Spika awauliza mawaziri kwa nini wanapeleka miradi kwa wapinzani wakati hawaungi mkono bajeti

Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewashangaa mawaziri kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya upinzani wakati wabunge hao wamepiga kura ya hapana kwenye bajeti ya serikali
Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Mbeya mjini Sugu kuhoji juu ya maelekezo ya awali aliyoyatoa juu ya watakaopiga kura za hapana, ndio na ku abstein

Basi nchi igawanywe
 
Nakodi ya hayo maeneo wasi kusanye mfano dsm, si iko upinzani wasilete miradi na kodi wasikusanye pia!!
 
Viongozi wengi wa CCM wapo very average Vichwani,
Ndio maana wabunge wengi wa CCM siku ile bajeti inasomwa walikurupuka kushangilia kufutwa Load License bila kufahamu kuwa imehamishiwa kwenye mafuta hivyo hata anaewasha Generator atalipia..

Na kuthibitisha hili angalia baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Mikoa wa awamu hii wanavyofanya Maamuzi,

Au angalia hata mikoa mingi ambayo CCM hupata kura nyingi Kama sio kupita bila kupingwa, utagundua walio wengi ni wenye Vipato Duni, Wenye Elimu Duni na Wazee. (Insecure groups)

Utafiti wa Twaweza uliofanywa hivi Karibuni una mengi ya Kutueleza.
Kumbe siku izi utafiti wa Twaweza mmeanza kuukubali...
 
Kama ni kweli kasema....basi majimbo ya upinzani yasilipe kodi watafute maendeleo yao wenyewe.......wajitenge...
Duuhh .........hatari huwa ina anza hivi.
Naunga mkono hoja!! Wananchi ambao wabunge wao wameikataa bajeti wasilipe kodi na wapange mipango yao wenyewe bila serikali kuwaingilia!!
 
Inawezekana Chadema walikuwa sahihi na Sera yao ya utawala wa majimbo ili sehemu kubwa ya raslimali ndani ya jumbo zitumike Kwa maendeleo ya jumbo Kwa sasa miradi ya maendeleo inategemea maamuzi ya kisiasa na watu wachache tu
 
Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewashangaa mawaziri kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya upinzani wakati wabunge hao wamepiga kura ya hapana kwenye bajeti ya serikali
Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Mbeya mjini Sugu kuhoji juu ya maelekezo ya awali aliyoyatoa juu ya watakaopiga kura za hapana, ndio na ku abstein

Pelekeni Mswada bungeni serikali isikusanye kodi kutoka kwa wapinzani!.
 
Yaaani mpaka sasa nashindwa kuamini kwamba viongozi wajuu wametamka hivyo.....Hatari kubwa saana.Sijui watajivuwa vipi maneno hayo.Niwaombe viongozi mengine musiyatamke hadharani yataleta matatizo
 
Jenista kapiga swali la msingi sana hawa wabunge wanaopinga bajeti wasiruhusiwe kabisa kuuliza maswali yakimaendeleo kwakuwa hawataki maendeleo.
Hebu jitahidini kuwa mnatumia akili hata kidogo tu. Serikali inatengeneza mpango wa matumizi ya wananchi kwa niaba yao. Inapeleka bungeni kuidhinishwa hayo matumizi..!! Huo ni utaratibu ambao tumejiwekea kwamba serikali iweke mpangilio wa matumizi yetu na wabunge wetu wakaidhinishe au kukataa hayo matumizi.

Wabunge wakiungana na kuyakataa hayo matumizi,maana yake wabunge wameikataa serikali kwa kuweka mpangilio wa matumizi usiofaa. Na kwa mujibu wa sheria zetu,baraza la mawaziri litavunjwa na bunge litavunjwa tunarudi kwenye uchaguzi.

Mpangilio huo wa matumizi ukikubaliwa na wabunge wengi,inaenda kutekelezwa kutokana na mpangilio uliowekwa na vipaumbele vyake. Hapo kwenye kupiga kura tunaangalia mambo mawili tu,kura za hapana zikishinda serikali inaanguka na kura za ndiyo zikishinda serikali inaenda kuisimamia hiyo budget.

Huu ujinga unaotaka kuletwa na akina ndugai,ni ujinga uliopitiliza kiwango cha ujinga. Kuna wakati kiongozi km spika wa bunge anapoongea ujinga wa kiwango hiki unajiuliza alifikaje pale.

Ukisema hutaki kupeleka huduma ktk hayo majimbo yenye kura za hapana,maana yaje unataka huyo mbunge akawaambie pia wananchi wake hakuna kulipa kodi yoyote kwa kipindi hicho kwa sababu haitamrudia.

Leo ndiyo nimeamini kuwa "Duniani kuna watu wa aina mbili tu wasioweza kubadili mawazo yao; Mpumbavu kuliko wote na mwenye Hekima kuliko wote."
 
Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewashangaa mawaziri kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya upinzani wakati wabunge hao wamepiga kura ya hapana kwenye bajeti ya serikali
Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Mbeya mjini Sugu kuhoji juu ya maelekezo ya awali aliyoyatoa juu ya watakaopiga kura za hapana, ndio na ku abstein

Halafu analalamika Wapinzani washiriki futari yake. Kimsingi huyu bwana ana roho ya ubaguzi. Sielewi kwanini Tanzania kupitia utawala huu ubaguzi unafanywa na viongozi
 
Basi zipigwe kura za siri. Yaani unawapa watu options tatu ili wachague moja kwa mujibu wa kanuni, halafu unataka wote wachague unayoitaka wewe kinyume na taratibu - mtu wa hivi lazima atakuwa na uelewa mdogo sana wa misingi ya demokrasia ya kweli na ni mvunja taratibu.
 
Ndugai aache ujinga wake wasipopeleka maendeleo huko si wanawaumiza wananchi na si mbunge inabidi spika awe anafanyiwa kipimo cha mataputapu hata kabla hajaanzs vikao

Kwani tafsiri ya matokeo ya hizo kura ni ipi? Je, wale wananchi milioni sita ambao hawakumchagua Rais Dr. Magufuli ambaye anahubiri maendeleo ni ya wote hawaongozwi na yeye? Misingi ya demokrasia ni kila mtu kuwa na haki ya kuchagua kinachomfaa na mara kura zikipigwa basi anakuwa tayari kwenye mkataba wa kukubali na kuheshimu matokeo ya aina yoyote.

Ma-profesa na madokta wa political science wanatakiwa kutoa semina kwa wabunge juu ya suala zima la demokrasia kwa mapana yake.
 
Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewashangaa mawaziri kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya upinzani wakati wabunge hao wamepiga kura ya hapana kwenye bajeti ya serikali
Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Mbeya mjini Sugu kuhoji juu ya maelekezo ya awali aliyoyatoa juu ya watakaopiga kura za hapana, ndio na ku abstein

Bora wasipeleke kabisa ili majimbo ya upinzani wazidi kujitegemea. Maendeleo ni hulka ya watu. Huwezi pelekea watu maendeleo kama wenyewe hawayataki. Hii hoja naiunga mkono na miguu kwa sababu mwanadamu hajawahi kuishiwa mbinu za kukabili mazingira yake kutokana na yanayomkabili.

Wasipopeleka hayo maendeleo hao wananchi waliochagua upinzani watayaleta wenyewe.

Hata kuchagua wapinzani ni maendeleo. Inahitaji IQ kubwa sana kukataa mfumo uliostawisha umasikini nchini kwa miaka zaidi ya 50.
 
Utasema hayo majimbo yenye wabunge wa upinzani ndiyo siyo ya watanzania, ccm wanajifanya wanajua umoja lakini ni namba moja kwenye kujitenga. Heshima imeshuka kwa huyu
 
huyu spika something wrong kichwani kwake,mbona kodi kutoka majimbo yanayoongozwa na upinzani serikali kuu inakusanya?,huyu spika anaigawa nchi yetu ,shame on him ,na mbaya zaidi eti he is my speaker,pumba tupu.aheshimu na asimamie sheria za bunge sio za vyama vya kisiasa.
 
Jenista kapiga swali la msingi sana hawa wabunge wanaopinga bajeti wasiruhusiwe kabisa kuuliza maswali yakimaendeleo kwakuwa hawataki maendeleo.

Kwahiyo na wale ambao hawakumchagua Rais anayekuwa madarakani hawatakiwi kuhoji au wanatakiwa kuhama nchi kabisa? hivi mnajua maana ya kura na maana ya maamuzi wa wengi?
 
Kama ni kweli kasema....basi majimbo ya upinzani yasilipe kodi watafute maendeleo yao wenyewe.......wajitenge...
Duuhh .........hatari huwa ina anza hivi.
Mkuu naona Spika ametoka kwenye njia kuu.
Anafanya kazi ya kuchonganisha ndugu bila kujua,mwisho wake ni utengano,atatuletea Biafra.Hata mbuyu ulianza kama mchicha.
 
Back
Top Bottom