GE2025 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CHAUMMA, Salum Mwalimu na Devotha Minja

GE2025 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CHAUMMA, Salum Mwalimu na Devotha Minja

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Uzi Maalum wa mijadala yote ya michakato ya ziara za kampeni za mgombea nafasi ya Urais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu na Mgombea mwenza Devotha Minja.

----------------
Agosti 27, 2025
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemteua Mhe. Salum Mwalimu kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Devotha Mathew Minja kugombea Kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

Hafla hiyo ya uteuzi iliyofanyika kwenye Ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma leo tarehe 27 Agosti, 2025 imeongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele

1756372340598.png

Soma pia GE2025 - Salum Mwalimu wa CHAUMMA atinga na nyomi kuchukua fomu ya Urais

Chanzo: Tume ya uchaguzi Tanzania
 
Back
Top Bottom