Somo la uzalendo 🇹🇿 🇺🇸

Somo la uzalendo 🇹🇿 🇺🇸

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,088
Reaction score
136,599
Kwangu elimu haina darasa. Elimu haina kuhitimu wala wahitimu. Elimu ni jambo endelevu.

Moja ya elimu yangu ninayojivunia ni fursa niliyoipata ya kuweza kutembelea sehemu mbalimbali hapa duniani. Na si kutembelea tu, bali hata kuishi na kufanya kazi.

Kati ya somo nililoweza kujifunza ni hili la kitu kinachoitwa uzalendo.

Uzalendo huu nauzungumzia katika muktadha wa nchi mbili: Tanzania na Marekani.

Kwa yeyote ambaye kaishi Marekani na Tanzania kwa muda wa kutosha [fanya makadirio yako mwenyewe muda wa kutosha ni kiasi gani], atakubaliana na mimi kuwa Wamarekani wapo kwenye kiwango kingine kabisa katika kuonyesha fahari ya uzalendo kwa nchi yao.

Katika utaifa wa kisasa, bendera huwa ndo alama bainishi ya nchi/ taifa.

Wamarekani wengi, bila kujali wanatoka kwenye kada ipi, ni watu wanaolipenda kwelikweli taifa lao.

Na mapenzi hayo huonyeshwa na vile ambavyo hupenda kupeperusha bendera ya taifa lao.

Iwe ni kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati, cha juu na kadhalika, uzalendo wao huonyeshwa na vile wanavyopeperusha bendera yao kwenye makazi yao, kwenye magari yao, sehemu zao za kazi na biashara, na kadhalika.

Ona mfano huu kwa mfano. Kwa muonekano tu wa mazingira, hapo panaonekana ni eneo la watu wenye kujiweza.


040B1971-2AC1-4D51-A538-7396D735A24C.jpeg



Sasa hebu angalia na hii. Kwa muonekano tu unaweza kuhitimisha kuwa aishiye hapo si mtu wa kipato kikubwa. Ni ki trailer tu kilichojichokea.

1AF84AC2-28A9-40F1-A5C3-2E9EBFBE0574.jpeg


Sasa jiulize ni kitu gani hapo unachokiona kilichopo kwenye picha zote mbili? Ni bendera!

Uzalendo wa hivi bado sijauona Tanzania. Sababu hasa sijui ni ipi.

Hivi kwa mfano nikiamua kuweka kamlingoti kadogo nyumbani kwangu halafu nipeperushe bendera yetu ya Tanzania, nitasumbuliwa na watu wasiojulikana licha ya kwamba lengo langu la kufanya hivyo ni uzalendo?

Hili suala la bendera na uzalendo Mzee Mwanakijiji aliwahi kulidokeza siku za hapo nyuma.
 
Marekani wana Viongozi Tanzania tuna Watawala.
Maisha yetu yanategemea na Watawala wameamkaje. Kuna watu Walishakamatwa kisa Wamevaa T-shirt yenye Maandishi Ukuta, pray for Lissu.. Nk
Kuweka Bendera inaweza kuwa Kosa kwa Tanzania ya sasa .
 
Mhh! Bendera!
Kama ofisi za polisi au shule watu wanaenda pale wamependeza na wana hadi vitambi, bendera zao zimechakaa vile za majumbani si zingekuwa uchafu.

Uzalendo wa bendera kwenye umaskini ni ngumu.
 
Marekani wana Viongozi Tanzania tuna Watawala.
Maisha yetu yanategemea na Watawala wameamkaje. Kuna watu kwa Walishakamatwa kisa Wamevaa T-shirt yenye Maandishi Ukuta, pray for Lissu.. Nk
Kuweka Bendera inaweza kuwa Kosa la kwa Tanzania ya sasa .

Kwani unadhani Marekani kila raia anakubaliana na viongozi waliopo madarakani?
 
Marekani wana Viongozi Tanzania tuna Watawala.
Maisha yetu yanategemea na Watawala wameamkaje. Kuna watu Walishakamatwa kisa Wamevaa T-shirt yenye Maandishi Ukuta, pray for Lissu.. Nk
Kuweka Bendera inaweza kuwa Kosa kwa Tanzania ya sasa .
Marekani wana tume huru ya uchaguzi huku mmmm.... 'comments reserved'
 
  • Thanks
Reactions: prs
Mhh! Bendera!
Kama ofisi za polisi au shule watu wanaenda pale wamependeza na wana hadi vitambi, bendera zao zimechakaa vile za majumbani si zingekuwa uchafu.

Uzalendo wa bendera kwenye umaskini ni ngumu.

Mbona Marekani maskini wapo wanaopeperusha bendera kwenye makazi yao.

Ona hiyo picha ya pili hapo.
 
Umenikumbusha Waingereza walikuwa wanawasema Wamarekani.

Wakasema ukienda restaurant, ukinunua juice/ soda ya fountain, refil ni bure. Hawakuelewa hiyo concept.

Wakasema jamaa wanapenda bendera haoo, kila sehemu bendera!
 
Tanzania kwa miaka mingi ilikuwa ni kuinajisi bendera ya Taifa ikitumika tofauti na majengo ya serikali na mashule.
Nadhani ilikuwa jinai hata kuwanayo tu bendera,wakati wenzetu wakitumia kutengeneza hadi mavazi,na vitu mbalimbali vya urembo.
Nakubali kwa Marekani na Brasil(z) ndiyo nchi zilizo juu sana kwa matumizi ya bendera zao kama alama ya uzalendo,Brazil mtu anavaa chini rangi ya kijani na juu atavaa njano au atachanganya anavyoona inapendeza ilimradi amevaa alama za Taifa lake.
Haya ya kwetu sasahivi ndiyo kidogo yamelegea lakini ilikuwa ni kitu kizito na kigumu kuamua kukitumia.
 
Umenikumbusha Waingereza walikuwa wanawasema Wamarekani.

Wakasema ukienda restaurant, ukinunua juice/ soda ya fountain, refil ni bure. Hawakuelewa hiyo concept.

Wakasema jamaa wanapenda bendera haoo, kila sehemu bendera!

Came to do some grocery shopping at Kroger....just right now.

C2A979DD-AEC6-4AB7-A1FB-6F304B1E9ACC.jpeg
 
Hata kwenye fast food restaurants....bendera zinapepea tu.

497DE165-04C2-47E3-BF9E-CE1AE92122A4.jpeg
 
Uzalendo unajengwa kutoka moyoni kwa vitendo kuanzia ngazi ya familia, shule na makazini. Uzalendo haujengwi kwa bendera au vyama vya siasa

Kama ni hivyo basi hamna hata haja ya kuwa na bendera, siyo?
 
Back
Top Bottom