Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,050
- 144,458
Katika hali isiyo ya kawaida,Spika Makinda leo hii asubuhi wakati wa mjadala wa wizara ya fedha alisifu mchango wa mh.Kafulila alipochangia katika bajeti ya wizara ya fedha.
Kilichotokea ni kuwa muda wa mh.Kafulila kuchangia ulikuwa umeisha ila spika alikuwa amapetiwa kuangalia muda na hivyo Kafulila akaendelea kuchangia kidogo huku muda wake ukiwa umeisha.Baaada ya spika kugundua kuwa muda wa Kafulila umekwisha na sijui ilikuwa ni baada ya kushituliwa na wasaidizi wake au ni yeye mwenyewe tu alisema maneno matamu ya Kafulila yamemfanya apitiwe kuangalia muda.
Ni kweli leo Kafulila alifunguka kwa kiasi kikubwa kwa kuiponda serikali kwa kushindwa kuhakikisha makampuni mengi ya kibiashara yanaingizwa katika list ya Dar-es-salaam Stock Exchange(DSE) na hivyo kukwepa kulipa kodi na hivyo serikali kupoteza mapato. Kafulila alieleza kwa kirefu na kwa kutoa mifano ya makampuni kama vile airtel n.k yanavyoibia serikali kwasababu tu hayajaorodheshwa katika orodha hiyo ya DSE huku akiishushia lawama nzito serikali kwa uzembe huu.Mh.Kafulila aliisifu kampuni ya bia ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa Dar-es-salaam(DSE) kwa kulipa kodi kubwa serikali licha ya serikali kuwa na hisa ya asilimia 4 tu huku kampuni ya airtel ambayo serikali ina hisa ya asilimia 40 ikilipa kiasi kidogo cha kodi serikalini.Kafulila ameishangaa serikali ni kwanini makampuni mengine hayaorodheshwe katika list hiyo ya DSE.Mh.Kafulila amedai kuna watu wanafaidika na uzembe huu na ndio mana makampuni hayo hayaorodheshwe katika list ya DSE.
Mchango huo wa Kafulila ndio ulimfanya spika ajisahau kuangalia muda na kukiri kuwa Kafulila alikuwa na maneno matamu ya kumsililiza.