Spika aongezewa ulinzi

Maelezo yako hayana uhusiano na topic ya thread. Tusitoke nje ya mada. Hayo yako unaweza kuyaanzishia thread, tutakuja kuchangia...

1. Unaweza kueleza kwanini chadema wanalitia gharama taifa?

2. Umetumia maneno kulitia gharama taifa unaweza kutuwekea tafsiri sahihi ya maneno hayo na yalilenga nini?

Ukiweka maelezo hayo tutaendelea mkuu.
 
Its cheaper akijiuzulu na achaguliwe ambaye watu wanampenda.., Huu ni ufisadi wa kufuja mali za watanzania
 
1. Unaweza kueleza kwanini chadema wanalitia gharama taifa?

2. Umetumia maneno kulitia gharama taifa unaweza kutuwekea tafsiri sahihi ya maneno hayo na yalilenga nini?

Ukiweka maelezo hayo tutaendelea mkuu.

Mkuu, its simple mathematics - chadema wamesema maneno ambayo yamewafanya wananchi wafanye mambo yaliyojenga hofu juu ya usalama wa spika. Matokeo yake serikali inaingia gharama kuhakikisha usalama wa spika.
Bado unahitaji maelezo zaidi?
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

Angekuwa hakeli asingetumiwa hizo meseji, but madam spika anabore sana kwa ubabe wake wa kutetea uozo na kuwafanya wa TZ wajinga . Tuache unafiki!
 
Kama spika anaamini alichokuwa anafanya bungeni ni sahihi hana sababu ya kuhofia usalama wake maana Bwana atamlinda. Maana bwana asipoilinda nyumba, wote wakeshao wafanya kazi bure.
 
Mkuu, its simple mathematics - chadema wamesema maneno ambayo yamewafanya wananchi wafanye mambo yaliyojenga hofu juu ya usalama wa spika. Matokeo yake serikali inaingia gharama kuhakikisha usalama wa spika.
Bado unahitaji maelezo zaidi?

1. Unaweza kuorozesha hayo maneno na hatari zake?
 
kama madam spika anajiona anatenda haki wasiwasi wa nini?
roho inamsuta sasa.anajutia kosa lake la kupindisha sheria.
kwa hatua waliofikia watanzania ya kumtukana kama ni kweli basi ajue hatendi haki.
hata hivo watanzania hawana muda wa kulipiza kisasi ujumbe alishaupata ajirekebishe.
meseji senti.
 
Dhambi ya unafiki na uzandiki itamtafuna makinda hata atajuta kupewa uspika na mafisadi.
 
Hata waongezewe ulinzi wa kijadi, kamwe hamuwezi kuzuia wenye HAKI kudai haki yao! Dhulma mnayoifanya kwa Watanzania itawafisha mkiwa dhalili...Namba zipo shime wadau tuendelee kuwa tumia sms, Mimi nimewatumia huu ujumbe muda si mrefu:- " Ewe Anne Makinda/Job Ndugai...Kwa Maslahi Mapana ya Nchi yetu, Watu Wetu, Watoto wetu na Vizazi vyetu vijavyo NA Kwa Kulinda Heshima ya Bunge letu...Nawashauri Mjiuzulu nyazifa zenu zote za kuliongoza bunge letu. Mmedhihirisha kuwa Hamtendi HAKI wala Hamtangulizi Maslahi ya Watanzania Mbele bali Mpo Kuitumikia kikundi kidogo cha wachache wenye KUFISADI mali za Watanzania! Mshahara wa DHAMBI ni Mauti, Bado mna nafasi ya kutubu na kuwaomba radhi Watanzania, Hima mfanye haraka ikiwa ni pamoja na kuweka hadharani hoja zote zenye maslahi mapana kwa watanzania mlizozuia KABLA LAANA ya WATANZANIA hazijawashukia"...
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

Acheni uzushi CDM imefanya lini mkutano Mwembe Yanga? mwandishi kanjanja.............. na mhariri kanjanja......!!!!!!
 
Another example of physical thinking rather than brain thinking.

Kwanza, nani ana uhakika kuwa spika na naibu wake wametukanwa?[

Ni matusi gani aliyotukanwa?

Watu wanabwabwaja huku hawajui kama ni kweli spika ametukanwa au hajatukanwa. Hata Mnyika alipotamka kuwa, 'Chanzo cha matatizo mengi ya nchi hii ni kuwa na Serikali na Rais dhaifu', wapo wengi waliosema kuwa ametukana. Lakini je, maneno haya ni tusi? Kama tungeelezwa hizo message zimesema nini, huenda wengi wetu tungeshangaa kwa vile kinachotajwa kuwa ni matusi inaweza kuwa ni kuambiwa ukweli jinsi spika na Naibu wake wanavyofanya kazi. Kama ni matusi kweli, wapeleke mahakamani, wanangoja nini? Namna nyingine hizi ni hadithi za alinacha.


Nilipokuwa pale chuo kikuu wakati wa utawala wa Mwinyi, chuo kilifungwa kwa maelezo kuwa sisi wanachuo tumemtusi Rais matusi ya nguoni (kwa mara ya kwanza ndiyo hilo neno 'matusi ya nguoni' lilisikika kwenye msamiati wa kiswahili) lakini ukweli ni kuwa hakuna mahali iwe kwa maandishi au kauli tuliona au kusikia hayo yaliyotajwa kuwa ni matusi ya nguoni. Nakumbuka maandishi pekee ambayo yalichukuliwa kuwa ni matusi kwa Rais ni bango liliandikwa kuwa: Jangala anataka kuendesha mambo yake kwa mila na desturi (wakati ule kulikuwa na mchezo wa Kibuku uliokuwa na mwigizaji maarufu Jangala akimlazimisha mtoto wake aitwaye Kidole kuwa ni lazima amwoe binti mmoja hapo kijijini kwa sababu ni mila na desturi mtoto kutafutiwa mchumba na wazazi wake), Mwinyi anaendesha mambo yake kwa mila na desturi (Rais Mwinyi alidai kuwa aliwashauri wanachuo kuingia darasanai lakini wao wakasema kuwa ushauri siyo lazima ukubaliwe, wanachuo walisahau kuwa kwa mila na desturi za kiafrika ushauri kutoka kwa mkubwa kwenda kwa mdogo ni amri, na kutoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa ni ombi), hivyo JANGALA = MWINYI. Maneno haya yalitafsiriwa kuwa ni matusi ya nguoni kwa Rais, chuo kikafungwa. Ikaundwa tume ya jaji kuchunguza utovu wa nidhamu uliofanywa na wanachuo kwa Rais. Taarifa ya tume ikasema kuwa serikali ilifanya makosa na wanachuo hawakuwa na hatia, chuo kikafunguliwa, hakuna hata mtu mmoja aliyeshtakiwa kwa kumtusi Rais maana hakukuwa na tusi.

Sasa kwa Makinda, huenda ikawa ni namna hiyo hiyo. Subirini mwone kama kweli kuna kesi yoyote ya matusi kwa spika itafunguliwa, nasema hakuna kesi ya matusi kwa Spika itakayofunguliwa mahakamani zaidi ya hizi porojo za mitaani.

Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
 
Makinda ajilaumu mwenyewe kwa tamaa yake ya kukubali kutwishwa zigo ambalo alijua dhahiri haliwezi. Nafasi ya spika haikuwa chaguo lake na ni wazi kuwa alijua haiwezi ndiyo sababu alikuwa anagombea nafasi ya naibu ila kuna watu walimdanganya ili waweze kupenyeza mambo yao ya kifisadi na kulivuruga bunge kwa manufaa yao binafsi.
 
Mkuu samahani, lakini naona unanirudisha hatua mia nyuma. Hilo naomba unisamehe sitakujibu.

Mkuu niliandika hivi, nataka kuweka kumbukumbu sawa.


Ukanijibu hivi

Maelezo yako hayana uhusiano na topic ya thread. Tusitoke nje ya mada. Hayo yako unaweza kuyaanzishia thread, tutakuja kuchangia...

Nikakuulia hivi

1. Unaweza kueleza kwanini chadema wanalitia gharama taifa?

2. Umetumia maneno kulitia gharama taifa unaweza kutuwekea tafsiri sahihi ya maneno hayo na yalilenga nini?

Ukiweka maelezo hayo tutaendelea mkuu.

Ukanijibu hivi

Mkuu, its simple mathematics - chadema wamesema maneno ambayo yamewafanya wananchi wafanye mambo yaliyojenga hofu juu ya usalama wa spika. Matokeo yake serikali inaingia gharama kuhakikisha usalama wa spika.
Bado unahitaji maelezo zaidi?

Nikakuuliza hivi

1. Unaweza kuorozesha hayo maneno na hatari zake?

Umejibu hivi

Mkuu samahani, lakini naona unanirudisha hatua mia nyuma. Hilo naomba unisamehe sitakujibu.


Tuendelee

Nimekurudisha nyuma kwasababu yote haya yanatokea kwasababu za upumbavu wa spika, Naibu spika na baadhi ya wabunge wa ccm

1. Kushabia elimu ya kipuuzi, Mbatia amepeleka jambo la msingi ushabiki unaingia on the expense ya walalao kuikosa haki

2. Katika bunge hilohilo ushabiki unaingia wanajadili mambo kwa mkutadha wa kuwachonganisha rai kupitia mahakama lengo nini wagawe uwatawale kupitia chuki za kidin.

3. Ni katika bunge hili bunge lilopita huko nyuma, chini ya makinda hoja za afya zilipigwa chini bungeni, matokeo yake ccm ikamtumia Rama Igondu kumzuru Dr ulimboka, je maslahi ya afya yameathilika kiasi gani chini ya makinda, ndugai, Pinda, W. Lukuvi na Mtembezi?

huwezi kuliona hili! kwasababu umevaa miwani ya uccm.

4. Je sio chini ya makinda, Pinda na Mtembezi tumekuwa tunapigwa danadana kuhusiana na walioficha fedha uswis? huoni relation hapa mwana maheabu this is easy either from logic or relation, by far you may use projection if you like.

5. Kuhususiana na mikataba ya hovyo kwanini mikataba ya gesi kupitia bunge hilihili inawekwa chini ya meza kwa maslahi ya nani? Niliongezea ya KINANA na Richmond nk kwasababu by histogram or normal distribution curve ccm makes such a function to exist and will never be separated unless the reality is revealed. (data can be collected and ploted conerning mafisad under CCM ruling and The parliment under Madam makinda)


a) Nilikuwa naakuuliza maswali kukuweka sawa kwamba upumbavu wa ccm kumtumia makinda na Ndugai ndiyo wanalisababishia hasara taifa "kwa msemo wako walisababishia gharama"

b) Makinda anaongeza gharama zaidi za ulinzi, kwasababu ya upumbavu wake kukubaali kutumika bila kuifuata kweli.

c) Sasa ulitaka wananchi wafanyaje pale wanapoona wazi Spika na Naibu wake wanapindisha sheria na kuwaacha wananchi waonekane mbumbumbu?

Hiyo ndiyo sura halisi ya maswali yangu na mtazamo wangu chini ya hoja Spika aongezewa ulinzi swali kwanini hayo ndiyo majibu. Tumia akili zako vizuri kupambanua mambo

-Sasa nataka na wewe utuwekee hapa hayo maaneno waliyoyasema chadema na hatari yake
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
acha kufikiria kwa kutumia masuburi kenge wewe! Unajua nini maana ua ujumbe? Ukilima ndimu utavuna ndimu hata kama utaziwekea mbolea na kuzimwagilia, hauwezi kuvuna maharage. Ndicho Makinda na magambayenu mnachovuna:majani7: Namba za spika zipo mtandaoni tele, na yeye sio mtu wa ajabu kiasi kwamba namba zake asiwe nazo mtu ni pandikizi la ccm kumnyima sita uspika na sasa wamemwambia azime hoja za upinzani bila kujua ndo wanamwaga petrol panapofuka moshi:majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7::majani7:
 
Na bado wabadilishe hata makazi yake yawe London, Huna haja ya hayo yote ulinzi, kubadili namba, kuongeza walinzi, nadhani wangemwacha tu maana kama limepangwa lolote kutokea litatokea tu. wangapi wana hadi bullet proof kwenye magari yao wanakufa? dereva wake akiligongesha walinzi watamuokoa? anakuwa mkimbizi ndani ya nchi yake, haishi kwa amani kisa zawadi ya uspika? Aendelee tu, hoja anazozizima bungeni ni kwa maslahi ya watanzania sio wabunge wa upinzani, au kwa kuwa maji yapo makazi yao dar ndio suala la maji wanalifuta, elimu watoto wao wanasoma nje hivyo elimu ya hapa haina msaada kwao? Watoto wetu wawe kama Mulugo anayesema tanzania ni muungano wa visiwa vya zimbabwe na pemba?? Hii ndhio tanzania aitakayo makinda, ndugai? Haya yote yana mwisho na mwisho upo karibu.
Nashauri JWTZ watumike kumlinda, mbele na nyuma ya gari yake waweke vifaru na pia helikopta juu iwe inamlinda na pia apatiwe ka room pale ikulu awe anaishi. Polisi wanakunywa viroba wanaweza kujisahau mama wa watu akauliwa. pia wamfunge cctv camera ziwe zinaangalia wanaomfuata ni kina nani
 
"Mungu asipoulinda mji waulindao wakesha bure" Spika Anna Makinda hata angelindwa kama kobe ndani
ya gamba kama ni madhara atayapata kwa sababu ya laana za watanzania wanyonge kwa kuwatendea yasiyopaswa
kufanywa na mwanadamu tena mama.Lakini akitenda mema kwa watanzania hawa hahitaji ulinzi wowote wa mwanadamu
Mungu mwenyewe atamlinda"
 

Mkuu wewe ni GT big up"
nakuongezea hapo Kinana analitia hasara taifa akiwa anajua kabisa madhara ya kutumia dola badala
ya Tzs kwenye malipo yetu ya ndani,kupitia kampuni yake ya shipping line na yard ya magari ya TALL
wanacharge malipo yote kwa kutumia dollar badala ya Tshs"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…