Spika aongezewa ulinzi

Shule bwana sasa hao wanamtumia vitisho wakati namba zao za simu wamezisajiri wakikamatwa wakabinywa korodani kwa plais wanabaki wanalia lia
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

Kwani kusema mtumie ujumbe speaker ni kusema kamtukane speaker, viongozi waache ulevi wa madaraka, hatuko kwenye enzi za chama kushika hatamu!
 
Bado wanazidi kutumia kodi zetu vibaya,upuuzi huu unaweza kufanyika Tanzania tu.

Lakini mda si mrefu Haki itashinda.
 

Physical confrontation kama ipi washike mapanga? kama kuandamana wameandamana, wamehudhuria mikutano na wamechukua hatua za kidemocrasia kuelezea kutokuridhika kwao na matendo ya maspeaker ulitaka wananchi wafanye nini zaidi!
 
kwangu mimi hii haina tija yoyote ila naona kama wanataka kufanya iwe habari kuu ili tusijadili mambo ya msingi
 
Anachotakiwa nikuomba radhi tu na kuamua kujiuzuru basi na hizo meseji zitakoma.NI kweli wananchi wanahasira sababu pengo la walionacho na wasionacho limezidi kupanuka huku wachache na familia zao wakifaidi matunda ya nchi na mbaya zaidi basi hao wachache wakumbuke basi huku pembeni kuna mwananchi ambaye hata kula yake hana uhakika nayo.

Ardhi zinatolewa holela kwa wawekezaji kutoka ughaibuni ilhali watanzania wanahitaji ardhi yao.Spika angekuwa "FIRM" na mkali kwa serikali yake iliyomuweka madarakani basi CHADEMA wangekuwa wala siyo tatizo na wananchi wangemsupport.

Aombe radhi tu wananchi halafu atimue vumbi.
 
Tumemtisha kidodo tu ameshtuka -- ha ha ha

mama hatuwezi kukudhuru na wala hatuna mpango huo kabisa cha msingi tunataka hicho kiti uwaachie wanaoweza kukimudu.
 
Ufisadi mwingine huo!pesa za kubadilisha hayo magari wamepata wapi?yaan magamba bwana!wanatumia vibaya pesa za serikali,we ngoja tu dawa yao inachemka!
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
'unawashwa washwa' nukuu ya Mabumba
 
CHADEMA wamefanya ka maana sana ili ajue ni namna gani watu wanakerwa na utendaji wake.

Hilo bunge si mali yake wala si mali ya ccm.Na watambue kuwa bunge hilo linaendeshwa kwa kodi zetu.
 
 
Kwanza ajiulize kwanini apewe ulinzi zaidi? kwa kosa gani katika taifa hili! kwanini watu zaidi ya 400 wawe na hasira naye?

Makinda atambue kuwa Nelson Mandela alikuwa gerezani kaburu akadhani yatakwisha.
Mondlane aliuawa Dar es salaam mreno akajua yatakwisha.

Siku zote na mahali popote imethibitika pasi na shaka kuwa nguvu kubwa duniani ni nguvu ya umma.
Hao walinzi hawana ulinzi wa maana, ulinzi wa maana ni yeye kujiuliza amefikaje hapo alipofikia mahali pa kutegemea kulindwa!

Ni wajibu wa makinda kujiuliza, hivi amewatendea wananchi kosa gani hadi ahofie kuwa huenda wanaitafuta nafsi yake?

Kwa ushauri wangu,
Makinda hakika hakuna tena ulicho nacho cha kulisadia taifa hili.
Bunge limekosa maana ya bunge na limekuwa kama kijiwe cha watu kukusanya mapato.
Umeshindwa kuliongoza bunge kama spika.

Mama Makinda, umepoteza role model kwa mabinti zetu, umefuta matumaini na imani juu ya uwezo wa akina mama.
Kibaya zaidi katika taifa masikini kama Tanzania kuendelea kuwa na wewe ni ni jeraha juu ya kidonda.

Kweli wananchi wana hasira dhidi ya uongozi wako. Njia iliyobaki ni wewe kujiuzulu.
Kujiuzulu kwako kuna maana kuu mbili.
1. Kulisaidia taifa maana wewe ni tatizo kubwa kuliko matatizo tuliyo nayo.
2. Ni kulinda heshima ya akina mama ambao bado tunaamini wana uwezo, kadri unavyoendelea kuwa Spika subra inatutoka na uwezekano wa kutofikiria mwanamke tena katika uongozi unazidi kuongezeka

Tunashukuru kwa utumishi wako wa kukaa bungeni kwa miongo kadhaa, tunakutakia mapunziko mema yasiyohitaji ulinzi.

Tunakushukuru sana kwani kwa kupitia wewe jibu la kwanini sisi ni masikini linapatikana kiurahisi.
Mama Makinda, hivi utavumilia aibu hii mbele ya taifa hadi lini ?
 
Ndugu Mingoi, wewe ndo mnazi wa kupitiliza, kwani anachokifanya spika na wasidizi wake hatuyaoni?kwahiyo wananchi wakimwomba aachia ngazi ni noma?kazi imemshinda kabisa ya kutetea maslahi ya taifa badala yake natetea maslahi ya MAFISADI. siku ya tukio Ndugai alisema watanzania mnaona wenyewe mtoe maamuzi sasa maamuzi ya mahakama kuu (UMA) ni waachie ngazi inakuwaje tena watunyime kuona bunge letu?wanachokificha nini? hizo wanazosema wabunge wengine wanatafuta umaarufu, kama ni umaarufu usiokuwa na tija kwa uma si uma utaona nyewe na kumdharau badala na kupata umaarufu? MAFISADI wanajua kabisa kwamba wanachikifanya CDM ni kwa masilahi ya UMA na uma ya watanzania watazidi kuwachukia na kuipenda CDM lakini suluhisho si kuturudisha enzi za ujima bali ni wajirekebishe wafanye mambo yote kwa maslahi ya uma. OTHERWISE HATA WAKIZUNGUMZA GIZANI TUTAPATA KWAMBA WAMEZUIA/WAMEPITISHA NINI KWA MASLAHI YAO.na tutazidi kuwachukia kupita kawaida. FANYENI KAZI KWA FAIDA YA UMA. Mama Makinda jiuzulu make si dhambi ni ushujaa kwani unafanya kazi za ccm na si za Taifa.
 

Mzee Mwanakijij

Para yako ya kwanza haina tatizo. Umesaidia kuweka vyema. Namba za viongozi wa umma, si siri ya vyumbani mwao. Ingawa pia kuna wakati mambo ya vyumbani mwao, mengine si siri zao pia. Zinakuwa mali za umma.Kwenye para yako ya pili, ikiachwa hivyo inaweza kuibua hisia kuwa hili jambo halikuwa na mpangilio. Kwa maana ya kwamba CHADEMA walikurupuka. Si kweli. Ulikuwepo ujumbe. Nakumbuka Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndugu Kabwe Zitto alivyokuwa akisisitiza na kurudia. Halikadhalika Ndugu Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini.

Wananchi wawapigie simu au kuwatumia msg Spika wa Bunge Anna Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, na waambiwe "umeshindwa kuendesha bunge...tunakutaka ung'oke. Ng'oka". Ujumbe ulipaswa kuwa na pressure ya kuwataka wawajibike. Siyo kuwambembeleza. Ndiyo maana ikasisitizwa lisitumike neno 'ng'atuka'. Hapana, bali 'ngoka, umeshindwa kusimamia na kuongoza bunge kwa maslahi ya wananchi'.

Unless kama unamaanisha kwamba CHADEMA wangeandika ujumbe kisha wausambaze kwenye simu za watu...vinginevyo there was a very clear, specific, standard, short and pointed msg for the wananchi to tell the number 1 and 2 in our parliament.
 
Ndio kosa la wanasiasa wetu wengi;
Huwaacha wananchi katika limbwi kubwa la sitofahamu;
Matokeo yake ujumbe uliokusudiwa haufiki;
Bali inakuwa fujo naam mchafugoke.
Tubadilike na Tujisahihishe.


Bazazi!

Sidhani kama ni sahihi kwa wanasiasa kuwaambia wananchi nini cha kumwambia Spika anayekandamiza demokrasia. Kuna haja gani kwa wananchi zaidi ya 500 kutuma ujumbe wa aina moja. Kwa nini nipoteze hela zangu kupiga simu au kutuma ujumbe kuongelea kitu hicho hicho ulichoongelea wewe?? Suala hili limemgusa kila mwananchi kwa namna tofauti na hivyo kila mtu anatuma ujumbe kwa jinsi alivyoguswa. Lazima muelewe kuwa hata sisi wananchi TUNAWEZA KUVUKA BARABARA bila kuongozwa na nyie wanasiasa na hatugongwi na magari. Nyie ni viongozi wetu, tupeni nyavu samaki tukavue wenyewe na sio kutupa samaki tule
 
Wakuu, hivi kiongozi wa umma unapokua hutakiwi na umma huo huo hivi njia sahihi ni kuongezewa ulinzi au kuachia ngazi? Wananchi hawakutaki halafu system inakutaka, mbona busara inaonesha tu wewe hutakiwi kwenye huo muhimiri! Achia ngazi mama, mwenye nchi yao hawataki uendelee kuongoza chombo chao, mbona rahisi tu, fanya kama alivyo fanya Mr. White Hair!
 
Kuishi kwa tension na kuzungukwa na mabunduki mda wote hiyo tu ni karaha katika haya maisha... Huyu mama akubali tu kuwa ametumika vibaya na katika hilo kachemka sana...Pole zake huko aliko....
 
Nilisahau hivi nilikua bado sijatuma msg yng kwa bibi kiroboto ngoja niongeze idadi iwe 401, mods alishanipa ban 2 tyms naomba nimrukie live. Yan huyu mama anatia hasira sana ngoja nkamfikishie mwenyewe machungu yangu, na namba ya dr kashilila katibu wa bunge, pls mwenye nayo waungwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…