?

Mjadala mnaojadili bungeni wa katiba unachukuliwa kwamba ni wako wewe pamoja na wabunge wa chama chako, mawaziri na rais tu na sio mjadala wa wananchi.

Naomba utambue kwamba wananchi wanataka kuona maoni ya wapinzani yanasikilizwa na kama hayafai yapingwe kwa hoja na sio mijadala ya kumjadili mtu.

Katiba ni mali ya watanzania wa sasa na wa wakati ujao hivyo ni kosa kubwa na hukumu yake ni kifo kwa mtu yeyote anaeichezea katiba kwa maslahi yake binafsi au chama chake.

Jihadhali na matokeo ya hicho mnachokijadili kama katiba kumbe ni maamuzi kandamizi ambayo watanzania wamechoshwa nayo, kilichompata gadafi na bagbo kinakuja tanzania kama hamta sikiliza wananchi.
 
Mbunge la Mh. Sita lilikuwa na mvuto kwa sababu alikuwa hajali masilahi ya ccm, lakini huyu mama hana lolote, anakataa hoja ya upinzani halafu anaruhusu wabunge kuacha kujadili katiba na kuanza kumjadili Lisu, kafulila na wapenda nchi wote.
yeye sheria kwake ni issue pia ndio maana hawakatazi hao wenzake. hakuna kifungu cha bunge atakitaja bila kuangalia kitabuni hata kama amewahi kuwa naibu wa spika
 
Anna Makinda deserves nothing!
But in similar point of view, we want to show something so that she realizes that she is in power in order to serve the country's interests rather than the party's interests.
 
Inashangaza kuona Spika anawapeleka puta wabunge na mawaziri waulize na kujibu maswali kwa kifupi sana lakini anaruhusu wabunge kutumia muda mwingi kutoa mipasho kwa Chadema bila kujali kuwakatiza kwa kisingizio cha muda.
 
Hawezi kuwazuia wakati hawana lolote la kuchangia maana yeye na wao walishakubaliana upite baada ya kuaminishana kwamba hauna marekebisho ndo maana wenye akili wameususia na tunawaelewa
 
Back
Top Bottom