Lakini ukiangalia factor mbalimbali, ni bora kununua gari kutoka japan coz tuseme gari yako imeharibikia huko milimani ugweno na gari inahitaji spea ili iendelee na safari. Hakuna muda wa kuagiza spea online mpaka ije wakati we unahitaji kuendelea na safari. Spea za gari za japan unaweza pata popote hata huko milimani.
Nissan ilinunuliwa na Renault ya Ufaransa siku nyingi tu. Mjapan hana chake hapo.
Nissan imebaki kuwa ni gari ya kijapani pamoja na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika sharing. Hizo gari za Kifaranza zimemezwa kabisa na Nissan na kinachosikika ni Nisasan gari ya Kijapan.
Kuna timu kubwa za mpira wa soccer, football, basketball nk za ulaya na Marekani zinamilikiwa na watu wa mataifa mengine lakini zinabaki ni timu za nchi husika, haziwezi kuhamishiwa nchi waliko wamiliki.
Mchezaji wa mpira wa kikapu James Libron ana hisa timu ya Liverpoor ya Uingereza, hapa huwezi kusema timu hiyo ni ya Marekani.
Kwa makampuni kujitanua kuwa na matawi nchi nyingine lakini haki za kibiashara zinamilikiwa na nchi husika Japan.
Magari yote duniani wenyewe ndio hap hao tu, hata nyumbu utakuta tunajidai tu lakini vipuli ndio walewale tu wenyewe:
Asikudanganye mtu, availabiliy ya spea za magari hayo ni almost zero. Usidanganywe na vingereza picha vilivyowekwa humu na waliotoka nje ya mada wengi tu. We njoo na hiyo migari aaffuu ikufie ukiwa unapandisha kishumundu ndo utajuwa kama NISSAN ILINUNULIWA AU INA SHEA NA RENAULT. Usihadaike na hayo mashindano ya ujuwaji hapo, kutaka spea za magari hayo hapa TZ ni sawa na kuingia buchani na kuuliza kama unaweza ukanyolewa humo.