Ruvuma kupaa: Ndege za ATCL kuongezwa, vyuo vikuu viwili kuanza Oktoba, mkandarasi barabara ya njombe kukabidhiwa mradi

Mindset100

Member
Joined
Jun 23, 2026
Posts
26
Reaction score
73
RUVUMA KUPAA: NDEGE ZA ATCL KUONGEZWA, VYUO VIKUU VIWILI KUANZA OKTOBA,MKANDARASI BARABARA YA NJOMBE KUKABIDHIWA MRADI

Ongezeko kubwa la abiria wanaoingia na kutoka Songea mkoani Ruvuma sasa limeisukuma Serikali kuongeza safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), hatua inayotarajiwa kuufungua zaidi uchumi wa mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed,akizungumza kwenye kikao maalum cha Halmashauri kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea, amesema safari za ndege zitafanyika Jumapili, Jumatatu na Jumatano, huku Ijumaa ikitarajiwa kuwa na safari mbili ambazo zitafanyika asubuhi na usiku. “Mazungumzo ya mwisho yanaendelea kukamilishwa ili safari hizi zianze rasmi,” amesema.

Katika sekta ya miundombinu, RC Abbas amesema Julai Mosi Serikali inatarajia kumkabidhi mkandarasi mradi wa ujenzi wa barabara ya lami nzito kwa kuanzia kilometa 100 kutoka Songea hadi Lutukira-Madaba pamoja na bypass ya kilometa 16 ndani ya Manispaa ya Songea na kwamba Waziri wa Ujenzi Abdalah Ulega anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.

Wakati huo huo, elimu ya juu nayo inachochewa kwa kasi katika Manispaa ya Songea ambapo RC Abbas amesema Kuanzia Oktoba mwaka huu, vyuo vikuu viwili vya SOCAITE (zamani AJUCO) na Chuo cha Uhasibu Kampasi ya Songea vitaanza kutoa kozi za cheti, diploma na baadhi ya shahada, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za elimu na ajira kwa maelfu ya vijana wa kusini mwa Tanzania.

Ruvuma sasa si tena mkoa wa pembezoni; unajijenga kuwa kitovu kipya cha usafiri, elimu na uwekezaji.
 
Attachments

  • FB_IMG_1782633547097.jpg
    FB_IMG_1782633547097.jpg
    33.9 KB · Views: 12

#RuvumaMpya #ATCL #ElimuYaJuu #MaendeleoYaKusini
 
Ahsante kwa taarifa ila mumchunguze huyo mkandarasi wa barabara asijenge kwa kujikadiria ili baadae ya miaka kadhaa tena apewe tenda ajipigie mabilioni kadhaa
 
Back
Top Bottom