Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 61,802
- 38,016
mama wa mirembe aja na mpya
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Sophia Simba, amevijia juu vyombo vya habari akidai kwamba vinatumiwa vibaya kumchonganisha yeye na wana CCM wenzake ili kukimaliza chama hicho.
Aidha Simba ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), amezinyooshea kidole baadhi ya nchi za Magharibi bila kuzitaja majina akizituhumu kwamba hazifurahishwi kuona CCM inaoongoza Serikali tangu Tanzania ipate uhuru.
Alitoa tuhuma hizo juzi katika mkutano wake na viongozi na wanachama wa UWT wa wilaya za Iringa, Kilolo na Mufindi uliofanyika mjini hapa.
Simba aliyepata mapokezi makubwa kutoka kwa wanawake wa wilaya hizo na ambao walikuwa wakimkatiza mara kwa mara, katika hotuba yake wakimuita mwanamke jasiri ambaye hawako tayari kumpoteza, aliwataka wanawake hao kujihadhari na vyombo vya habari hasa magazeti kwa madai kwamba yanatumiwa kuwachonganisha.
Yanafanya propaganda chafu dhidi yangu kwasababu wanajua nina watu UWT, wanataka kunimaliza, alisema na kuongeza kuwa pia vyombo hivyo havina nia njema CCM.
Alisema licha ya nia hiyo mbaya ya vyombo hivyo na CCM, pia havimtakii mema Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chao cha kumshinikiza awafukuze baadhi ya wasaidizi wake kwa sababu zisizo na ushahidi wa kutosha.
Vyombo hivi vinatumiwa na watu wanaotaka kuimaliza CCM kwa hiyo ni lazima tushikamane vizuri ili wasiendelee kuuza habari za upotoshaji, alisema.
Alisema amekuwa akishtushwa anaposoma baadhi ya magazeti yanayomuandika kwa uzito wa juu kwamba kwenye baadhi ya vikao vya juu vya chama aliwatukana na kuwavua nguo viongozi wenzake tena mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete.
Mimi siwezi kumtukana mwana CCM mwenzangu kikaoni tena katika vikao vya juu kama Kamati Kuu ambacho Mwenyekiti wake ni Rais wa nchi, alisema.
Kwa upande wa wahisani alisema hawapendi kuona CCM ikiendelea kuongoza Serikali kwa sababu katika Bara la Afrika chama hicho ni moja ya vyama vichache vinavyoendelea kutawala tangu Uhuru