Spika Makinda awadhalilisha wasomi wanasheria

Hivi huyu mama na chama chake cha magamba wanatumia akili kweli, maana nashangaa wanaposema mswada sio wa kuandika katiba mpya ni kuchagua kamati ya kuratibu. Ninavyojua katiba inaanza kuandikwa kwanza pale unapokubali kuiandika plus michakato yote inayofata na ikiwa ni hautakuwa serious tokea mwanzo kwenye foundation unaweza kutoa kitu cha ajabu. Naomba spika Makinda na wenzake wana CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao waache kuwapotosha wananchi kwamba mswada uliopelekwa sio wa kuandika katiba mpya.

Na kama wanasema mswada sio wa kuandika katiba mpya na huo mswada ni wa nini basi, na hiyo tume ni ya nini basi.
 
Bi Kiroboto nae...wasomi ambao wamesoma robo ya elimu inayohitajika ndio wapi hao?..lol
 
Mbona CV yake inapingana na utetezi wake kufuatilia kauli ya Pius Msekwa ya kushauri Spika awe mwanasheria? Katika utetezi wake yeye alisema amesoma uhasibu na kwamba elimu ya sheria iliuwa sehemu ya course yake. Inawezekana akawa hata hakumbuku alisoma nini?
 
Angekuwa kwenye yale maeneo yetu angecharazwa bakora zisizokuwa na mfano!! Huyu Mama anatakiwa kuadabishwa mapema kwani naamini kuna baadhi ya fuse kwenye ubongo wake zilishaharibika ama hazipo kabisa.
 
Mbona kwenye hayo maelezo hapo juu hasemi ukweli ni upi sasa kama wasomi walikuwa wanawapotosha wananchi? Watu wengine bana,... wanavaa mavazi makubwa kuliko size zao!

Lakini ndugu yangu hivi kweli huwezi kuelewa kwamba utaratibu mzuri wa kupata katiba mpya ndiyo unaozaa katiba nzuri? Hivi kama walipotosha kwa nini umerudishwa ili utengenezwe vizuri? Ninavyojua muswada ukipelekwa Bungeni kwa hati ya dharura leo hii ingekuwa bunge lilishapitisha na Rais kusaini, sasa kama mpaka leo hii bado Bunge halijapitisha unategemea kwamba wasomi waliopinga walikosea na kwamba walipotosha, fikilia kwamba tume ingeundwa tuseme kwa 'sheria' ile halafu ikapendekezwa na tume wazalamo wote wauawe, halafu mtu asihoji kwa kuhofia atakayehoji mapendekezo ya tume atakuwa ametenda kosa la kustahili kutumikia kifungo, wewe ungejisikiaje?

Fikilia kwamba tume ndiyo muandaaji wa rasimu ya katiba, ndiyo muelimishaji, ndiyo mpigaji wa kampeni kuhusu kura ya maoni haruhusiwi mtu ama kikundi kufanya kazi hizo hivi hii ni demokrasia ya wapi hiyo? Mbona Kenya vyama, mashirika mbalimbali yaliruhusiwa katika kutoa elimu na kupiga kampeni kuhusiana na mapenedekezo hatimaye watu wakachuja pumba na mchele katiba ikapitishwa. Imenikumbusha uchaguzi wa miaka ya 90 ambapo mgombea wa urais au ubunge anakuwa mmoja halafu anapiga kampeni ili mumpe kura ya ndiyo na nyimbo zinaimbwa hakuna wa kupiga kampeni kumpinga huyo ni kichekesho ambacho naona watu hawataki kukirudia lakini wanaonekana wasaliti. HONGERA WASOMI, hata mitume walionekana hawafai lakini leo wanaonekana wakombozi, songa mbele historia itawahukumu.
 
kumbe hii lack of political leadership inasababishwa na lack of education,nilikua sifaham:crying:
 
dah, sikujua kama huyu bibie ana elimu ndogo hivi! this explains everything. kwa kweli tumsaidie anahitaji every assistance that can be given...mradi na yeye awe na werevu wa kuelewa usaidizi atakaopewa
 
Hata hivyo Spika Makinda alielezea jinsi anavyokerwa na baadhi ya wasomi ambao huwapotosha wananchi kuhusu Muswada wa kuundwa kwa tume itakayoratibu mchakato wa wananchi kutoa maoni kuhusu Katiba mpya.

Alisema wasomi hao ambao wamesoma robo ya elimu inayohitajika, wamelenga kufanya upotoshwaji ili wananchi waamini kwamba Serikali imeandaa Muswada wa Katiba mpya jambo ambalo halikuwa na ukweli wa aina yoyote.

Alisema Muswada ambao ulisababisha baadhi ya wasomi kuzomea bila kujua nini kimeandikwa, ulikusudia kupata maoni ya wananchi juu upatikanaji wa tume hiyo kulingana na mapendekezo ya Rais Jakaya Kikwete.

“Baadhi ya wasomi wetu wamepata elimu robo robo, wameshindwa kuelewa Muswada unataka nini….hawa ni watu wa kuelimisha wananchi kweli, wengine wanazomea kiholela tu bila kuusoma vyema,” alisema.

Alisema Muswada huo uliwasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge, lakini kabla haujasomwa mara ya pili wananchi walipata fursa ya kutoa maoni katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar, lakini kuliibuka vurugu zilizosababisha kurejeshwa serikalini.

Hata hivyo alisema Kamati za Bunge zilizokuwa zikiratibu maoni hayo zilipata maoni mengi ambayo yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha Taifa linapata utaratibu ambao utasaidia upatikanaji wa Katiba mpya.

Source: Habari leo - Makinda: sitishiki, natumia busara

Tatizo la watanzania wakiambiwa ukweli huwa hamkubali, spika amesema kweli !
 
Anadharau alisema wabunge hawjui kiu eti yeye ni spika,ni mama na pia mlezi kwa hiyo akianza kuwapiga rungu wabunge sasa hivi itakuwa ni kuwaonea anawaandalia semina nyingine ,ha ha ha
 
Anadharau alisema wabunge hawjui kiu eti yeye ni spika,ni mama na pia mlezi kwa hiyo akianza kuwapiga rungu wabunge sasa hivi itakuwa ni kuwaonea anawaandalia semina nyingine ,ha ha ha

Kwani bi- Kiroborobo anajua malezi ni nini? Angekuwa amewahi kuwa mlezi asingeongea pumba hizo wakati ilmu yake ni ya sekondari na kisha awaponde wasomi wa ilmu ya Vyuo vikuu.

Bi Kiroborobo hana taaluma yo yote ya Sheria ataweza mikiki mkiki ya vijana wanasheria machachari akina Tundu Lisu, Mnyika nk? Unaona kaishiwa hoja anakuja na usanii wa kuzoeleka ciciem eti wamesomea roborobo, yeye hata 1% ya roborobo hana kwa kuwa hajatia mguu kwenye ilmu ya sheria.

Aibu kubwa Tanzania kuwa na Speak msimamizi wa baraza la Kutunga sheria za nchi wakati hajui cho chote misingi ya taaluma ya sheria ila kusoma kilichoandikwa tu.
 
Back
Top Bottom