Spika Makinda, athibitisha 'Muswada Umeondolewa'

Mimi nilitokwa na machozi pale nilipoona wanachama wa CCM "kwa kutojua"
wakishabikia huo muswaada tata wa katiba mpya. Nilichoweza kusema ni kwamba
Labda hawajui walitendalo kwani kwa mapendekezo hayo hata kama CDM wengeingia
madarakani, basi watanzania tugeendelea kuteseka kwani hiyo ilikuwa katiba ya watawala
na sio katiba ya watanzania.

Eeeh Yesu ninakushukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na ya watanzania wengine
kwa kutunusuru na hila za CCM za kutupatia katiba fake inayokidhi matakwa ya aliyeko madarakani.

Nimefarijika sana hii ni zawadi nzuri sana ya PASAKA. Mungu wetu tunaomba utuepushe na
hao waovu wasiopenda kuona Watanzania tukipata katiba yetu.
 
Maandamano ya CHADEMA yamezimwa kwa mantiki hiyo

Sijui kama hili ni swali,statement au ?
maana nimeona gazeti moja hivi la udaku wanasema maandamano hamna!
Website ya chadema ndo imezubaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
sijui ipo kwa ajili ya nini
 
Ninaamini tukiweka nguvu kidogo pia vile vipengele vinavyoondoa haki yetu ya kubadadili katiba vitaondolewa, ili turuhusiwe kujadili Muungano na madaraka ya rais na pia nadhani watakubali mjadala utoke bungeni na kamati zote ziteuliwe bungeni na siyo rais
 
Wanabodi,

Ile sintofahamu ya Muswada imemalizika,
Wenye access watch TBC Live Now!.

Spika ametangaza Kamati ya Sheria na Katiba imeomba marekebisho kadhaa ikiwemo kuletwa kwa lugha ya Kiswahili, na kutangazwa kwenye magazeti ili iwafikie Watanzania wengi.

Wabunge wapiga vigelegele kwa kuimba CCM..CCM...as if ni CCM ndio wameshinikiza mabadiliko hayo.

Spika ameomba Watanzania tudumishe mila za kujadili kwa utulivu na amani

Kuondolewa kwa Muswada huu, ni uthibitisho mwingine kwa JF iko juu kwenye kupata breaking news za jikoni, na JF ni very reliable source of information.

Viva JF.

Pasco.

Duh! Hapo kwenye rangi usanii mtindo mmoja! Hata aibu hawana! Walioshinikiza kuondolewa muswada huo ni CDM lakini wanashangilia CCM!!! Kweli CCM wamejaa wasanii wa hali ya juu!
 
Makinda kazi imemshinda maana hawezi hata kuishauri serikali kwenye mapungufu na badala yake analazima mswada uendelee bila kuzingatia wananchi anaowatumikia.
 
Tuzidi kuomba sana lakini lazima tuanze kubadilika sisi wadogo huku kusema kweli tunanyanyasana tukiweza hili basi twaweza kuwa wamoja wa kweli kuwatoa mijabali wa ufisadi
 
Ndio maana yake, tatizo ninaloliona mimi, kwenye Chadema, kuna wanachama, wafuasi, mashabiki na manazi wa Chadema, hivyo hata baada ya serikali kukubali matokeo na kuuondoa, manazi wa Chadema bado watashinikiza wanataka maandamano yao yawe pale pale!.

Mswaada ilikuwa ni moja ya hoja zitakazopingwa na kuzungumzwa kwenye maandamano na mkutano respectively. Kwahiyo kuondolewa kwakwe haina maana maandamano yasiwepo, bado wana wanatakiwa waelimishwe kuhusu ule mswaada na katiba kwa ujumla! Maandamano lazima yawe pale pale!!!!
 
Wapendwa,hivi mmeshagundua kwanini Wabunge wa Chama cha Magamba(Ccm)walikuwa wanashangilia baada ya Speaker Makinda kuahirisha swala la Muswaada wa Katiba?.Wamepata nafuu ya muda maana Chadema wangeandamana kuhusu katiba,Wao wangeonekana Hopeless mbele ya Jamii.

Pili,wangeshindwa kujibu maswali ya Wananchi wao pindi watakaporudi Majimboni kwao.Sasa niwaeleze,huu muswaada wa mapendekezo ya Madiliko ya Katiba,utakuja hivyo hivyo bila changes za Msingi zaidi ya Mabadiliko ya Lugha.Ccm wanataka watu wapunguze munkari kwa muda fulani ili wapate wasaa wa kuzunguka Mikoani na kuzungumzia issue zao za kujivua gamba na kurudisha imani za watanzania kwao,then kama siyo Bunge la June,basi ni la October,kilekile kinarudi.

Tuombeane uzima
 
Nimesadiki maneno ya Baba wa Taifa miaka kadhaa kwamba Tanzania kuna chama kimoja tuu cha upinzani kinachoweza kuleta mabadiriko vingine ni mamruki, nina amini kwa asilimia 100 kwamba in absence of CHADEMA muswada ungekuwa tayari umepita sasa. VIVA CHADEMA, VIVA JF, VIVA WATANZANIA WAPENDA MABADIRIKO.
Siyo kwamba ungepitishwa hata huo mbovu usingetengenezwa. CHADEMA walilazimisha CCM kuimba wimbo wa katiba na sasa wanawapa maelekezo ya jinsi ya kuutengeneza. CCM ime prove kwamba haiko makini na imekurupuka kwasababu ya pressure ya CHADEMA na peoples power. Katika muda mfupi CHADEMA imeweza kuiamsha serikali iliyolala usingizi angalau wamekumbuka kufungua macho japo bado wako kitandani.

Shime watanzania monotony kwenye siasa ni hatari sana; hivyo tusikubali kurubuniwa tena upinzani lazima uwepo ili kukifanya chama chochote tawala kiwe watumishi halisi wa mabosi wao yaani wananchi. Thanks CHADEMA. And my credits goes to mwenyekiti na viongozi wote waandamizi wa CHADEMA kwakutimiza ahadi yao kuwa kama serikali ikiondoa mswada nao watasitisha maandamano. Nimemsikia mwenyekiti akitoa maelezo kuwa wamesitisha maandamano. Hii ni muhimu kwani mnajenga uaminifu kwenye public ambayo itajenga imani ya wengi na kuona kuwa hamfanyi ushabiki bali siasa iliyotukuka.

CCM mjifunze na ninyi kuwa wakweli siyo mnakuja na matamko mia kiasi hatuelewi nani anasema kweli na nani ni mwongo as far as katiba issue is concerned. Rais alisema katiba mpya; waziri anasema hatuna fedha; mwanasheria anadai hatuhitaji katiba mpya ila marekebisho sasa hapo nani mkweli na yupi ni mwongo?
 
I just commented;

Kuna trend naiona kwa sasa, vitu wanavyopanga kufanyia maandamano CDM vinafanyiwa sarakasi haraka. Ni vema waendelee kuwa wanafanya hivi, ni vema kwa ustawi wa taifa letu.

Kwa mara ya kwanza, nawapongeza CDM kwa kusababisha serikali kuwa inachukua maamuzi haraka

Hii ndio maana ya kuwa UPINZANI na system ya Demokrasia! Taratibu Chadema wanabadilisha nchi wakiwa Wapinzani huku wamebeba sauti ya wengi!! Ni lazima wapewe hongera!
 
Back
Top Bottom