Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Israel + Marekani vs Iran

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Israel + Marekani vs Iran

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
710
Reaction score
1,610
Kwa miaka mingi, Marekani na Israel zimekuwa na hofu kuwa Iran inatengeneza bomu la nyuklia. Israel anaamini bomu hilo likikamilika, Iran italitumia kuifuta nchi yao kwenye ramani, hivyo wamekuwa wakitafuta namna ya kuzuia mpango huo kwa nguvu.

madarakani Januari 20, 2025, aliweka msimamo mkali wa "Maximum Pressure". Alitaka Iran iache kabisa urutubishaji wa uranium na iharibu mitambo yake yote, jambo ambalo Iran ililiona kama ni kudhalilishwa na kupoteza uhuru wake.

Wiki iliyopita, nchi ya Oman ilijaribu kuwakutanisha Marekani na Iran ili kuzuia vita. Hata hivyo, Marekani ilitoa masharti magumu ambayo Iran iliyakataa katakata. Mazungumzo hayo yalivunjika rasmi tarehe 26 Februari, na wajumbe wa Iran wakagoma kuendelea na diplomasia.

Baada ya diplomasia kufeli, Marekani na Israel hazikusubiri. Siku ya Jumamosi, tarehe 28 Februari, zilianzisha operesheni kubwa ya anga. Walishambulia vituo vya nyuklia, kambi za jeshi, na makazi ya viongozi wa juu wa Iran mjini Tehran ili kuuvunja nguvu utawala huo mara moja.

Leo Machi 1 hali ni ya taharuki. Kuna ripoti kuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Khamenei, ameshambuliwa vibaya na kuuawa. Iran imekanusha na kujibu kwa kurusha makombora kuelekea Israel na kambi za Marekani. Dunia nzima ina hofu ya kuanza kwa Vita ya Tatu ya Dunia, huku bei ya mafuta ikipanda kwa kasi ya ajabu.
-----------
Israel imedai kuwa ilirusha zaidi ya mabomu 1,200 nchini Iran ndani ya siku moja, ambapo Jeshi la Anga la nchi hiyo limesema mashambulizi hayo yalifanyika kwa ushirikiano na Marekani.

Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni pamoja na shule ya msingi ya wasichana iliyopo Minab, katika jimbo la Hormozgan kusini mwa Iran, ambapo takribani watu 148 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa “makumi ya watoto wasio na hatia” waliuawa katika shambulio hilo la shule, na kusisitiza kuwa tukio hilo “halitapita bila kujibiwa.”

----------
Wizara ya Ulinzi ya Falme za Kiarabu UAE yathibitisha Iran kushambulia kwa Makombora

Iran ilirusha mamia ya makombora na droni kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo, ikieleza kuwa jumla ya makombora 137 na droni 209 zilirushwa siku ya Jumamosi, huku mengi yakizuiliwa na mifumo ya ulinzi wa anga.

Katika tukio lililotokea kwenye uwanja wa ndege wa Abu Dhabi, mtu mmoja aliuawa na wengine saba kujeruhiwa baada ya mabaki ya vifaa vilivyodunguliwa kuanguka eneo hilo, wakati pia uwanja wa ndege wa Dubai—ambao ni miongoni mwa wenye shughuli nyingi zaidi duniani kwa safari za kimataifa—ulilengwa na mashambulizi hayo

------------
Viongozi wa Iran waliouawa katika shambulizi la Israel na Marekani
  • Ayatollah Ali Khamenei- Kiongozi Mkuu wa Iran (Supreme leader)
  • Ali Shamkhani, - Mshauri wa masuala ya usalama (Khamenei’s security adviser)
  • General Abdolrahim Mousavi,- Mkuu wa Majeshi Iran (Iran’s Armed Forces chief of staff)
  • Aziz Nasirzadeh, - Waziri wa Ulinzi(Minister of Defence)
  • Mohammad Pakpour, IRGC commander-in-chief
-------------
IRNA yatangaza shambulizi la Israel katika mji wa Tehran

Shirika la habari la Iran (IRNA) imeripoti milipuko mikubwa katika mji mkuu Tehran, ikisababisha sauti za mlipuko zikisikika maeneo ya Seyyed Khandan, viunga vya Qasr, Vanak Square na Barabara ya Motahari, huku moshi na uharibifu unaonekana kuibuka ikiwa ni baada ya Jeshi la Israel kutangaza kufanya mashambulizi ya makombora ya anga katikati ya mji wa Tehran.

-------------
Iran inaona kisasi kama jukumu na haki halali kufuatia mauaji ya Ayatollah- Amesema Rais wa Iran

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa kutafuta kisasi kwa kuuawa kwa Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Iran ni “dharura na haki halali” ya nchi hiyo.

“Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona kuwa kutafuta haki na kulipiza kisasi kwa wale waliotekeleza na kuagiza uhalifu huu wa kihistoria ni dharura na haki halali, na itatumia nguvu zake zote kutimiza wajibu huu mkubwa,” alisema Rais Pezeshkian, akitoa pole zake.

1772357818829.png

--------------

Kiongozi mkuu wa usalama wa Iran ametoa onyo kuwashambulia Marekani na Israel kwa kishindo zaidi

“Jana Iran ilirusha makombora kuelekea Marekani na Israel, na yaliwadhuru,” alisema Larijani kwenye mtandao wa X.

“Leo tutawapiga kwa nguvu ambayo hawjawahi kuikumbuka hapo awali.”

Lugha yake ilikuwa kama onyo lililotolewa na Rais Donald Trump dhidi ya Iran siku hiyo hiyo.

“Iran imetangaza itapiga vikali leo, zaidi ya jinsi walivyowahi kupigwa hapo awali,” aliandika Rais Trump kwenye mitandao ya kijamii.

“Lakini bora wasifanye hivyo, kwani iwapo watafanya, tutawapiga kwa nguvu ambayo haijawahi kuonekana hapo awali!”

--------
PICHA: Raia wa Iran wameanza kukimbilia nchi jirani kwa usalama
1772364891758.png


1772365003535.png

People cross from Iran into Turkiye at Kapikoy border

------------

Updated: Idadi ya vifo yafika 8 na Majeruhi 27
......
Watu 4 wauawa kufuatia shambulizi la Iran katika mji wa Beit Shemesh, Israel

Watu wasiopungua wanne wameuawa na takribani 20 kujeruhiwa kufuatia shambulio la kombora la balestiki kutoka Iran katika mji wa Beit Shemesh, ulioko karibu kilomita 30 magharibi mwa Jerusalem

Jeshi la Israel limesema kupitia taarifa kwenye Telegram kuwa vikosi vya uokoaji na utafutaji, kwa kushirikiana na timu za matibabu pamoja na helikopta ya kuwahamisha majeruhi, vinaendelea na operesheni katika eneo lililopigwa.
----------
Wanajeshi 3 wa Marekani wauawa na 5 kujeruhiwa vibaya katika operesheni dhidi ya Iran

Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa wanajeshi watatu wameuawa na watano kujeruhiwa vibaya katika operesheni dhidi ya Iran — vifo vya kwanza vya Marekani tangu mashambulizi yaanze, kwa mujibu wa Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa wanajeshi watatu wameuawa na watano kujeruhiwa vibaya katika operesheni dhidi ya Iran — vifo vya kwanza vya Marekani tangu mashambulizi yaanze, kwa mujibu wa US Central Command (CENTCOM)..

1772393439874.png

Pia soma:
 
Mwaka huu lazima mambo yakae sawa ili heshima iwepo
Nalog off Z
 
Kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa Irani Dunia ya kiislamu imeonesha Umoja wa hali ya juu sana kulaaani tukio Hilo.

Wale waliokuwa wanasema shia siyo waislamu wameaibika!
 
Kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa Irani Dunia ya kiislamu imeonesha Umoja wa hali ya juu sana kulaaani tukio Hilo.

Wale waliokuwa wanasema shia siyo waislamu wameaibika!
Shia ni waislamu ila wa imani kali sana..kama ukristo washia ni kama walokole
 
Hali ni mbaya sana. Dunia isipoungana dhidi ya Marekani, tutaishi maisha ya taabu sana hapa duniani
 
Israeli Air Force in ACTION 🇮🇱🇮🇱🇮🇱
 

Attachments

  • FB_IMG_17726500156755361.jpg
    FB_IMG_17726500156755361.jpg
    191.6 KB · Views: 5
"Alqiswaswa hakki....
Allah akbar"
Hii kauli watakua wameiongea sana jeshi la iran ila bado wanapigwa...
Wakome kung`ang`ania mambo ya wakubwa
 
kinachowapa shida wakristo wa TZ,Venezuela,North Korea,Russia,China,South Africa , baadhi hazina dini zingine zina wakrsisto wengi zipo pamoja na Iran,halafu kuna wao wazee wa mungu wa Israel Kila kinachofanywa na nchi yenye waislam wengi wanakiponda😁🙃😅🤣,
 
Back
Top Bottom