Special kwa wale waliopitia mafunzo ya JKT

patience96

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
1,353
568
Kwa wale wenzangu mliopitia JKT kwa mujibu wa sheria au vinginevyo.
Ni mkasa gani MKUBWA ambao ulikumbana nao ukiwa JKT aidha kwa uzembe wako mwenyewe kwa kutozingatia kanuni na sheria za JKT, kuonewa na Afande, au kosa la kuruta mmoja kisha kombania nzima kuumia?

Nakumbuka matukio mengi, zaidi matukio mawili sitayasahau!

1. Mimi nilikuwa kombania "Charle" na pacha mwenzangu alikuwa kombania "Danger". Siku moja pacha mwenzangu ali-jongo kwenda Mbauda Arusha kwa kupanda magari ya kusomba mchanga, Kumbe wakati akikata mitaa OC wa kombania yangu alimuona!
Kesho yake wakati wa master parade niliitwa mbele ya kombania yetu. Niliulizwa ruhusa ya kwenda mjini nilipewa na nani, nami nilikataa kata kata kuwa siyo mimi.
Kama kawaida daktari wa kikosi alipima afya yangu kama niko fit, kisha extra drill ya nguvu toka kwa MPs wawili na hatimaye Quarter Guard!
Kama hiyo haitoshi niliongezewa guard kama 5 hivi!
2. Kisa cha pili; Afande mmoja alikuwa akimtaka dada mmoja wa kombania yetu, lakini msimamo wa yule dada kukataa ilikuwa kiyama chetu kombania nzima; katika zoezi zima la "kuruka ndege" na "kusukuma dunia" bila sababu ya msingi, dada mmoja ali-breed!

Unakumbuka maneno haya:
Mapororo/pororo,
Kujongo,
Mahaba,
Gazeti,
C ya matron,
serengeti,
disco,
Adjutant,
CO,
Usawa wa gudulia,
Bigura,
nyakua,
imetoka,
serule,
kuruta, pitshort, green vest ya kijani, AK-47, Ajwaa, kuangusha maembe, chafu kabisa, roll call
n.k.

Kwa wale waliopitia Oljoro JKT, sehemu nzuri ya ku-jongo ilikuwa: korongoni, mizabubini, kwa mzee Paraseko n.k.
 
Yaani aroo unanisimamia rimwanamke ririroachika. Rengo ra gesi ni kukufanya uwe muchovu na upokee amri ukiwa muchovu. Askari mtiifu utamjua akiwa muchovu.Sio unanisimamia kama rimwanamuke rikikojozi araa.
 
Back
Top Bottom