Somo la uzalendo 🇹🇿 🇺🇸

Somo la uzalendo 🇹🇿 🇺🇸

Ukitembea sehemu mbalimbali Tanzania pia utaona bendera za CCM zinapepea kwenye nyumba nyingi ,magari mengi nimeyaona yakiwa na bendera na nembo za CCM, ofisi nyingi zina picha ya Mh.Rais,huu wote sio uzalendo kwako?

Nazungumzia uzalendo wa taifa; siyo unazi wa chama au vyama.
 
Hii Mada Ya Kuonyesha Uzalendo Kwa Kupeperusha Bendera Imenikaa Kwa Kweli.,,,,,,,wakuu Niombe Kuuliza Hivi Ikitokea Umeamua Kumiliki Bendera Yako Kiuzalendo ,,Taratibu Za Kuipandisha Na Kuishua Kila Siku Zitakuwa Ni Zile Zile Za Kupuliza Filimbi Ili Watu Wapitao Karibu Na Makazi Yako Wasimame Au Waweza Kuishusha Kiholela Tuu,,,,,, Halafu Nipende Kujuzwa Bei Ya Bendera 1 Na Mahali Pa Kuipata Hata Kama Ni Kwa Kufuata Taratibu
Taaratibu Ni zile zile bendera zinauzwa kwenye maduka ya bohari
 
Huku Tanzania uzalendo unapimwa kwa kupeperusha bendera za CCM kwenye nyumba,ukitembea huko maeneo ya pwani unakuta mtu nyumba ya tembe kaweka bonge la bendera ya kijani,yaani sisi ndiyo uzalendo wetu.
 
Usifananishe USA na vitu vya kijinga kasome emblem act ya mwaka1971 ndio uje upost
 
Uzalendo hauletwi kwa kuvaa Bendera ,wapo walio Vaa hizo Bendera na wengine wamezishonea kwenye Makaunda Suti yao na Dhamana tume wapa lakini ndio wa kwanza kuiuza Nchi kwa kuingia Mikataba isiyo na maslahi na Taifa lao.

Uzalendo unajengwa na mambo mengi ,kama kweli hawa Viongozi wetu wangekuwa Wazalendo tusingekuwa na Hali mbaya hivi Kiuchumi na kisiasa.Uzalendo hauletwi kwa kuhubiriwa kama Matangazo ya Biashara.
 
Kwangu elimu haina darasa. Elimu haina kuhitimu wala wahitimu. Elimu ni jambo endelevu.

Moja ya elimu yangu ninayojivunia ni fursa niliyoipata ya kuweza kutembelea sehemu mbalimbali hapa duniani. Na si kutembelea tu, bali hata kuishi na kufanya kazi.

Kati ya somo nililoweza kujifunza ni hili la kitu kinachoitwa uzalendo.

Uzalendo huu nauzungumzia katika muktadha wa nchi mbili: Tanzania na Marekani.

Kwa yeyote ambaye kaishi Marekani na Tanzania kwa muda wa kutosha [fanya makadirio yako mwenyewe muda wa kutosha ni kiasi gani], atakubaliana na mimi kuwa Wamarekani wapo kwenye kiwango kingine kabisa katika kuonyesha fahari ya uzalendo kwa nchi yao.

Katika utaifa wa kisasa, bendera huwa ndo alama bainishi ya nchi/ taifa.

Wamarekani wengi, bila kujali wanatoka kwenye kada ipi, ni watu wanaolipenda kwelikweli taifa lao.

Na mapenzi hayo huonyeshwa na vile ambavyo hupenda kupeperusha bendera ya taifa lao.

Iwe ni kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati, cha juu na kadhalika, uzalendo wao huonyeshwa na vile wanavyopeperusha bendera yao kwenye makazi yao, kwenye magari yao, sehemu zao za kazi na biashara, na kadhalika.

Ona mfano huu kwa mfano. Kwa muonekano tu wa mazingira, hapo panaonekana ni eneo la watu wenye kujiweza.

View attachment 1149927

Sasa hebu angalia na hii. Kwa muonekano tu unaweza kuhitimisha kuwa aishiye hapo si mtu wa kipato kikubwa. Ni ki trailer tu kilichojichokea.

View attachment 1149929

Sasa jiulize ni kitu gani hapo unachokiona kilichopo kwenye picha zote mbili? Ni bendera!

Uzalendo wa hivi bado sijauona Tanzania. Sababu hasa sijui ni ipi.

Hivi kwa mfano nikiamua kuweka kamlingoti kadogo nyumbani kwangu halafu nipeperushe bendera yetu ya Tanzania, nitasumbuliwa na watu wasiojulikana licha ya kwamba lengo langu la kufanya hivyo ni uzalendo?

Hili suala la bendera na uzalendo Mzee Mwanakijiji aliwahi kulidokeza siku za hapo nyuma.
Chini ya Utawala wa huyu dikteta wa Kihutu jaribu sasa kupeperusha bendera kama hivyo hapa Tanzania kama hutapewa kesi ya kujaribu KUMPINDUA Maguzijuto...cheza na akili matope ya kijani wewe!
 
Kwangu elimu haina darasa. Elimu haina kuhitimu wala wahitimu. Elimu ni jambo endelevu.

Moja ya elimu yangu ninayojivunia ni fursa niliyoipata ya kuweza kutembelea sehemu mbalimbali hapa duniani. Na si kutembelea tu, bali hata kuishi na kufanya kazi.

Kati ya somo nililoweza kujifunza ni hili la kitu kinachoitwa uzalendo.

Uzalendo huu nauzungumzia katika muktadha wa nchi mbili: Tanzania na Marekani.

Kwa yeyote ambaye kaishi Marekani na Tanzania kwa muda wa kutosha [fanya makadirio yako mwenyewe muda wa kutosha ni kiasi gani], atakubaliana na mimi kuwa Wamarekani wapo kwenye kiwango kingine kabisa katika kuonyesha fahari ya uzalendo kwa nchi yao.

Katika utaifa wa kisasa, bendera huwa ndo alama bainishi ya nchi/ taifa.

Wamarekani wengi, bila kujali wanatoka kwenye kada ipi, ni watu wanaolipenda kwelikweli taifa lao.

Na mapenzi hayo huonyeshwa na vile ambavyo hupenda kupeperusha bendera ya taifa lao.

Iwe ni kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati, cha juu na kadhalika, uzalendo wao huonyeshwa na vile wanavyopeperusha bendera yao kwenye makazi yao, kwenye magari yao, sehemu zao za kazi na biashara, na kadhalika.

Ona mfano huu kwa mfano. Kwa muonekano tu wa mazingira, hapo panaonekana ni eneo la watu wenye kujiweza.

View attachment 1149927

Sasa hebu angalia na hii. Kwa muonekano tu unaweza kuhitimisha kuwa aishiye hapo si mtu wa kipato kikubwa. Ni ki trailer tu kilichojichokea.

View attachment 1149929

Sasa jiulize ni kitu gani hapo unachokiona kilichopo kwenye picha zote mbili? Ni bendera!

Uzalendo wa hivi bado sijauona Tanzania. Sababu hasa sijui ni ipi.

Hivi kwa mfano nikiamua kuweka kamlingoti kadogo nyumbani kwangu halafu nipeperushe bendera yetu ya Tanzania, nitasumbuliwa na watu wasiojulikana licha ya kwamba lengo langu la kufanya hivyo ni uzalendo?

Hili suala la bendera na uzalendo Mzee Mwanakijiji aliwahi kulidokeza siku za hapo nyuma.

Naamini kwa Wamarekani wanaamini ktk Uzawa na si Uzalendo.

Uzalendo kwa Tz uko kwa chama twawala, na uzalendo wao ni mbioza mwenge, Sera zetu ni NA HATA HILI LITAPITA TU NA TUTASAHAU, tushasahau la Jana, tunasubiri kesho ifike na ipite

Hata hivyu uzalendo wa bendera ni uvivu tu wa kufikiri.

atakubaliana na mimi kuwa Wamarekani wapo kwenye kiwango kingine kabisa katika kuonyesha fahari ya uzalendo kwa nchi yao.
Wakati wa pambano la Mayweather and Mcgregor watu waliacha kupeperusha bendera ya Marekani na kupeperusha ile ya jamhuri ya Ireland, hapo utaona unafiki wa uzalendo wa bendera.

Na siku congress itakapo kubali reparation kwa ADOS (American descendants of slaves) hizo bendera hutaziona kwa hao hillbillies.
 
Back
Top Bottom