Spika awauliza mawaziri kwa nini wanapeleka miradi kwa wapinzani wakati hawaungi mkono bajeti

Jenista kapiga swali la msingi sana hawa wabunge wanaopinga bajeti wasiruhusiwe kabisa kuuliza maswali yakimaendeleo kwakuwa hawataki maendeleo.
Mkuu maana ya kura ni ipi?? Hivi demokrasia maana yake ni nni?? Watu hawapingi maendeleo ila kuna vitu vichache kwenye bajeti wanapinga sasa unapogeneralise kuwa wanapinga una maana gani??? Yaani zitto alikataa bajeti ya wizara ya maji kwa kuwa imepunguzwa bajeti hivo basi na yye asipelekewe maji kigoma??? Na wala asiulize swali kwenye bunge kuhusu maji???

Kumbuka bajeti ikipitishwa inahesabika ni bunge zima irrespective ya nani kakataa nani kakubali sasa kma kisheria ni bunge limepitisha ni wajibu wao kuisimamia serikali kwenye utakelezaji wa kilichopitishwa

Kma mnataka ipitishwe tu basi isiletwe bungeni maana haina maana kabisa
 
bado tunasafari ndefu san kama waziri anaweza omba muongozo wa namna hyo, upinzani wanapinga bajet kwa sababu inamapungufu wangetaman yabadilishwe lakini kwasababu kura za ndio simekuwa nyingi lazima ipite,sasa haimanishi kwamba wao hawatahusika kwenye mgawanyo,nin sas maana ya kupiga kura
 
Namuunga Mkono wasipeleke,ila kwa masharti kwamba wawaambie watanzania kwanini Serikali haitapeleka Pesa za maendeleo huko.Maana huwezi kusema ndiyo kwenye Bajeti unayojua haitekelezeki na inamuumiza mtu wa kawaida.

Ni vyema wakasema Bajeti hii ni kwa ajili ya wanaCCM tu,na kodi zitolewe na wanaccm tu.Ili wale tusio wanaCCM tutoe kodi kwenye maeneo yetu ili kujiletea maendeleo.Mbona tunaweza bila hata hiyo pesa ya serikali?

Ha ha ha, kwenye issue ya kodi ni pengine hapo mkuu.
 
Hata Mkapa aliwahi kusema hatapeleka pesa ya maendeleo kwenye majimbo ya wabunge wa upinzani.

Jk ndio aliachana na utaratibu wa kutopeleka Huduma za Maendeleo Maeneo waliyomkataa, naona Awamu ya Tano inaanza ya Mentor wake wa Awamu ya Tatu
 
Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewashangaa mawaziri kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya upinzani wakati wabunge hao wamepiga kura ya hapana kwenye bajeti ya serikali

Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Mbeya mjini Sugu kuhoji juu ya maelekezo ya awali aliyoyatoa juu ya watakaopiga kura za hapana, ndio na ku abstein


Jamani wanasheria kamata huyu msukule wa kigogo haraka sana ana mpango wa kupeleka nchi jahanam huyu!!
 
Jk ndio aliachana na utaratibu wa kutopeleka Huduma za Maendeleo Maeneo waliyomkataa, naona Awamu ya Tano inaanza ya Mentor wake wa Awamu ya Tatu
kama hawatapeleka miradi ya maendeleo pia tra waache kukusanya kodi kwenye majimbo hayo. ni uvunjaji wa katiba ya nchi. viongozi wetu wakumbuke waasisi wetu walitumia nguvu kubwa kujenga umoja wa taifa letu.
 
Kwani huko inakopelekwa wanaishi wapinzani peke yao au hao mawaziri wanatumia pesa zao za mfukoni na maendeleo wanapeleka kama sadaka? Huko yanakopelekwa wananchi hawalipi kodi? Na kwanini apingane na mwenyekiti wake anayesema hana chama wala ubaguzi wowote kwenye maendeleo?
 
JUZI; ACACIA hawa ni wezi, hawana leseni ya kuchimba madini nchini, hawana usajili, hatuwezi kuwalinda kwa askari wetu wezi wanaotuibia hawa.., hakuna mchanga kutoka nje.., ni wezi.

JANA; mimi kama mbunge wa eneo hilo, sasa natoa Rai kwa wananchi wangu, kuhakikisha tunazuia hawa wezi wa ACACIA wasituibie tena, tunakwenda kuzuia madini uetu yasisafirishwe.

LEO; HAPANA.., huyu mbunge ni mchochezi.., akamatwe na aunganishwe kwenye watu wenye vurugu, anahatarisha usalama wa nchi, anawasumbua wawekezaji.., akamatwe!!

#My_Take; Muombe Mungu kila siku.., usipewe ubongo na akili kama za ndugu zetu wa CCM.., ni laana, sasa ndugu zetu ndio wamebeba tafsiri sahihi ya neno "matumizi mabaya ya akili za binadamu", hawajui hata wanataka nini, kama bendera kavu tu, wanapepea!
 
Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewashangaa mawaziri kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya upinzani wakati wabunge hao wamepiga kura ya hapana kwenye bajeti ya serikali

Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Mbeya mjini Sugu kuhoji juu ya maelekezo ya awali aliyoyatoa juu ya watakaopiga kura za hapana, ndio na ku abstein


UBAGUZI! UBAGUZI! UBAGUZI!
Leo mtabagua majimbo ya upinzani mkimaliza hapo hiyo laana haitaishia hapo itaendelea kuwatafuna mtaanza kubagua hata makabila mwisho mtajibagua wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama.
Watanzania hatujazizoea kauli kama hizo kutoka kwa viongozi wetu.
 
Muoneeni hatuna. Haelewi maana ya Bunge na pia haelewi maana ya kidemokrasia. Kwa mtindo huo huo mikataba mibovu ya madini na gesi ilisainiwa
 
Mr.Job Ndugai is the worst ever speaker of Tanzania parliament since independency.
Ni spika anyeongoza kwa maslahi ya chama na ni mtu wa kulipuka,hana uvumilivu.
Spika Job anaongoza bunge bila kujali kanuni za kuendesha bunge,ana adhibu wapinzani kwa hisia na hasira kwa mambo madogomadogo
Nadhani anaongoza kwa maelekezo maalum kutoka pande za Feri
\##Spika acha upendeleo,endesha bunge kwa maslahi ya nchi.
/##Spika jiamini,usiongozwe na mwingine yule.Asikwambie cha kufanya maana wewe humwambii cha kufanya
 
Back
Top Bottom