Sound Bar vs Home Theater

papag

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
1,137
1,609
Habari wakuu?

Naomba mnipe tofauti ya hivyo nilivyo taja hapo juu. Nini matumizi yake? Faida na hasara zake?
Na ni ipi bora kuwa nayo nyumbani?

AHSATENI
 
Nilishawahi nunua lg hometheater kwa 750k, mziki nilivyoufunga ulikuwa unazidiwa mkito na zile speano za laki na 50. Bahati nzuri alieniuzia akanielewa malalamiko yangu nikarudisha mzigo nikamuongezea 250k nikachukua jbl sound bar 2.1... Ni vidude viwili tu tena ambavyo havina mawaya waya ya kuungana ungana, ila mziki ulioko hapo balaa
 
Hometheater ungechukua ya sonny ndiyo uone utamu wake, sonny kwenye sound wapo vizuri
 
Huyo Jamaa hajui mziki, hata hiyo LG HD 750 Home Theater yenyewe huenda walimpiga.

Watu tunaweka volume 20 tu ila mpaka mtaa wa nne tunapongezwa "hongera kwa sherehe".

Je ukiweka hadi 25 ilihali volume hadi 40 si hatari tupu?

Extrovert njoo huku umalize utata maana ninyi ndiyo wenyewe...
 
Home theater ni balaa Mkuu, ukikutana na za kisasa hizi huhangaiki kabisa kuseti base, loud stereo sounds wala sounds quality.

Yani ukishika music remote wewe unachagua tu settings za sound effects "Jazz, Classic, Bass etc" kama kwenye simu vile, mfano mimi nimeseti kwenye Bass yani kila mziki unajichuja kwa kiwango kile kile kilichopikwa nacho studio, sasa ukikutana na miziki iliyoenda shule ya mamtoni kwa hip-hop, R & B, zouk, raggae, raggae danso, country music na ukarudi African musics kama bolingo, old bongo flavors, Zulu, ni shiiida.

Bado gospel songs kama za Bahati Bukuku, Matha Mwaipaja, Cristina Shusho, Ambassadors of Christ, Light Bearers, Ambwene, Rose Muhando, Mabibo L.C, A.I. C Makongoro, Addo November, Medric Sanga, Abiud, Rebecca, Paul Mwai, Psalmist, Prospa Ochimana, Sinach etc huwa najihisi naelea mawinguni kabisa.

Home Theater ni habari nyingine kabisa kwa mziki tulivu wa nyumbani.
 
Huyo Jamaa hajui mziki, hata hiyo LG HD 750 Home Theater yenyewe huenda walimpiga.

Watu tunaweka volume 20 tu ila mpaka mtaa wa nne tunapongezwa "hongera kwa sherehe".

Je ukiweka hadi 25 ilihali volume hadi 40 si hatari tupu?

Extrovert njoo huku umalize utata maana ninyi ndiyo wenyewe...
hakuna home theatre inayoizidi nguvu sea piano.
tofauti iko kwenye ubora wa mziki tu.

vile tumekuwa watu wazima tunaangalia ubora wa vitu sio ujazo(quality/quantity).kama utaweka 1/1 sea piano hapo na home theater pale,unaweza kujiona mjiinga kwa kutoa laki 750 badala ya kutoa 250,ila ubora wa mziki kutoka HT,utakufanya ujipongeze.

tukirudi kwa mada ya ndugu yetu.

kwa ziki la nguvu lenye ubora kama la sabufa Sound bar ni chaguo sahihi,kwa mziki wa kawaida unaotosha na matumizi ya kutizama movie HT ni sahihi zaidi.
tafuta kuanzia watts 600 SB hutajuta,wakati HT watts hizo ni lightweight sounds.
 
Sea Peano toleo la awali kuanza nao maisha geto 2009 Dar, bado una lolote?

Ungekuwa mziki mwingine tofauti na Sea Peano ningekukubalia lakini mbali na hapo bado kabisa, tena eti Subwoofer aina ya Sea Peano ni mziki mnene kwa kaliba ya home theater?

Hata kwa 50% tu Sea Peano haigusi kwa Home Theater LG Watts 1200 LHD 756 toleo la kisasa si kwa mdundo, ubora hata sauti za kwenda mbali zaidi.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom