Songwe imepata bilioni 16 kujenga miradi ya maji kwenye Vijiji visivyokuwa na maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,811
11,981
SONGWE: Katika kuongeza asilimia ya upatikanaji wa Maji vijijini kutoka 73% hadi kufika 100% za upatikanaji wa maji vijijini, Mkoa wa Songwe umepata fedha za utekelezaji wa miradi ya maji vijijini shilingi Bilioni 16.4 za lipa kwa matokeo (PfoR) ambazo utekelezaji wake utaanza muda wowote.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brig. Gen. Nicodemus Mwangela amesema miradi ya maji inapojengwa na kukamilika ndio inaongeza asilimia ya upatikanaji wa Maji kwa wananchi wa vijijini.

"Nitoe wito kwa jamii kutunza vyanzo vya maji na kuilinda miradi ili wananchi wapate maji kwa muda mrefu" Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mwangela.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe, Eng. Charles Pambe amesema kitendo cha utekelezaji wa miradi ya maji kupitia force akaunti kumesaidia watalamu kuwajengea uwezo na kutekeleza miradi kwa 100% kwa gharama ndogo tofauti na Mkandarasi na tumejipanga baada ya miaka 3 vijiji vyote viwe na maji Songwe.

Meneja wa RUWASA Mkoa Eng. Charles Pambe amesema Mkoa ulipata fedha Bilioni 5.6 za PfoR kama mbegu kwa ajili utekelezaji wa miradi lakini kutokana na Mkoa kufanya vizuri kwenye utekelezaji zimeweza kuzalisha mara 3 yake Bilioni 16.4 ambazo zitakwenda kwenye vijiji ambavyo havina maji, hivyo tunatarajia kufikisha 90% ya upatikanaji wa Maji vijijini tutakapoanza utekelezaji.

IMG-20210208-WA0067.jpg
IMG-20210208-WA0063.jpg
IMG-20210208-WA0064.jpg
IMG-20210208-WA0065.jpg
IMG-20210208-WA0066.jpg
 
Mbona hujataja vijiji vyenyewe,mfano:-
Mkwajuni
Mwambani
Totowe
Galula
Itaka n.k
 
Back
Top Bottom