Ni jambo pia la kujivunia kuona waafrika wenzetu wanapenda lugha yetu na kuitamani iwe yao. Hatuna budi kumtumia bwana Malema salamu za umoja na kumzawadia uraia wa kidiplomasia ili kazi hii tuifanye pamoja na kwa kasi inayotakiwa.Kiswahili ndiyo "lingua-franca" ya ukanda wa nchi za Maziwa Makuu. Kinazungumzwa sana Afrika baada ya Kiarabu na Kifaransa. Ni Lugha rasmi, Kenya, Tanzania na Uganda. Katika nchi ya DRC, Kiswahili kinazungumzwa zaidi pia na kinazungumzwa zaidi kwenye majimbo matano kusini mwa nchi hiyo (DRC). Kimeshatumika katika muziki, na sanaa ya filamu. Mwanamuziki Michael Jackson katika wimbo wake wa "Liberian Girl" katumia Kiswahili, mtoto wa Bob Marley (Damian Marley) akishirikiana na NAS katika wimbo wao wa "As We Enter" kadhalika wametumia Kiswahili. Nitamatishe kwa kusema kuwa, bila shaka hii ndiyo lugha ya Kiafrika inayostahili kutumika rasmi. Asante Julius Malema.
baki tu apa nchini usisafiri kama mkuu....Nakubaliana naye Mia kwa Mia Africa iwe Na lugha yake.Kiswahili kitakuwa mkombozi wa wengi mimi nikiwemo.Nikisafiri nje napata shida sana kisa tu kingereza hakipandi
udhaifu wa Zuma ulimbeba sanaIla jamaa kapotezwa siku hizi. Sio yule Malema wa kipindi kile.
Back to topic: yeye anajua hicho kiswahili?
Yuko sahihi. Ndoto ya Mwalimu nyerere PAN Afrikanism ilikuwepo tangu zamani. Yuko sahihi kabisa. Kuonyesha yuko fair kasema kiswahili na siyo lugha ya kwao.Jamaa ana siasa kali za kizalendo, yaani za kibaguzi, racist, black nationalist, tribalist
Ni kama wale wazungu wapinga uhamiaji wasiopenda nchi zao kuingiliwa na Weusi ama Waarabu
Huyu anazungumzia Kiswahili kwa kuwa tu ana chuki na wazungu na sio kwamba linaamini katika intergration ya ukweli baina ya binadamu hapa duniani
Muda huu tu BBC wameripoti Waafrika weusi wanauawa huko Afrika Kusini kisa tu sio wazawa, wazungu pia wanauawa kisa siasa za kichochezi na kibaguzi za huyo jamaa
Na ishu ya kuunganisha Afrika sijui ni ndoto ya saa ngapi
Nchi nyingi za Afrika zimeshindwa tu kujiunganisha kwa ndani zenyewe, unawaza bara zima kuungana, DRC, Sudan, Nigeria, Ethiopia, Cameroon n.k watu wanabaguana na kuuana kisa tu kabila tofauti ama dini, na viongozi wao wameshindwa kuwaunganisha, malaika gani ataunganisha bara zima?
Halafu single currency kwa biashara ipi tunayofanya pamoja?
Nchi za Kiafrica zinafanya biashara na China na Marekani & Ulaya kwa 90%, sisi hatuna vitu vya kuuziana labda sijui unga na maziwa
Sababu hatuzalishi bidhaa, tunaingiza kutoka ulaya na china kisha tunawauzia bidhaa ghafi, sasa hapo utahitaji single currency ya kazi gani? Au mihemko ya kuiga EU?
Wanasiasa wengine bana
Ila jamaa kapotezwa siku hizi. Sio yule Malema wa kipindi kile.
Back to topic: yeye anajua hicho kiswahili?
Nasikia anaugua "ngoma" amekonda sana.
Ili kung'amua inabidi kuwa na king'amuzi.Tangulini ngoma ikawa ugonjwa. Kwanza hamna ugojwa unaoitwa ngoma.
Kwanini mkuu mbaoHaiwezekani Milele.