Pishi la maini ya kuku

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
772
Mahitaji
Maini ya kuku 1/2 kilo
Vitunguu vikubwa 2
Hoho 1
Pilipil 1
Limao 1/2
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia

Matayarisho
Safisha maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo. Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali. Ni matam balaa. Enjoy!

1692104648929.png
 
Nafikiria maini nusu kilo ya kuku ni kuku wangapi na gharama yake
 
Nafikiria maini nusu kilo ya kuku ni kuku wangapi na gharama yake
Maini ya kuku yapo super markets unaweza kununua kwa portions upendazo nadhani yanaanzia nusu kilo sababu wao huchinjisha kuku na kutenganisha kila kitu kama sehemu ya bidhaa kujiongezea faida maana ukisema uchinje mwenyewe utachinja kuku wengi kupata maini kilo moja ila supermarkets yapo tayari.
 
Wanauza yakiwa tayari supermarket yapo hata firigisi zipo
Me mara nyingi nabeba firigisi zikiwa na maini full hata sijui km kuna maini ya kuku peke ake!!! Jiko lenyewe nishamsusia dada na hivi sina mume jikoni kuingia kwa nadra sana 😂😂😂😂😂
 
Me mara nyingi nabeba firigisi zikiwa na maini full hata sijui km kuna maini ya kuku peke ake!!! Jiko lenyewe nishamsusia dada na hivi sina mume jikoni kuingia kwa nadra sana
Mungu akujaalie upate chaguo la my heart wako.....horneyyy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom