Acheni kueneza uwongo jamani, yaani Sophia Simba kama hajui kiingereza kabisa angeweza vipi kufanya seminars, presentations na madudu kibao ya LLB pale mlimani kuanzia 1987 mpaka 1991?
Hata kama kuna kubebwa lakini asingelijua Kiingereza ingelikuwa ngumu sana kumbeba kwenye masomo yote. Lazima tuelewe LLB sio mahesabu na bila lugha kabisa huwezi kufanya la maana.
Huyo mama is not among the brightest but also she is not dull as some of you guys want us to believe.
China, Urusi, Japan wanatumia Kingereza au lugha zao kuendesha serikali?
Mkulima, hujawahi kusikia digrii za chupi wewe? isije kuwa labda alitumia kamtindo hako na ndio maana mimi sina wasi wasi , kama digrii za namna hiyo zipo sidhani kama atashindwa kutuwakilisha huko, anaweza bwana... yaani WHY ashindwe kama uzoefu wote anao wa miaka nenda rudi!!:smile-big:
Wadau msimlaumu spika au naibu wake kwa kumwondoa sophia kujieleza wakati wa kuomba kura za sadc huyu mama hajui kiingereza kabisa kwa hiyo chama kimelinda aibu""funika kombe mwanaharamu apite""
Labda ungefafanua zaidi nini maana ya Sophia hajui kiingereza kabisa?
Huyu mama amesoma bachelor of law (LLB) pale mlimani miaka ya 80. Sasa kama hajui kiingereza kabisa angewezaje kumaliza masomo hayo?
Naelewa huyo mama aliingia mlimani kama mature student na alikuwa ana struggle na shule lakini kama alimaliza kwa vyovyote hawezi kushindwa kiingereza cha kujieleza. Kumbuka miaka hiyo faculty ya sheria ilikuwa inachukua wanafunzi wacahcahe wenye uwezo (kama 60 kwa mwaka) na mwanafunzi akichemsha tu, ilikuwa inakuwa ngumu sana kumaliza.
Anaweza asiwe na kiingereza kizuri sana lakini sio cha kushindwa kabisa kujieleza.
Kwa kuongezea tu huyu Mama kasoma post graduate nje ya nchi..sasa huko alikuwa anatumia lugha gani? Isitoshe ameongoza ma delegations chungu nzima kwenye mikutano ya kimataifa huko nako alikuwa bubu?
Tuache kuwa na nongwa wakati wote!
China, Urusi, Japan wanatumia Kingereza au lugha zao kuendesha serikali?
Kwa kuongezea tu huyu Mama kasoma post graduate nje ya nchi..sasa huko alikuwa anatumia lugha gani? Isitoshe ameongoza ma delegations chungu nzima kwenye mikutano ya kimataifa huko nako alikuwa bubu?
Tuache kuwa na nongwa wakati wote!
ooooh!!!!!! Sasa ilikuwaje akapewa uwaziri???
kwani kiswahili hajui? Hii nchi lugha ya taifa ni kisw
Nakumbuka kuna wakati fulani waliwahi kumuita Dr alipokuwa wizara ya afya wenye taaluma ya wakaja juu Dr ikafa kifo cha mende, hivyo kujua kiingereza au la kwa ccm si hoja ila kuna umuhimu wa kufuatilia sehemu nyingine alizosoma asije akawa pure kihiyo hatupeleki watu kukaa tu tunataka wenye uwezo wa kuchaganua mambo internationally, lakini alikuwa waziri wa utawala bora pale ni kiswahili atakutana na mzungu gani
Ndio maana walimtoa kwenye kujieleza. Ila jamani aibu nyingine ziwe za hapa kwetu tu, bora hata wangempa cheo kingine hapa ndani kuliko kwenda kutuaibisha huko nje??? Hawa m..wa sijui wanataka tukiwa nje ya nchi tuone aibu ya kutaja taifa tunalotoka kwa aibu ya kuwa na mwakilishi ambae hajui lugha achilia mbali hana uwezo wa kuwakilisha mawazo yenye kujenga nchi. ONE DAY YES!!!!!
Kuna watu wengi wamesoma Chguo Kikuu lakini uwezo wao wa kuongea na kuelewa lugha ya kiingereza ni mdogo ajabu. Kuna watu wamesoma nje ya Tanzania(kwenye nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza) lakini uwezo wao wa kuongea na kuelewa lugha ya kiingereza ni mdogo sana.
Hata sasa nenda kwa watanzania wanaoishi Uingereza unaweza kukuta wengine hata kiingereza bado mgogoro.
Lakini ili kuiwakilisha Tanzania, uwezo wa kuongea kiingereza si kitu kikubwa sana, kikubwa ni uwezo wa kichwa chako kufikiri, kuchanganua, kupima na kuamua. Naweza kusema tukiangalia yaliyopita huko nyuma haya yote ni matatizo kwa Sofia Simba. Hayuko mentally matured kuwa na public office au kuwa representative wa nchi. Kama kigezo ni merit na qualification, i do not think she does.
Kuna watu wanaongea kiingereza vizuri sana lakini IQ yao ni extremely low, wapo wengi tu. Kiingereza si kigezo kizuri cha uwezo wa mtu kufanya kazi.
Tuna mifano mzuri tu hapa Tanzania, Nani kati la Lau Masha na Mrema alikuwa waziri mzuri wa mambo ya ndani? Nani anaweza kuonge kiingereza vizuri?
HAPA bongolander,u is missing the point,mzungu wa barabarani kutojua kingereza does not affect anything,hata wewe mswahili kama hujui kiswahili maadam maisha yako ni ya kula tu uta survive the point ni kwamba huyu bibie carries the hope of tanzanians on her shoulder na katika omba omba yetu(misaada)inabidi awa convince donors sasa kama hawezi kuji express what next-one example MREMA akiwa waziri aliwasili GENEVA miaka hiyo akiwa na assistant ambaye ni fluent in both english and french-huyu assistant hakuwa na off sababu lazima awe by the side of mrema.Hapa ina maana serikali ilingia gharama ya bure sababu kiongozi wake fluency katika lugha ina mgogoroSi wazungu wote wanaojua kiingereza. Na anaweza kujua kiingereza vizuri sana lakini asiwe na uwezo wa kuchanganua hoja, kujieleza hata kuwa articulate. Angalia utendaji wake utawala bora, sikiliza kauli zake alizoongea hapo ndio unaweza kujua uwezo wake.