Wanabodi,
Kuna msemo unaosema kuwa, ukijibishana na kichaa na wewe unakuwa ni kichaa. Kwa maana nyingine, ukijibishana na "mpiga porojo" na wewe unakuwa ni "mpiga porojo".
Kwa viongozi wa CHADEMA kama wanavyopenda wananchi waamini, Nape Nnauye ni "mpiga porojo" lakini katika "porojo hizo", wanatumia nguvu kubwa katika kuzijibu. Kwa sisi tunaoangalia kwa mbali tunaachwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu zaidi ya kurudi kwenye usemi wa mwanzo na kuwa na hitimisho kuwa basi hata viongozi wa CHADEMA nao ni "wapiga porojo" (manzi ga nyanza) na kama sivyo, basi inawezekana maneno ya Nape Nnauye yakawa yamebeba ukweli ndani yake mpaka kufikia kujibiwa kwa nguvu na viongozi wengi wa chama kinachotaka watu wakiamini kama ni makini katika utendaji wake (damage limitation).
Watanzania kwa sasa hatuutumikishi ubongo wetu katika kujenga hoja na maswali magumu na kuyatafutia majibu na suruhisho mbadala badala yake tunaridhika kuwa kwenye "comfort zone" za kimaskini katika mawazo na fikra kuimba nyimbo zilezile ambazo wanasiasa wanaziimba.
Ndiyo maana hata wanasiasa wetu wako kwenye "comfort zone" za kimaskini katika mawazo na fikra. Kwa mawazo haya, Siyo kitu cha kushangaza pale wanasiasa wa vyama vyetu vikuu nchini wanapoanza kujadili kwa wiki nzima achilia mbali sekunde tano kuhusu kadi ya chama ( unayo, sina, mwanachama, siyo mwanachama ). Silly politics.
Nchi inahitaji jamii yenye mawazo na fikra pevu katika kupambana na changamoto za karne ya 21 na hii itatokea kama Wananchi wataondokana na hizi siasa za matukio na mufilisi.
Kama hivyo vyote vipo, basi siasa za Tanzania zina kansa ambayo inatakiwa "amputation" ndani ya fikra za wananchi kwa sababu nchi haiwezi kujengwa kwa porojo za kisiasa kama hizi bali kwa fikra malidhawa na zenye maono ya kukabiliana na changamoto za karne hii ya sayansi na tekinologia.