Speed ya dunia dhidi ya speed ya ndege na mawingu imekaaje hapa

Mzingo wa dunia kuzunguka ikweta(circumference) ni km40,075.
Dunia inazunguka wastani wa km1600 kwa lisaa limoja (1600km/hr) katika mzingo huu.

Kwa mantiki hiyo ni speed kubwa mno kuliko hizi ndege za abiria tunazopanda.Na kukamilisha mzunguko mmoja ili tupate usiku na mchana mfano ikiwa ni saa moja asubuhi ikifika kesho saa moja asubuhi maana yake dunia imezunguka kwa saa 24 hadi ikarudia usawa ule ule ilipokuwa jana.
Kuna mambo au maswali yamenitatiza kwa muda mrefu:-

1.What is the impact of the speed of plane relative to speed of earth?Mathalani vile dunia inazunguka magharibi kwenda mashariki.Ndege ikaondoka juu usawa wa ikweta kuelekea Marekani.

Mbona isitumie muda mfupi sana vile dunia inazunguka speed kubwa mno kinyume chake?Na je kama ni hivyo kwanini isingening'inia tu angani kuitegea dunia ijizungushe yenyewe ikifika usawa wa Marekani ishuke?

Upande mwingine wa shillingi sasa ipae usawa ule ule wa ikweta sasa ielekee mashariki kule dunia inakoelekea kuzunguka kama kwenda India.je speed ya dunia ilivyo kubwa kuliko ndege yenyewe mbona haizidiwi kiasi kwamba kule inakotaka kwenda panakwenda kasi zaidi kwenda mbele?

2.Vile speed ya dunia ni kubwa mno mbona mawingu hatuoni tunapishana nayo tukiyachungulia tukiwa chini mithili vile tukiwa kwenye gari tunaona miti kama inatembea kurudi nyuma?

Naomba tuelimishane wana JF humu wataalamu wa Aviation na marubani pamoja na wataalamu wa jiografia watujuze.

Mkuu, na mimi naomba nichangie kidogo kwa upeo wa kile alichonipatia Mungu.

Mimi nitajaribu kukujibu kwa ujumla ili kupunguza wingi wa hadithi.

Maswali yako ni mazuri na yenye challenges ambapo mtu itampasa afikiri na kurejea maandiko ili kupata majibu na kujifunza pia.

Wakati Dunia inapojizungusha katika mhimili wake speed kubwa (the surface velocity) huwa katika ikweta na unapoelekea kweye poles kutoka Ikweta hiyo velocity hupungua, lakini hiyo surface velocity ni function ya radius ya dunia kutoka kwenye axis yake au (ni product ya radius na angular velocity ya dunia ambayo ni constant). Hivyo kitu chochote kilichopo juu ya uso wa dunia kikielekea to the poles kutoka ikweta lazima angular momentum yake ibadilike with time na hapo ndipo inapozaliwa kani (force) inayojulikana kama "Coriolis force" iliyovumbuliwa na mwanamahesabu wa kifaransa kwa jina Gaspard Gustave de coriolis.

Kujibu swali lako ni kwamba hiyo coriolis force inayo athari kwenye hewa yetu na hasa yenyewe ndiyo chanzo cha vimbunga (huricanes and tornodoess) na mikondo bahari (sea currents), hivyo ndege inaporuka angani kuelekea katika poles (longitudes) kutoka Ikweta au vise versa lazima uelekeo na speed yake itakuwa affected ukizingatia kuwa ndege inapokuwa angani huwa imebebwa na hewa ambayo nayo imeshikamana na dunia, lakini ndege inapoelekea along ikweta au latitudes coriolis force ni sifuri na hivyo hapo inakuwa ikitembea katika speed yake ya kawaida to the earth reference frame.

Kifupi ni kwamba speed ya ndege huathiriwa ndege inapo elekea along longitudes na haiathirwi inapoelekea along latitudes taking into account the earth being a rotating reference frame.

Kwa Kiasi gani coriolis force inaathiri vyombo vinavyosafiri juu ya bahari, uso na anga ya dunia hilo ni swala la mahesabu na mada mpya.
 
-Dunia ni pamoja na atmosphere/anga lake.

Swali la pili pia linajibiwa na la kwanza.

Nikuoe mfano.

Hivi ukiwa kwenye gari umekaa kwenye siti yako hakuna bumps au kadaraja barabara ya lami imetulia na chupa yako ya chai ukaimimina kwenye kikombe je hiyo chai itamwagika kwa kuwa inaenda na speed ya gari hivyo kikombe kitabaki nyuma????
Umeeleweka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali lingine;
ikiwa kuna chombo kimetumwa sayari nyingine kama vile mars,kuna uwezekano wa kutumia muda tofauti wa kwenda na kurudi kwa spidi ile ile?

Yeah, muda lazima utakuwa tofauti sababu dunia na sayari zingine zote zinatumia mda tofauti wa kulizunguka jua na kujizungusha kwenye mhimili wake, maana yake ni kwamba umbali uliopo kati ya sayari moja na sayari nyingine unaenda ukibadlikia kila mda. Ina maana mda ambao hiyo satellite inaenda kwenye hiyo sayari umbali uliopo kati yake utabadilika wakati hiyo satellite inarudi sababu sayari zote zinatembea kwa mwendo tofauti..unless hiko chombo kisubiri wakati sayari zimejipanga kwa umbali ule ule unaofanana wakati wa kuondoka..

Ndo maana kwa wale wafuatiliaji wa night sky objects watajua kuwa sayari tofauti huwa zinaonekana kwa nyakati tofauti za mwaka wakati wa usku na kwa mida tofauti..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzingo wa dunia kuzunguka ikweta(circumference) ni km40,075.
Dunia inazunguka wastani wa km1600 kwa lisaa limoja (1600km/hr) katika mzingo huu.

Kwa mantiki hiyo ni speed kubwa mno kuliko hizi ndege za abiria tunazopanda.Na kukamilisha mzunguko mmoja ili tupate usiku na mchana mfano ikiwa ni saa moja asubuhi ikifika kesho saa moja asubuhi maana yake dunia imezunguka kwa saa 24 hadi ikarudia usawa ule ule ilipokuwa jana.
Kuna mambo au maswali yamenitatiza kwa muda mrefu:-

1.What is the impact of the speed of plane relative to speed of earth?Mathalani vile dunia inazunguka magharibi kwenda mashariki.Ndege ikaondoka juu usawa wa ikweta kuelekea Marekani.

Mbona isitumie muda mfupi sana vile dunia inazunguka speed kubwa mno kinyume chake?Na je kama ni hivyo kwanini isingening'inia tu angani kuitegea dunia ijizungushe yenyewe ikifika usawa wa Marekani ishuke?

Upande mwingine wa shillingi sasa ipae usawa ule ule wa ikweta sasa ielekee mashariki kule dunia inakoelekea kuzunguka kama kwenda India.je speed ya dunia ilivyo kubwa kuliko ndege yenyewe mbona haizidiwi kiasi kwamba kule inakotaka kwenda panakwenda kasi zaidi kwenda mbele?

2.Vile speed ya dunia ni kubwa mno mbona mawingu hatuoni tunapishana nayo tukiyachungulia tukiwa chini mithili vile tukiwa kwenye gari tunaona miti kama inatembea kurudi nyuma?

Naomba tuelimishane wana JF humu wataalamu wa Aviation na marubani pamoja na wataalamu wa jiografia watujuze.

It’s true I was going to Kuala lumpa with Quatar Airways from Doha to Malaysia is about 5 to 6 hours but we left Doha around 0230 hours and we arrived KL 1530 and trip back we left KL 0220 and we arrived Doha around 0430
 
Ukimaliza vidato utajua na utajishangaa kwanini uliuliza maswali ya kiboya na kwanini ukusubiri mwalimu akufundishe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hilo ni jibu mujarabu kwenye forum kweli?

Ninavyoelewa forum huwa haina hadhi ya mwalimu wala mwanafunzi.

Kinachotakiwa ni kuchangia mada kama unalielewa jibu lake.

Na kama lipo juu ya uwezo wako, basi una mute na kuendelea na post zingine, kimyakimya kistaarabu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wemgi huwa mnakosea hapo kwa kujibu maswali haya bila kuangalia kuwa muuliza swali kauliza kwa ndege ambayo haina contact na ardhi ya dunia na wewe ukamjibu kwa mfano wa mtu ambaye yupo in contact na gari(dunia).
-Dunia ni pamoja na atmosphere/anga lake.

Swali la pili pia linajibiwa na la kwanza.

Nikuoe mfano.

Hivi ukiwa kwenye gari umekaa kwenye siti yako hakuna bumps au kadaraja barabara ya lami imetulia na chupa yako ya chai ukaimimina kwenye kikombe je hiyo chai itamwagika kwa kuwa inaenda na speed ya gari hivyo kikombe kitabaki nyuma????
 
Jibu fupi tu. Inazunguka na atmosphere yake. Yaani chochote kilichoshikiliwa na dunia, kinacheza mziki wa dunia kipende au kisipende.
Kwa hiyo ndege ikitoka katika sayari nyingine ikawa inakuja duniani ikigusa ile anga ya dunia ambayo nayo inazunguka alafu ile ndege ikaganda pale pale nayo itakuwa inazunguka na ile atmosphere?

Na jee ndege iliyotoka katika atmosphere ya dunia ikaja mpaka katika sehemu ambapo hakuna force ov gravity ile ya duniani maana yake hapo hakuna mvutano.na tukumbuke ndege imetokea katika point flani mpaka kufika nje ya mvutano wa dunia.
Sasa jee ikitaka kurudi inaweza kuingilia katika point ile ile ambayo imetumia kupenya pale mwanzo mpaka kutoka kufika huku nje?
Au itasubiri dunia inapozunguka ikifikia ile point ndo nayo ndege izame pale tubwiii iende katika nchi yake?

Kwa sababu kama dunia inaUnguka na atmosphere yake maana yake mpaka ile point yenyewe itakuwa inazunguka tena kwa spidi kubwa sana,sasa bila kusubiria ifike ile sehemu ya point uingie badala yake ukaingia kichwa kichwa tu katika anga ya dunia je hakuna uwezekano wa kwenda katika nchi ya mwenzio?

Yaani mfano chukua mpira alafu chora alama ya peni katika mpira(point) alafu sasa zungusha mpira wako alafu ile peni iweke katika mpira unaozunguka pasi na kuzingatia ile point bila shaka peni itatua sehemu nyingine kinyume na ile point kwa sababu mpira unazunguka.na hapo itakuwa umetua katika Nchi ya mwenzio kinyume na pale point ya mwanzo

Hii ikoje?
 
-Dunia ni pamoja na atmosphere/anga lake.

Swali la pili pia linajibiwa na la kwanza.

Nikuoe mfano.

Hivi ukiwa kwenye gari umekaa kwenye siti yako hakuna bumps au kadaraja barabara ya lami imetulia na chupa yako ya chai ukaimimina kwenye kikombe je hiyo chai itamwagika kwa kuwa inaenda na speed ya gari hivyo kikombe kitabaki nyuma????

Mkuu unapozungumzia juu ya dunia (the rotating object in its axis) na unapozungumzia juuu ya kitu kiachotembea juu yake kwa speed fulani kuelekea to the north or south hemisphere, kitu hicho kiwe hewa,ndege, meli, maji ya bahari, rockets nk, ni lazima ufikirie juu ya THE COLIORIS FORCE, na athari zake juu hivyo vitu vinavyotembea juu ya uso wa dunia na athari hiyo inaitwa CORIOLIS EFFECT, na hiyo athari ni ndogo unapokuwa Ikweta na inazidi kuwa kubwa unapoelekea to the poles kutokana na kubadilika kwa angular momentum ya vitu vinapoelekea to the poles ambapo surface speed ya dunia hupungua kadiri unavyo elekea to the poles na jambo hilo huzalisha kani inayoitwa coriolis, hiyo kani haizalishwi unapoelekea kwa speed upande wa latitudes (along the latitudes) kwa sababu surface velocity ya dunia inakuwa ni constant at that particular latitude.

Kifupi unapo neglect the coriolis force basi vyombo vyote vinavyo safiri juu ya uso wa dunia kuelekea to the poles vitatembea sambamba na dunia kama jinsi mtu anaposafiri na inzi ndani ya gari au ndani ya ndege, huyo Inzi haathiriwi na mwendo wa ndege anaporuka humo ndani kwa sababu anakuwa ni sehemu ya hiyo ndege.
 
Mchukue inzi muweke ndani ya basi ataruka kwenda mbele na kurudi nyuma hata kama basi nipo speed 100.Kwahiyo hiyo ndege ndio nzi na basi ndio dunia.
 
Naona watu wanapisha pishana humu sababu alieuliza swali haeleweki aliposema dunia alikiwa anamaanisha nini? Ki kawaida ukisema dunia maana yake ni dunia yenyewe ikiwemo ardhi na atmosphere yake.. So kitu kilichopo duniani ni kila kitu kilichopo chini ya ardhi, kwenye ardhi(juu ya uso wa ardhi) na vyote vilivyopo ndani ya atmosphere yake iwe juu au chini au ndani ya maji.. Vyote hivi vipo duniani. Na hivi vyote vinatembea na spidi ya dunia.. Ukisema nje ya dunia maana yake ni nje ya atmosphere ya dunia..kwa kawaida ni in space.

So unapoongelea ndege ki hivi ni sawa na unapoongelea gari tu.. Ishu ni kuwa ndege inaruka juu tu ila ipo humo humo ndani ya atmosphere so bado ipo duniani.. By the way hakuna ndege inayoruka nje ya dunia.. Na ndo maana hata ndege iende upande gani wa dunia bado itakuwa inaenda relative na spid ya dunia so hakuna kitu cha kusema itaachwa nyuma au itawahi kufika.

Kuna mtu alitoa mfano wa nzi au chai ndani ya gari.. Ni sahihi kabisa.. Na kwa wale wasioelewa basi chukulieni huyo inzi yumo ndani ya ndege au hiyo chai.. Swali linakuja huyo inzi akiwa ndani ya ndege je ndege ikiwa angani na yeye akawa anaruka ruka mle ndani je ataachwa nyuma kwa spidi ile ya ndege na kwenda kujibamiza kule nyuma ya ndege? Au vile anavyokuwa anakughasi mle ndani ya ndege ni kweli kuwa na yeye anakuwa anatuka kwa spidi kama ya ndege ya 500+km/hr? Au chukulia mtu tu aliye ndani ya ndege wakati ikiwa angani je ikitokea akaruka kidogo humo humo ndani ya ndege je na yeye ndege itamuacha na kuishia kujibamiza kulee mwishoni mwa ndege? Sasa kwanini hawaachwi? Sababu wanatembea na atmosphere ya ndani ya ndege kamam ndege invyotembea na atmosphere ya dunia na yenyewe haiwezi kusema inaachwa na spidi ya dunia sababu eti haipo ardhini..

So ishu sio kuruka juu ishu ni kuwa hii ndege ipo wapi.. Kama ndege zingekuwa zinaruka hadi nje ya dunia(nje ya atmosphere) hiyo ni habari ingine sawa na kuongelea satellites na rocket zinazoenda anga la juu.. Hizo ndo zina hayo mambo ya timing na spidi ya mzunguko wa dunia.. Sio ndege hizi za kawaida..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah, muda lazima utakuwa tofauti sababu dunia na sayari zingine zote zinatumia mda tofauti wa kulizunguka jua na kujizungusha kwenye mhimili wake, maana yake ni kwamba umbali uliopo kati ya sayari moja na sayari nyingine unaenda ukibadlikia kila mda. Ina maana mda ambao hiyo satellite inaenda kwenye hiyo sayari umbali uliopo kati yake utabadilika wakati hiyo satellite inarudi sababu sayari zote zinatembea kwa mwendo tofauti..unless hiko chombo kisubiri wakati sayari zimejipanga kwa umbali ule ule unaofanana wakati wa kuondoka..

Ndo maana kwa wale wafuatiliaji wa night sky objects watajua kuwa sayari tofauti huwa zinaonekana kwa nyakati tofauti za mwaka wakati wa usku na kwa mida tofauti..
Sent using Jamii Forums mobile app
Hicho chombo kitatumia spidi gani kuiwahi spidi ya dunia ili kisiachwe? kumbuka hicho chombo kitakuwa nje ya atmosphere ya dunia kwa wakati huo.
 
Back
Top Bottom