Yote yatapita tu, hakuna lisilo na mwisho. Hebu tujuzeni ni nini kinachoendelea huko muda huu? kwani nimepata simu kutoka huko kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi ametua huko muda si mrefu...:A S embarassed:
Nakumbuka enzi za Lyatonga Mrema...Kwa majibu ya kejeli aliyotoa RPC wa Ruvuma na madhara yaliyotokea huko leo...Mzee wa kibaraghashia tayari angekuwa kisha piga chini mtu....
Halafu ile thread ya vurugu za Songea mbona siioni...imekuwa moved wapi?Msaada wakuu.
Pametulia, polisi wanashika doria ya nguvu. Mhsh Dr. Norbert Mtega ameinanga serikali kuacha majibu ya ujanja ujanja kwenye shida za wananchi. Amesema wawe wepesi kujibu kero za wananchi. Ameendelea kuwa yaliyotokea Arusha, mwanza, mbeya, tabora na songea serikali isipuuze ni ishara kuwa kuna jambo. Amewaasa vizuri sana!
Pametulia kiasi,hatujui wananchi wanafikiria nini,maana wenzao wameuwawa kwa risasi na polisi,hatujui hasira iliyopo mioyoni mwao,mungu atunusuru sisi wasongea isiwe kama ile vita ya wanajeshi na wananchi ya kuchomeana vitu
ningekuwa mwananchi wa mazingira hayo,popote anapoishi polisi panatiwa moto. Ni bora hasara ya nyumba kuliko uhai wetu unaopotea sabab ya wajinga wachache wanaoshirikiana na wezi. Nawachukia polisi kuliko kawaida
Jamani KATIBA ni muhimu sana sana sana.Mkuu wa polisi wa mkoa achanguliwe na wananchi na sio achaguliwe na Mkuu wa polisi wa nchi.TUSIMAME SISI HUKU NJE TULIANDAMANA KWENYE NCHI YA WATU MPAKA WHITE HOUSE NA TUWASILISHA MAOMBI YETU STATE DEPT. YA USA.MAFISADI WANATAPATAPA WAMEBAKIA KICHWA TU ILI WAZAME,NDIO MAANA MNAYAONA HAYA YOTE.TUPIGE KICHWA CHA HUU NYOKA ILI AFE ,ILI WATANZANIA WAWE NA HAKI,AMANI YA KWELI NA WAFURAHIE MAISHA .HAO MAFISADI HAWAFIKI MIA MBILI JAMANI.TUSIRUDI NYUMA TWENDE MBELE SHAMBULIA TU WATAKWISHA
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.