Soviet Female Assassins: Majasusi wa kike wa K.G.B na silaha ndogo ya hatari sana iliyoitwa "Lipstick Pistol" (The Kiss of Death)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Soviet Union Female Assassins: Majasusi wa kike wa K.G.B na silaha ndogo ya hatari sana iliyoitwa "Lipstick Pistol" (The Kiss of Death)

lg.jpg


UTANGULIZI
=====
Mnamo mwaka 1969 bwana Markov akaondoka kutoka nchini Bulgaria akahamia nchi za magharibi. Kwanza alianzia Italy kisha akaweka makazi yake ya kudumu jijini London kwenye miaka ya 1970 ambapo akajifunza kiingereza na kisha kufanya kazi kama mwanahabari kwenye idhaa ya ki bulgaria ya shirika la utangazaji la uingereza (BBC) Deutsche Welle (DW) pamoja na Radio Free Europe.

Asubuhi ya tarehe 7 mwezi wa September mwaka 1978, bwana Georgi Markov alikuwa njiani akielekea kazini kwake mejengo ya ofisi za shirika la BBC. Wakati akiwa anasubiri kupanda bus akiwa pamoja na abiria wengine pale kituoni, ghafla akahisi maumivu ya ghafla na makali sana nyuma ya paja lake la kulia ambapo baadaye akaja kusema ni kama aling'atwa na mdudu tu.

Mtu aliyesimama karibu yake, ambaye alizungumza kiingereza kilichojawa na lafudhi ya kigeni, glafla akamsogelea na kuokota MWAMVULI uliokuwa umedondoka chini na kusha kusema kwa sauti ya chini sana "samahi sana mwamvuli wangu umekugonga kwa bahati mbaya". Kabla yule jamaa mwenye mwamvuli akapandacha taxi chaaaaap na gari kuwasha moto na kuondoka.

Baada ya kufika kazini na kujitazama kwa umakini zaidi, Markov akagundua kashimo kadogo, kekundu na kanakouma sana nyuma ya mguu wake ule. Kadri siku zilivyozidi kwenda alizidi kuumwa sana kisha kupelekwa hoapitalini akiugua homa kali sana. Bwana Georgi Markov akafariki mnamo tarehe 11 September.

Ripoti ya kitabibu ikaja kuonesha ya kwamba bwana Markov aliuwawa kwa punje ndogo iliyorushwa kama risasi katika mguu wake asubuhi ile ya majonzi. Baada ya uchunguzi wa maiti uliofuata, forensic pathologists wakaja kugundua punje ya chuma kidogo iliyokuwa na umbo na duara mbele ikiwa na ncha kama ya pini ikiwa imetumbukia ndani ya mguu wake.

Ile punje ya chuma ilirushwa kwa kutumia bunduki ya mwamvuli ikiwa imejazwa somo hatari sana aina ya Ricin yeye ujazo wa 0.2 milligrams. Bunduki ya mwavuli sio aina pekee ya silaha iliyokuwa ya kificho. Mwanadamu amejaribu kuficha bunduki kwa kutumia karibu kila kitu unachoweza kufikiria.

Nilisimulia full story hapa>>> Umbrella Gun: Usalama wa taifa la Urusi (KGB) walivyoua msaliti wa Bulgaria kwa sumu ya mwamvuli

Bunduki zimekuwa zikifichwa kwenye masanduku ya vidonge, scribe’s casing, filimbi, penseli na katika makopo ya soda za pepsi na Coca. Kumekuwa na bunduki za kufanana na saa za mfukoni, bunduki za pete, bunduki za pampu za baiskeli, pamoja na bunduki za rangi ya kupaka mdomoni (lipstick guns/pistol), ambazo ndio lengo kuu la thread hii.

aqaqsdefds.jpg


KGB LIPSTICK GUN (THE KISS OF DEATH)
==========
Neno "busu la mauti" (The Kiss of Death) linaweza kuwa na maana kadha wa kadha. Unaweza kuwa unazungumzia juu ya usaliti wa Yuda kwa Yesu kwa busu la kinafiki katika bustani ya Gethsemane, unaweza pia kuongelea ishara ya Mafia wakati mtu amewekewa alama ya kifo, au unaweza kuwa unazungumzia juu ya busu ya kifo - "Lipstick Pistol" iliyotumiwa na majasusi wa KGB wakati wa Vita baridi.

vfvfghytr.jpg


Bastola hii ilikuwa ni ya risasi moja (a single shot 4.5 mm) iliyokuwa inaweza kufichwa vizuri na kwa usiri sana ndani ya pochi ya dada/mama mrembo (Femme Fatale). The gun could be fired with a simple twist of the tube.

Hakuna ajenti wa kike anayejiheshimu wa KGB wakati wa vita baridi angekuwa anatembea bila kuwa nayo hata moja - pistol bora kabisa kwa kulipulia vichwa vya wapenzi wa kiume (malaya) wasiohitajika tena ndani ya CIA.

Ikipigwa karibu na mtu mlengwa, nyuma ya kichwa chake ilikuwa na accuracy pamoja na madhara makubwa sana. KGB haikuwahi kuuza kabisa bastola yake hii ya risasi moja iliyoundwa kama bomba la lipstick (a tube of lipstick). Wanawake walikuwa ni wapelelezi wenye mafanikio sana wakati wa vita baridi.

Ingawa hakujawahi kutokea uhalifu wowote ndani ya Marekani unaohusisha hii bunduki ya lipstick lakini walikuwa walikuwa wanaweza kubeba bunduki hii ndogo ya mililita 4.5 (4.5 millimeter single-shot gun ) kwa miaka hiyo ya 1960 kwa maana ilionekana haina madhara yoyote na ilikuwa ni rahisi kuificha kisha kuitumia na kufyatua risasi kwa distance ya karibu ambayo isingeweza kuwapa mashaka yoyote polisi wakati wa upelelezi.

72650628-bullet-pintalabios-killing-belleza-concept-3d-prestación.jpg


Ingawa bastola hii ya lipstick iko kwenye rangi yake ya asili ya wekundu, miaka ya 1960s zilikuwa zinaanza kutengenezwa rangi mbalimbali zisizo na kawaida za midomo kama rangi ya pinki, fedha na hata nyeupe.

ITAENDELEA NEXT TIME. NIMESHTUSHWA SANA NA KIFO CHA MZEE MKAPA. MUNGU AMPE PEPO NJEMA BABA YETU HUYU.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom