Abby Newton
JF-Expert Member
- Nov 12, 2017
- 1,227
- 2,197
Upinzani uko hoi bin Taabani.Ni km mgonjwa anaesubiri siku tu ya kwenda kumzika lakini ndugu na jamaa tayari wameshakata tamaa.
Tumefika hapa kwasababu ya kila mmoja wetu anahusika, japo wachache wanaulaumu upande mmoja wa shiringi. Kivipi?
1. Magogoni, Bunge na Mahakama.
Mihimili hii mitatu imetengeneza utatu mtukufu wa kuwabana wapinzani kila kona. Wapinzani hawana pa kupumulia, bila kuvisahau vyombo vya dola.
2. Vyombo vya habari. Hawa wamekuwa very bias katika kueleza habari na "kubalance" mzani.Ni mara chache Wapinzani kupewa "air time"hasa kwenye mainstream media. Praise team imetawala kuanzia asubuhi hadi jioni.
3. Wananchi. Sijui ni mihemko, ulimbukeni, ujinga au uoga baadhi yetu tumeaminishwa na kuamini eti wapinzani ni wapinga maendeleo, vibaraka wa mabeberu na wasioitakia mema nchi hii. Tumesahau kuwa ni hawahawa wapinzani tunaowadharau leo ndio waliosimama kidete kuvumbua "corruption skendo"kubwa kubwa kama Richmond,Dowans, Meremeta, mikataba mibovu ya madini, rushwa kubwa n .k
Ile dhana kwamba wapinzani ndio watetezi wa wanyonge na maslahi ya nchi tumeitupilia mbali. Unafiki umetutawala.
4. Watumishi wa serikali
Hapa namaanisha hasa watumishi wa Halimashauri kama Waalimu, watendaji na maafisa Ugani. Hawa wamekuwa km tawi la chama ndani ya serikali. Waliunda vikundi( Jumuia) kuhakikisha ushindi wa mia kwa mia unapatikana. Sijajua walifanya kwa mapenzi au woga wa kulinda mkate wao. Wamesahau ni wapinzani ndio wamekuwa wakiwatetea wapandishiwe mishahara pamoja na vyeo.
5. Wasomi elimu ya juu.
Imefika hatua Profesa si wa kuheshimika tena. Mtu anadhalilisha elimu yake na kwenda kinyuma na taaluma yake ili mradi tu aonekane akiunga juhudi. Wameogopa kukosoa na kuonya pale mambo yanapooenda ovyo na kubaki wakisifia hata visivyostaili kusifia.
6. Wasanii wa mziki,filamu na vichekesho.
Hawa ndo wameonyesha usanii wa kiwango cha juu. Umeona wapi nchi nzima wasanii wote kuwa chama tawala we umeona wapi?...
7. Viongozi wa dini.
Nina wasi wasi km Bwana Yesu au mtume Muhammed S.A wakirudi leo wanaweza kumpata kiongozi wa dini mwenye hadhi na viwango vya kuingia mbinguni.( Kulingana na imani zetu).
Viongozi wengi wa dini ni wanafiki, waoga na wenye upendeleo.
Wamekubali kutumika na kuegemea upande mmoja. Sifa ya kiongozi bora wa dini ni kusimama katika haki maana Mungu ni wa HAKI.
7. Wapinzani wenyewe.Tamaa ya vyeo, pesa na usaliti,ni kirusi kingine kilichowaangamiza wapinzani wenyewe. Wengi si wapinzani halisia bali ni wafuata upepo wa mafanikio. Ndio maana wengi wapo tayari kuuza utu wao na kutumika kuhujumu vyama vyao.
Hivyo, tunapoendelea kuwashangaa akina Mdee nazani tuendelee pia kujishangaa wenyewe km taifa je tunaelekea wapi? Je ni kweli wapinzani hawana maana tena au sisi ndo hatujielewi?
Nawasilisha