Songea - Madiwani CCM wasusia vikao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Songea - Madiwani CCM wasusia vikao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 7, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hali ya kisiasa CCM Songea yazidi kuwa tete
  MADIWANI wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini wamesusia kikao kilichoitishwa na viongozi wa Chama hicho wilaya kwa kile kilichodaiwa ni mgomo wa kudumu kushinikiza kujiuzulu kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Charles Mhagama. Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwa nyakati tofauti nje ya Ofisi ya CCM ambapo kikao hicho kilipangwa kufanyika walisema kuwa wameshtushwa na taarifa ya kuitwa kwenye kikao hicho bila kuelezwa ajenda zake wala muda wa kukaa kikao hicho Walisema kuwa walifika kwenye kikao hicho na walishindwa kuwaona baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao ndio waliowaita kitendo ambacho kinaonyesha ni dharau dhidi ya madiwani.

  Baadhi ya Madiwani hao Christian Matembo wa Kata ya SeedFarm, Kurabest Mgwasa wa Kata ya Msamala na Faustine Mhagama wa Kata ya Mshangano walisema kuwa kiu kubwa ya madiwani ni kutaka kuona Charles Mhagama ambaye anadaiwa kuwa ni Mstahiki Meya anajiuzulu ili uchaguzi mpya uitishwe kwani kura alizopata wakati wa uchaguzi hazikuwa halali “Tumechoka kuogopana ndani ya chama kwa kuwaacha wachache wawaburuze wengi kwa maslahi yaliyojificha kwani hatuwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa demokrasia vya kuwatisha madiwani waliotimiza haki yao ya kupiga kura za hapana kwenye uchaguzi wa umeya uliopita hivi karibuni kwa kuwaita ni wasaliti wa chama,” alisema Matembo. Alisema kuwa madiwani wengi wamempigia kura za hapana Charles Mhagama, lakini tunashangaa kuona mtu huyo anatembelea gari ya Mstahiki Meya na kufanya kazi kama Meya wakati siku ya kupiga kura uchaguzi ulivurugika na kusababisha madiwani kushikana kutokana na kumkataa Mhagama.

  Diwani wa Kata ya Mshangano Faustine Mhagama ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wote wa CCM alisema kuwa kitendo cha viongozi wa CCM wilaya cha kupendekeza madiwani watano wa chama hicho wavuliwe uanachama ni kuongeza mpasuko ndani ya chama kwani kura walizopiga zilikuwa za siri hivyo kuwahukumu hao ni kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao za msingi.

  Mhagama alisema kuwa kanuni za kudumu za halmashauri zina eleza kuwa jambo lolote litakalofanyika kwenye kikao cha Baraza la Madiwani halipaswi kuhojiwa wala kujadiliwa na mamlaka nyingine hivyo CCM Wilaya ya Songea Mjini kupitia Kamati ya Maadili na Siasa kuwahoji Madiwani kwa kile kilichotokea kwenye Baraza ni kukiuka kanuni na kusababisha utendaji wa kosa kwa makusudi na kuendekeza makundi bila sababu ya msingi “Ili kulinda heshima ya Chama ni vema Charles Mhagama aridhie kujiuzuru nafasi hiyo ili uchaguzi urudiwe upya badala ya kuwanyanyasa baadhi ya madiwani wanaodaiwa kupiga kura za hapana na kusababisha diwani huyo kupitishwa kwa kura za hapana 14 na za ndiyo 12,” alisema Mhagama. Alisema kuwa madiwani wataendelea kususia vikao vitakavyoitishwa na Chama na Halmashauri ya Manispaa ya Songea mpaka uitishwe uchaguzi mwingine ambapo madiwani watamchagua kiongozi watakaomuona anafaa na sio kulazimishiwa kiongozi wasiyemtaka.

  Naye Diwani wa Kata ya Msamala Kurabest Mgwasa alisema kuwa Ccm Wilaya imependekeza Madiwani watano wavuliwe uanachama ambapo hatma yao ipo kwenye ngazi ya chama hicho mkoa, lakini cha kushangaza madiwani hao nao wameitwa kwenye kikao hicho jambo ambalo lingeweza kuleta vurugu kubwa.

  Kwa upande wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini Alfonce Siwale alikiri kuitisha kikao hicho ambacho kilipaswa kifanyike jana lakini kilishindikana kutokana na mahudhurio hafifu ya madiwani ambao hawakufika hata nusu yao. Alisema kuwa madiwani wengi wameshindwa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa wapo safarini na hivyo kikao hicho kimepangwa kufanyika Oktoba 11 katika ofisi za chama hicho na kueleza kuwa madiwani hao hawana mgomo wowote Alieleza kuwa chama hicho kina madiwani 21, lakini waliofika kwenye kikao hicho walikuwa wanane na kufanywa kikao hicho kutofanyika na kwamba kwenye kikao hicho madiwani waliopendekezwa kufukuzwa na chama ndio waliojitokeza kwa wingi.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  watajiju
   
 3. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  twaendelea kushuhudia mengi ndani ya ccm, kazi ipo!
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  kuna mengi yatajulikana muda mfupi ujao
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naona nao wanataka kuvuana magamba! Kuna siri imefichika hapo,
   
 6. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Siri zinaendelea kuvuja wezi wote wanaendelea kufichuana,CCM huwa hawashindi kihalali ila kwa kuiba tu.
   
 7. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Baada ya miaka 50 ya ufungwa na utumwa wa fikra za zidumu fikra za mwenyekiti sasa watu wameanza kufunguka na kupata ufahamu....
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Walipogoma wa Arusha, watu waliuawa na PM akasisitiza uchaguzi ni halali. Huko Songea Meya kapata kura 12 za ndio na 14 za hapana, bado tunaambiwa uchaguzi ni halali!? Tanzania zaidi ya uijuavyo!
  Mbona Mkuchika yuko kimya? Au ndio kunya anye kuku....!?
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Hapo huwezi kumsikia hata kidogo ila wangekuwa wa CDM angechonga sana, na kusema wanataka kuvuruga amani, wanachofanya sasa ni kuwatafutia ban hao madiwani baaaasi.
   
 10. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Si wavuane magamba tuingie kwenye uchaguzi waone wanavyonyolewa kistaraabu
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Wezi wetu wameanza kujiumbua wenyewe. Tusubirie mengi zaid kutoka ccm.
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Hawa magamba Mi naona wameishiwa na fikra.
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Komaeni mpaka kieleweke! Wakiwatimua karibuni chama makini, CDM. Hongera madiwani wote 14 kwa 12. Wapi na wp? CCM wabakaji democrasia!
   
 14. DGMCHILO

  DGMCHILO Member

  #14
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatizo sio madiwani waliopiga kura za NDIYO au HAPANA
  bali tatizo ni huyu NCHIMBI
  ndiye aliyevuruga zoezi zima la uchaguzi wa meya SONGEA
  WATANZANIA tuwe macho sana na mtu huyu ni hatari sana kwa TAIFA letu
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Hatimaye kisu kimefika kwenye mfupa... Wanagomeana wenyewe kwa wenyewe.
   
 16. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ila ccm kuna vituko, yaani madiwani wa ccm songea wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani tena. Yaani ndani ya chama viogozi wanagomeana sasa nani tena itaiamini ccm ikiwa viongozi wenyewe wanageukana. Serious ccm inakufa.
   
 17. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  endeleeni kupasuana,huku wengine wanajenga vyama vyao.
   
 18. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  hivi Nchimbi na bichwa lote lile alikimbiaje na box la kura? CDM Singida is another fish to fry. Ngoja kwanza wazikane......
   
 19. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kujua siri ya wapendanao/washirikianao ngojea wakorofishane/waselewane
  Otherwise you can't.
  mambo mengi yatajulikana
   
 20. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Anguko kuu la magamba linaendelea kupata kasi
   
Loading...