tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,134
- 280
Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.
Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.