Hizi timu zinafanana mno mbinu za uchezaji.. yaani ni kama majina ya timu/nchi yanavyofanana
Hahaha tupia tu hata vya 'treble winners', mi ntakuwa shabiki wako number moja.
hahahah Si unajua tena nguo ya kuazima haisitiri.....nitaumbuka miye.......
Halafu ukitoka uwanjani baada ya mpira kwisha umenuna ile mbaya baada ya kukung'utwa kwa uzembe wa timu. Mie mpira wa Bongo nilishanyoosha mikono juu maana ni masikitiko tu miaka nenda miaka rudi. Halafu hawa TFF kwa upumbavu wao badala ya kuhakikisha wanakuza vipaji vya Watanzania wanaruhusu timu za kwenye ligi kuu zisajili mpaka wachezaji wanane wa kigeni. Hii TFF yote ni ya kutimuliwa haraka sana.
Mimi huwa ndo sielewi kitu hata ukiniambia niwataje watano tu nitachemka.......nimeskia kwa bahati mbaya eti hadi Uganda leo wametupiga 3 hii too much sasa......
Nimeuona uzi humu few minutes ago ukidai baada ya matokeo haya kocha wa Taifa Stars katimuliwa, sasa Waziri wa michezo naye atimue timu yote ya uongozi wa TFF na kuitisha uchaguzi mwingine in 45 days.
Na hilo ndo linatakiwa lifanyike sasa sisi tunaweza nin jamani? Hivi hakuna mashindano ya ufisadi labda? .......Juzi nimecheka nilikuwa naskiliza redio moja hapa bongo mmoja wa wasikilizaji akapiga simu akasema anashangaa hao wanaoitwa watanzania walioshinda mbio za magari maana last Sunday kulikuwa na ushindani wa mbio za magari sasa wote walikuwa ngozi nyeupe asili ya Hindi... Akasema itabidi na kwenye michezo mingine hasa mpira tutafute watanzania wa dizaini hiyo maana ndo inaonekana wanaiweza kazi.