Sophia Mfaume: Wakuu wa wilaya hatuna Magari, tunaazima Halmashauri na kwa RAS

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
137
509
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Mfaume Kizigo amesema Wakuu wa Wilaya hutumia magari ya kuazima Halmashauri na kwa RAS na kwamba leo hutumia gari hili, kesho lile na wakati mwingine huwa wanapanga ziara huku mtu mwenye gari akitaka kulitumia pia.

Ameyasema haya kwenye Mtandao wa X wakati akichangia Mjadala wa kwanini TAMISEMI imetenga kiasi kikubwa cha pesa kununua Magari 56 ya Wakuu wa Wilaya wakati wananchi wakiwa hawana huduma za Msingi.

Screenshot 2024-04-17 091115.png


********
Mdau: Ni lazima uwe na lako mwenyewe hata kama wananchi wana matatizo mengi kuliko wewe kukosa gari lako binafsi.
DC Sophia: Gari sio yangu ni ya ofisi na ofisini hakuna DC peke yake, kuna watumishi wengi.

Mdau: Sikumaanisha serikali ikununulie wewe kama Sofia. Halmashauri ina magari, hata kama ni ya kuchangia, DC ni mtumishi kama watumishi wengine lakini shida yake ya gari (la kutembelea) inakuwa kipaumbele ukilinganisha na shida nyingi tulizonazo kama taifa.
DC Sophia: Bila usafiri atatimizaje majukumu yake uwandani/site? Magari ya halmashauri yana matumizi pia. Ni changamoto sana sema kama huiishi huwezi kujua. Movement ndani na nje ya wilaya inakua issue sana, hapo unahitaji kuzunguka vijijini kuwafikia wananchi.

Mdau: Kwahiyo mkuu unataka kutuambia katibu tawala anapewa gari mkuu wa wilaya (msaidizi wa raisi/ mwakikishi wa serikali kuu kwa ngazi ya wilaya) anakosa.
DC Sophia: RAS pia ni mteule, tena wa ngazi ya mkoa.

Mdau: Hujajibu swali langu mbona.
DC Sophia: Mara ya mwisho nimetumikia ofisi yenye gari ya DC nilikua Namtumbo. Nilipohamia Mkalama hakukua na gari, na hata hapa nilipo hakuna. Changamoto ni kubwa. And yes, Katibu tawala anaweza akawa na gari wakati DC hana.

Mdau: Ingepebdeza zaidi Dr. Zikifika halmashauri mnunue hard top msinunu V8 nibora chenji inayo baki muwajali wananchi na watumishi wanahali mbaya.
DC Sophia: Magari mengi halmashauri ni hardtop na double cabin. Kitu ambacho wengi hapa wanachanganya ni muingiliano wa halmashauri (local Gvt) na ofisi ya DC (central Gvt). Wengi hawajafahamu kwamba kuna utofauti kwa hizi taasisi 2, hivyo hata resources ina mifumo tofauti ya manunuzi.

Mdau: Kwani lazima iwe V8?
DC Sophia: Si lazima.

Mdau: Mhe. samahani naomba kuuliza. Kama ni gari ya ofisi ina maana ofisi kwa sasa haina magari? Mpaka liwepo ambalo linasoma DC ndiyo ofisi itahesabika ina gari? Je DC wa kabla yako alikuwa anatumia gari gani?
DC Sophia: Gari ya ofisi ya DC haisomi DC inasoma STM (kwa sasa). Ofisi kwa sasa haina gari. DC wa kabla yangu aliazimwa gari na RAS, na kabla yake aliyekuwepo aliazimwa pia. Nimeambiwa hakuna gari tangu 2016.

Mdau: Asante kwa majibu mazuri sana mh. Hivi wilaya unayohudumia ww unaona changamoto zilizopo? Je ukiwa kiongozi wa hapo shida zilizopo na kununua gari jipya la 500m ni kipi kinaweza kuwa kipaumbele chako kama kiongozi? Unaweza kuwa tayari watoto wakose vyoo mashuleni ili upate gari?
DC Sophia: Sifahamu gari gani zitanunuliwa ila sidhani kama itacost 500M. My brother kila ķitu kina umuhimu, afya bado tuna safari, elimu, kilimo, miundombinu ya usafiri na usafirishaji... ndio maana sekta zote zinaangaliwa kwa pamoja (at per). Huwezi kufanya hiki kwanza kingine kisubiri.

Mdau: Sikulaumu ww ila nadhani shida ni serikali na vipaumbele vyake. Viongozi wetu wote cha kwanza ni wao wafanye kazi kifahari,waishi maisha ya kifahari halafu shida za wananchi baadaye sana. DC hata RAV4 new inamfaa kwa kazi zake ila serikali inanunua v8 tena itakuwa ya mwaka husika.

Screenshot 2024-04-17 150819.png
Screenshot 2024-04-17 150858.png
Screenshot 2024-04-17 150940.png

Pia soma: Magari 56 ya Wakuu wa Wilaya kununuliwa mwaka wa fedha 2024/25
 
Anatulea Futuhi huyo ,Kila mwaka serikali inatumia zaidi ya Bilioni 580 kununua magari halafu yeye anatuambia hawana magari....Kisha anatuletea comedy kwamba magari 56 serikali isinunue kwanza wakati wananchi wanashida hajui kwamba kila mwaka serikali inatumia 580B kununua magari?
 
Anatulea Futuhi huyo ,Kila mwaka serikali inatumia zaidi ya Bilioni 580 kununua magari halafu yeye anatuambia hawana magari....Kisha anatuletea comedy kwamba magari 56 serikali isinunue kwanza wakati wananchi wanashida hajui kwamba kila mwaka serikali inatumia 580B kununua magari?
Mpeni Gari
 
Huwa wanatetea kwa nguvu zote, wapewe posho ya mafuta watembelee magari yao. Utaona wanavyonunua ist. Lakini ikiwa mlipaji ni mwananchi basi wanataka mavi-80!
Mpeni Gari akizingua mchomoeni problem ni nini akizingua bila Gari kelele amesema ili atimize majukumu anataka Gari au mnunulieni Toyo/Bajaj basi sio kutembea na Boda au kwa MIGUU au kuishia kuombaomba Magari ya wenyewe
 
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Mfaume Kizigo amesema Wakuu wa Wilaya hutumia magari ya kuazima Halmashauri na kwa RAS na kwamba leo hutumia gari hili, kesho lile na wakati mwingine huwa wanapanga ziara huku mtu mwenye gari akitaka kulitumia pia.
Pongezi Sana Dr DC
 
Achen ubinafsi mbona watumishi kibao hawana magari wanatumia daladala na kazi zinafanyika,kwani nyie ni Bora kuliko walimu,manesi,nk
Nesi anafatwa, Mwalimu anafatwa. Huyu anatakiwa kuwafata wananchi hivyo gari ni lazima. Labda kuhoji aina ya gari, kwanini V8? Kwanini si hardtop kama Nissan? Maana ni gari za kazi zile na kampuni nyingi inazitumia.
 
DC anataka kuzunguka na gari kwenda wapi?

Nchi ina sijui DAS, sijui mkurugenzi, mbunge na watumishi kibao wanaotumikia wilaya...
Field mkuu. Walipo wananchi wenye kero zao. Hahaha.
 
Back
Top Bottom