Somo toka kashifa ya kampuni ya NVIDEA

Somo toka kashifa ya kampuni ya NVIDEA

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,073
Reaction score
1,332
Imeripotiwa kwanba Mtendaji Mkuu (CEO) wa (NVIDEA) Kampuni kubwa ya Teknologia ya Marekani ndugu Jensen" Huang mwenye Uraia wa Taiwan na Marekani ameamua kujiuzulu nafasi zake kwenye Kampuni kutokana na kinachodaiwa kuwa na uhusiano nje ya ndoa na mwanamama wa Kichina Alice Huang.

Vyombo vya ulinzi vya Marekani vinadai kwamba Alice Huang ni shushu aliyelelewa na Mamlaka za China za Kiusalama kwa minajili ya kupata taarifa mbalimbali hasa za kiteknojia. Ili Kupata taarifa tajwa kiurahisi, Alice Huang inasemekana aliamua kuwa “ Delila” wa zama hizi kwa kumwinda Jensen" Huang CEO wa Nvidia tuhuma ambazo Mamlaka za kiuchunguzi za Marekani zinazifanyia kazi.

Kwa yanayoendelea kwenye hii Scandal ya Nvidia, Jensen" Huang na Alice Huang Je tuna yepi ya kujifunza kama nchi? Je hizi intermarriage na majirani zetu (Nchi) nazo zinachunguzwe (vetted) kwa kina?
​
 
jana sema ujachelewa.
angalia hisa zilivyoshuka.
anyway wanawake wanaojiu...wako kibao unahangaika na ambaye sgeria za kampuni haziruhusu na ni hasara.
mchina naye japo 49+ ila akamtega na chip ni vita ya dunia
 
Back
Top Bottom