Spesheli Kwenu Wanaume..

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
17,520
2,000
Habari za usiku huu,

Rejea kichwa cha habari, leo hakuna mahaba. Lengo la uzi huu ni kuwapa faraja wanaume wote hasa wale ambao wanapitia kipindi kigumu kwenye maisha yao. Najua kuna wanaume ambao hawapitii au hawajapatwa na changamoto za maisha au ugumu wa maisha. Basi wewe mshukuru mola wako na endelea kutoa sadaka yasikupate yanayowapata wenzio.

Hii video hapa chini iwape faraja, angalia hilo gari ni Benz moja ya kampuni kongwe inayotengeneza magari ya kifahari duniani. Ukilitazama hilo gari linaonekana limechoka na kuchakaa. Lakini dereva na using wake hawajakata tamaa, angalia njia wanazopita ubovu wa barabara, lakini wako tuu. Wanabeba chepeo au spedi, mawe, mchanga vipande vya miti na vigogo ili kurekebisha njia safari yao iendelee.

Maana ya kuiweka hii video hapa ni kuwafikirisha maisha ni safari ukibahatika kupata mteremko well and good. Ukikutana na changamoto ndo upambane. Wewe kama mwanaume ndo kiongozi wa familia yako ya baba na mama na ndugu zako wakati huo huo ukija kuoa na kuwa na mke na watoto wote watakutegemea wewe. Sasa ikitokea ukikutana na changamoto za maisha halafu ukakata tamaa maana yake ndo mwisho wa familia yako ya wazazi na ya mkeo na wanao.

Kikubwa ujue kuwa wewe ni zaidi ya hilo Benz, unauwezo wa kuishi mazingira yeyote yale na ukapata ana na maisha na utasikia malango yako. Ila peke yako huwezi...... shirikiana na mkeo, wazazi wako, ndugu zako mliozaliwa tumbo moja, rafiki, wafanyakazi au wafanyabiashara wenzio kila mmoja kwa nafasi yake ili usilemewe na changamoto za maisha.

Chukulia mfano dereva wa hilo Benz angekuwa yuko mwenyewe asingekuwa mbali maana eneo la kuelekezwa wapi aelekeze tairi peke yake angeshaingia mtaroni. Kushuka kila saa kuweka mawe magogo na kuondoa vizingiti ili gari ipite angechoka na safari ingeishia njiani.Mwanaume Pambana Gangamala Pambana wewe ni Zaidi ya Benz.

Kasie Matata.
 

Attachments

  • File size
    10.2 MB
    Views
    42

Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,398
2,000
Hongera sana Madam kwa maneno ya kutia faraja na hamasa ambayo ni chakula cha akili kwa Wanaume wote, sio daily ni kuvisimanga viungo vya Uzazi Mara Vibamia, hujakaa sawa Mwanaume Mashine, ukigeuka huku Wanaume wananuka Mbupu, ilimradi kupeana karaha tu..,
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
17,520
2,000
Ujumbe mzuri,i hope utawapa tumaini wanaume wengi!

Natumai hivyo... pamoja na kuwapa tumaini watoke asubuhi na kupambana wasikubali kuwa hakuna ajira basi kushinda kutwa kuangalia telemundo.
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
17,520
2,000
Hongera sana Madam kwa maneno ya kutia faraja na hamasa ambayo ni chakula cha akili kwa Wanaume wote, sio daily ni kuvisimanga viungo vya Uzazi Mara Vibamia, hujakaa sawa Mwanaume Mashine, ukigeuka huku Wanaume wananuka Mbupu, ilimradi kupeana karaha tu..,

Asante kwa kushukuru, kiukweli hakuna anayependa kukosolewa na hata ikibidi basi mtu hijiona ameheshimiwa pale anapokosolewa kwa adabu na heshima na upole na kwa utaratibu na si kwa kebehi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom