Special Thread: Yanayojiri Uchaguzi TFF 2025

Special Thread: Yanayojiri Uchaguzi TFF 2025

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
8,011
Reaction score
11,429
Salaam Members:
June mwaka huu TFF walitoa tangazo la kuwepo kwa uchaguzi kwa nafasi ya Urais na nafasi za Wajumbe 6 wa kamati ya utendaji.
IMG_20250620_172818.jpg

Hapa utazipata updates za hatua zote za awali hadi uchaguzi mkuu utakaofanyika Tanga tarehe 16/08/2025.

Pia kama una updates zozote unaweza share nasi kwani kote bado ni kupata habari.
 
Inavyoonekana hadi sasa ni Wallace Karia amechukua Endorsement zote 47 kutoka kwa wajumbe ambao Wana haki kamili ya kushiriki uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo, hali inayopelekea kuwa mgomba pekee wa kiti Cha uraisi wa shirikisho hilo.

Nukuu toka kwa Richard Shija:
"Rais aliyepo madarakani anapochukua Endorsement zote maana yake anazuia wagombea wasiingie kwenye uchaguzi"

Kwa malalamiko aliyotoa Richard Shija leo huenda Mchakato wa Uchaguzi nafasi ya Raisi wa TFF na nafasi zingine Ukasimamishwa ila siyo hakika.
Tuone kama kwenye kamati ya maadili kuna lolote litajiri
 
Karia hataki kung'ooka hapo Tiefuefu
Ni kweli hataki kutoka lakini hawa wengine hua hawapigi mahesabu mapema, waanza mchakato saivi wakati ishu inatakiwa ianzwe miaka michache nyuma.
Wanapo kuja kushtuka, tayari mambo yamesha malizika
 
😂
Zinachukuliwaje?
Kila mgombea urais anatakiwa awe na wadhamini si chini ya watano, ambao ni vyama wanachama vya mikoa, klabu za Ligi Kuu, na vyama shirikishi kama cha waamuzi, makocha, madaktari na wachezaji.

Sasa kinachofanyika ni kuwahi wadhamini wote halafu wengine wanakosa wadhamini.

Mfano,
Saivi inaonekana Rais wa sasa anamiliki endorsement 47 ina maana wengine wakitafuta wadhamini tayari wamechukuliwa na mmoja hivyo unakosa wakati utaratibu unasema angalau watano tu inatosha lakini watu wanafanya umafia na wengine wanakosa.
 
Medani za vita
 
Ni kweli hataki kutoka lakini hawa wengine hua hawapigi mahesabu mapema, waanza mchakato saivi wakati ishu inatakiwa ianzwe miaka michache nyuma.
Wanapo kuja kushtuka, tayari mambo yamesha malizika
🤩
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Kilomoni Kibamba, amesema Kati ya wagombea 6 waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Tff ni mgombea mmoja tu Wallace Karia ndiye mwenye sifa za kikanuni kati yao.Hivyo basi wagombea 5 katika usaili wa awali wameshindwa kukidhi vigezo vya kanuni“Upande wa Uraisi kati ya 6 walio hudhuria usaili ni 5 mmoja hakwenda, kati ya 5 wanne wamekosa sifa na mmoja ndiyo kapata” Amesema Wakili Kilomoni Kibamba.
 
Matokeo ya Usaili wa Wagombea Uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

GvAcUWZWUAAgdWY (1).jpeg
 
Back
Top Bottom