Dkt. Bagonza: Kama Yuda alichokoza; aliyechokozwa asichokozeke. Kama Yuda amechokozwa; asichokozeke

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,439
Reaction score
42,119
YUDA AMECHOKOZWA; ASICHOKOZEKE❗️❗️❗️

Yuda wa Biblia alimsaliti Bwana Yesu. Siamini kama mleta hoja anamaanisha msalitiwa katika hoja yake ni sawa na Bwana Yesu!?!? Ipo siku tusiyoijua, “Yesu” huyu aliyefumbwa katika hoja hii, atafananishwa na “Mtume” asiyelinganishwa. Hapatatosha. Mleta hoja hajachagua vizuri maneno yake na mifano yake. NIMEMSAMEHE BURE.

Sakata hili lina mapichapicha sita ya hatari.

1. Msemaji aliwahi kuchokonoana na Rais wake huko kwao mpaka akajiuzuru. Mama yetu akamchukua, akamteua. Ina maana Rais yule na Mama yetu hawako shwari? Je Mama ni Yuda wa Rais yule kwa kuwa alimchukua mleta hoja?

2. Mleta hoja ni Mzanzibari, anamnanga Yuda Mtanganyika. Hii ni kero au ufa katika muungano? Alikosekana Mtanganyika wa kumrudi Yuda Mtanganyika?

3. Mleta hoja anasali Ijumaa; anamnanga anayesali Jumapili kwa kutumia picha ya (Yuda) anayeomba huruma makanisani. Tuseme katumwa na msikiti?!

4. Maneno yake yameingia kwenye Hansard. Bunge halikukanusha. Je ni bunge zima linamwita Makamu kuwa ni Yuda?

5. Naibu Spika alipomwongoza ajikite kwenye hoja, wabunge walipiga makofi. Walifurahia Naibu Spika kuingilia au walimshangilia mtoa hoja. Je makofi hayo ni mashangilio ya tumbili wa Kijaluo anayeshangilia pori linaloungua bila kuwaza atalala wapi usiku?.

6. Hoja imetolewa siku Rais ameondoka nchini na kwa mujibu wa katiba, Makamu ndiye Mkuu wa nchi wa zamu. Mtoa hoja anamaanisha hamtambui Makamu kama Mkuu wa nchi wa zamu?

Kwa vyovyote, kuna dalili mbaya. Matiti ya binti wa Kijaluo yakiishaota, hayafichiki na hayarudi nyuma.

7. Wakristo wanaamini usaliti wa Yuda ulileta wakovu. Bila usaliti, Yesu asingekufa. Bila kifo, asingefufuka; na bila kufufuka, wokovu usingepatikana. Hakuna wokovu bila usaliti. Waliookoka wameisaliti dhambi ili wawe huru. Mleta hoja kakosea. Hakuna Yuda na hakuna Yesu katika hoja yake. Zilikuwa ni saa za jioni; Dodoma mapito ni mengi, hatujui alipitia wapi kuja bungeni.

8. Kisiasa, CCM bila tishio la upinzani wa nje, inayumba. Tulishauri mapema sana Lisu aachiwe ili aiunganishe CCM, tukapuuzwa. Angeachiwa mapema, CCM ingeungana na kusahau tofauti zake za ndani ili kukabiliana na upinzani. Hivi sasa wapo wana CCM wanamtamani Lisu ili awasaidie kuona thamani ya umoja wa chama chao. Hamjachelewa.

9. Mama alikuja na “R” nne. Moja ya “R” hizo ni REFORMS, yaani mabadiliko. Lisu akamuunga mkono Mama kwa kusema “Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi” (NO REFORM, NO ELECTION). Akakamatwa kwa uhaini wakati aliunga mkono falsafa ya 4R! Mbadilishie mashtaka mseme alikosea kumuunga mkono Mama!

10. Wenye madaraka punguzeni nguvu, ongezeni hekima. Ruto alitumia nguvu, sasa ana nguvu lakini urais (Presidency) ni dhaifu. Kambarage alitumia nguvu na hasira Januari 30, 1984, Mpaka anaondoka duniani, jambo hilo lilimtesa. Trump alimnanga Pence hadharani, akaangushwa na Biden kwenye uchaguzi. Rais na Makamu hawatenganishwi kirahisi. Si mnatuimbia maridhiano!? Ridhianeni, wapambe tukose kazi.

Kama Yuda alichokoza; aliyechokozwa asichokozeke. Kama Yuda amechokozwa; asichokozeke.

Wajaluo bhana! Eti, hata anayepotea ana anakokwenda.
 
Anaandika Askofu Bagonza✍🏽
 
Attachments

  • FDownloader.Net_AQNAOUfPlX5KbZoQaz1vfQVxwnomGiIxg04KDBarrw_snv2Pk9bnKySbtkuPHBFvIJRPWM-n-Idu6G...mp4
    7.3 MB
FB_IMG_1780509141182.jpg
 
Nchimbi lianzishe tu vijana tuko nyuma yako kazi yetu kumalizia vijana tuna shauku na hamu pamoja na ari ya oktoba 29 volume 2 kisas ni haki
 
Mama alikuja na “R” nne. Moja ya “R” hizo ni REFORMS, yaani mabadiliko. Lisu akamuunga mkono Mama kwa kusema “Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi” (NO REFORM, NO ELECTION). Akakamatwa kwa uhaini wakati aliunga mkono falsafa ya 4R! Mbadilishie mashtaka mseme alikosea kumuunga mkono Mama!
 
Nchimbi lianzishe tu vijana tuko nyuma yako kazi yetu kumalizia vijana tuna shauku na hamu pamoja na ari ya oktoba 29 volume 2 kisas ni haki
Labda km JW, PT, na wengineo wawe nyuma ya Nchimbi,
Vinginevyo itakua zaidi ya Oct 2025.
 
7. Wakristo wanaamini usaliti wa Yuda ulileta wakovu. Bila usaliti, Yesu asingekufa. Bila kifo, asingefufuka; na bila kufufuka, wokovu usingepatikana. Hakuna wokovu bila usaliti. Waliookoka wameisaliti dhambi ili wawe huru. Mleta hoja kakosea. Hakuna Yuda na hakuna Yesu katika hoja yake. Zilikuwa ni saa za jioni; Dodoma mapito ni mengi, hatujui alipitia wapi kuja bungeni.
:BeerTime:
 
Kwa vile wamezoea kutengeneza wapinzani wa mchongo inawezekana wengine ndio hao hakina Simai ila bila kujijua wanajipaka matope
 
YUDA AMECHOKOZWA; ASICHOKOZEKE❗️❗️❗️

Yuda wa Biblia alimsaliti Bwana Yesu. Siamini kama mleta hoja anamaanisha msalitiwa katika hoja yake ni sawa na Bwana Yesu!?!? Ipo siku tusiyoijua, “Yesu” huyu aliyefumbwa katika hoja hii, atafananishwa na “Mtume” asiyelinganishwa. Hapatatosha. Mleta hoja hajachagua vizuri maneno yake na mifano yake. NIMEMSAMEHE BURE.

Sakata hili lina mapichapicha sita ya hatari.

1. Msemaji aliwahi kuchokonoana na Rais wake huko kwao mpaka akajiuzuru. Mama yetu akamchukua, akamteua. Ina maana Rais yule na Mama yetu hawako shwari? Je Mama ni Yuda wa Rais yule kwa kuwa alimchukua mleta hoja?

2. Mleta hoja ni Mzanzibari, anamnanga Yuda Mtanganyika. Hii ni kero au ufa katika muungano? Alikosekana Mtanganyika wa kumrudi Yuda Mtanganyika?

3. Mleta hoja anasali Ijumaa; anamnanga anayesali Jumapili kwa kutumia picha ya (Yuda) anayeomba huruma makanisani. Tuseme katumwa na msikiti?!

4. Maneno yake yameingia kwenye Hansard. Bunge halikukanusha. Je ni bunge zima linamwita Makamu kuwa ni Yuda?

5. Naibu Spika alipomwongoza ajikite kwenye hoja, wabunge walipiga makofi. Walifurahia Naibu Spika kuingilia au walimshangilia mtoa hoja. Je makofi hayo ni mashangilio ya tumbili wa Kijaluo anayeshangilia pori linaloungua bila kuwaza atalala wapi usiku?.

6. Hoja imetolewa siku Rais ameondoka nchini na kwa mujibu wa katiba, Makamu ndiye Mkuu wa nchi wa zamu. Mtoa hoja anamaanisha hamtambui Makamu kama Mkuu wa nchi wa zamu?

Kwa vyovyote, kuna dalili mbaya. Matiti ya binti wa Kijaluo yakiishaota, hayafichiki na hayarudi nyuma.

7. Wakristo wanaamini usaliti wa Yuda ulileta wakovu. Bila usaliti, Yesu asingekufa. Bila kifo, asingefufuka; na bila kufufuka, wokovu usingepatikana. Hakuna wokovu bila usaliti. Waliookoka wameisaliti dhambi ili wawe huru. Mleta hoja kakosea. Hakuna Yuda na hakuna Yesu katika hoja yake. Zilikuwa ni saa za jioni; Dodoma mapito ni mengi, hatujui alipitia wapi kuja bungeni.

8. Kisiasa, CCM bila tishio la upinzani wa nje, inayumba. Tulishauri mapema sana Lisu aachiwe ili aiunganishe CCM, tukapuuzwa. Angeachiwa mapema, CCM ingeungana na kusahau tofauti zake za ndani ili kukabiliana na upinzani. Hivi sasa wapo wana CCM wanamtamani Lisu ili awasaidie kuona thamani ya umoja wa chama chao. Hamjachelewa.

9. Mama alikuja na “R” nne. Moja ya “R” hizo ni REFORMS, yaani mabadiliko. Lisu akamuunga mkono Mama kwa kusema “Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi” (NO REFORM, NO ELECTION). Akakamatwa kwa uhaini wakati aliunga mkono falsafa ya 4R! Mbadilishie mashtaka mseme alikosea kumuunga mkono Mama!

10. Wenye madaraka punguzeni nguvu, ongezeni hekima. Ruto alitumia nguvu, sasa ana nguvu lakini urais (Presidency) ni dhaifu. Kambarage alitumia nguvu na hasira Januari 30, 1984, Mpaka anaondoka duniani, jambo hilo lilimtesa. Trump alimnanga Pence hadharani, akaangushwa na Biden kwenye uchaguzi. Rais na Makamu hawatenganishwi kirahisi. Si mnatuimbia maridhiano!? Ridhianeni, wapambe tukose kazi.

Kama Yuda alichokoza; aliyechokozwa asichokozeke. Kama Yuda amechokozwa; asichokozeke.

Wajaluo bhana! Eti, hata anayepotea ana anakokwenda.
Asante Moderator kwa uhakiki wa heading
 
Back
Top Bottom