Soup ya mchanganyiko wa nyama ya ng’ombe, figo na maini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Mahitaji
Nyama ya ng’ombe 1/2 kilo
Maini 1/2 kilo
Figo 1/2 kilo
Vitunguu viwili vikubwa
Pilipili hoho tatu
Pilipili kali unazoweza kula
Limao
Chumvi
Uduvi kikombe cha chai

Jinsi ya kupika
Osha nyama kata kata weka pembeni figo osha kata kata weka pembeni na maini hivyo hivyo

Weka sufuria kwenye moto weka nyama, kamua limao na pilipili kukata shombo. Acha nyama ichemke mpaka iive.

Nyama ikiiva osha uduvi weka ndani.

Baada ya dakika kumi weka figo, pilipili hohoho na vitunguu vilivyokatwa vidogovidogo,

kwakuwa maini hayachelewi kuiva yaweke mwisho na yakiiva soup iko tayari.

Weka chumvi na limao

Soup iko tayari kuliwa.


Uduvi (pia duvi, kijino au ushimbu) ni wanyama wadogo wa bahari wa oda Decapodakatika nusufaila Crustacea (gegereka). Hawa ni aina za kamba wadogo. Majina "uduvi" na "ushimbu" hutumika kwa kundi la wanyama hawa au kwa fungu sokoni. Wanyama pekee huitwa "duvi" au "kijino".

Wanatumika kama kitoweo cha chakula.
 
Mahitaji
Nyama ya ng’ombe 1/2 kilo
Maini 1/2 kilo
Figo 1/2 kilo
Vitunguu viwili vikubwa
Pilipili hoho tatu
Pilipili kali unazoweza kula
Limao
Chumvi
Uduvi kikombe cha chai

Jinsi ya kupika
Osha nyama kata kata weka pembeni figo osha kata kata weka pembeni na maini hivyo hivyo

weka sufuria kwenye moto weka nyama, kamua limao na pilipili kukata shombo.
Acha nyama ichemke mpaka iive.

Nyama ikiiva osha uduvi weka ndani.

baada ya dakika kumi weka figo, pilipili hohoho na vitunguu vilivyokatwa vidogovidogo,


kwakua maini hayachelewe kuiva yaweke mwisho na yakiiva soup iko tayari.

weka chumvi navuonje limao

soup iko tayari kuliwa.
Hivi maini na figo si vitu vya hatari sana kwa mwanadamu kula? Maini yanaondoa sumu na figo zinachuja uchafu na kutoa mkojo. Haina madhara kula hivyo vitu?
 
Hivi maini na figo si vitu vya hatari sana kwa mwanadamu kula? Maini yanaondoa sumu na figo zinachuja uchafu na kutoa mkojo. Haina madhara kula hivyo vitu?
Maini na figo Afrika ndiyo bidhaa ya kwanza kuisha kwenye butcher. Hata maji ukinywa mengi sana yanapunguza electrolytes mwilini. Eat in a moderation
 
Hii soup ukiwa unauguza mgonjwa atapata ahueni tu, ni full virutubisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom