Somo kwa Baraza Jipya la Mawaziri wa Serikali ya CCM!

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,642
2,000
Wana JF,

Nina hakika kwa sasa kila Mtz anasubiria kwa hamu kusikia Rais Kiwete akitaja safu ya Baraza jipya la Mawaziri baada ya mtikisiko wa Operesheni Tokomeza Ujangiri ambayo imeacha Mawaziri wanne wakifutwa kazi. Hii itakuwa ni mara ya 3 au 4 kwa Rais Kiwete kufumua Baraza lake la Mawaziri.

Pamoja na Semina na Warsha za Ngurundoto inaonekana Mawaziri hawakuwahi wala hawajawahi kuelewa somo.Kwa mtaji huo Kiwete atendeleakubadilisha Mawaziri kila wakti kwa vile inaonekana kuna tatizo kubwa katika uteuzi wa Mawaziri wa Serikali ya CCM. Ni dhahiri na siyo siri kuwa Mawaziri wengi wanapewa nafasi hizo kiundugu,kiushikaji,kiurafiki,kiudini na pengine kiumakundi ndani ya Serikali ya CCM.

Mawaziri wengi hawapewi kulingana na Uweledi wao(professionalism) katika maeneo husika(wizara).Nakumbuka Rais Kiwete kuna wati akiwahi kutamka kuwa Uwaziri HAUSOMEWI! Nafikiri hii haikuwa lugha sahihi. Pamoja na kwamba Uwaziri hausomewi ni lazima Waziri anayetuliwa kwenye nafasi husika awe na uweledi wa Wizara hiyo hata siyo core business kwenye wizara husika lakini awe na utaalamu wa Kuongoza na Kusimamia( Management and Administration). Kuna Wizara kama ya Afya, huwezi kuweka kwenye Wizara hiyo mtu ambaye amesomea UALIMU(Teaching) au SHERIA(Laws) hataweza, kuna mahali atachemka tu maana siyo profession yake!

Kuna msemo unasema hivi, ninanukuu ''PEOPLE DELIVERS WHAT YOU INSPECT NOT WHAT YOU EXPECT'' mwisho wa kunukuu. Maana yake ni nini. Kwamba watu watakuletee kitu kizuri tu iwapo wewe mwenyewe umekigua na si vinginevo. Kama unakaa tu ofisini ukitegemea uletewe kitu kizuri bila ya kukagua sahau!

Ndiyo maana leo tunazungumzia Mawaziri mizigo. Kama Waziri anakaa ofisini tu kupulizwa na kiyoyozi, kusaini mikataba ya kifisadi na kuidhinisha vocha na hundi za vikao visivyoisha vya semina,warsha,makongamano na mikukuta lazima atakuwa mzigo. Waziri anayekaa ofisini kupigwa kiyoyozi(AC) na akitoka ofisini anaingia kwenye Shangingi na na anaendelea kupulizwa na baridi ya kiyoyozi cha Shangingi halafu anategemea BIG RESULTS NOW lazima awe mzigo!
Kwa Mawaziri kama lazima itakula kwao. Operesheni Tokomeza Ujangiri imeonyesha wazi kuwa hawa jamaa 4 waliotimuliwa walikuwa ni aina hiyo ya Mawaziri! BIG RESULTS NOW imekuwa BIG RESULTS NOT!!!!

Huwezi kupata BIG RESULTS NOW kwa kujifungia ofisini! No sir. Mwalimu JK Nyerere(RIP) pamoja nakuwa Mkuu wa nchi kama Rais alikuwa anatoka kwenda kutembelea Wananchi. Kuna picha zinaonyesha alikuwa akifka kwenye mashamba ya Vijiji vya Ujamaa anashika jembe na kupiga ngwe! Huu ndiyo uongozi. Siku zote Mwalimu alikuwa akiwaambia watu kuwa kuongoza ni kuonyesha njia. Leo hii ni vigumu sana kupata viongozi aina ya Mwalimu. Inashangaza kuwa mtu akishapata madaraka whether ya Uwaziri,Ubunge,U-RC,U-DC ni kufikiria namna ya kuifisadi Tanzania kwa kutumia wadhfa aliopewa!

Chonde chonde wale mtakaoteuliwa ikiwa ni kwa sababu za kishikaji,kiurafiki,kiundugu,umakundi au kidini lazim mjipime, mtafkari na kuona kama kweli mnastahili na mtaweza kusimamia na kuongoza Wizara hizo. Kama mnafikiri Uwaziri ni kuuchinja/kuukata au kufaidi nchi basi muda si mrefu hizo ofisi mtaziona za moto na itakula kwenu. Kuongoza ni kuonyesha Njia. Kuna tofauti kubwa sana ya Kuongoza na Kutawala. Pengine ndiyo maana kila siku Chama Twawala CCM kila siku kuna kuwa na mabadiliko ya Baraza la Mawaziri kwa vile wa n Watawala na si viongozi! Mtawala hana tofauti na Dikteta. Hawa wote hutawala kwa mabavu na kwa kulazimisha mabo bila kutumia busara. Kwa mtawala au Dikteta kwake neno Demokrsia ni nadra kutamkwa. Yuko tayari kuua wale wale anaowatawala ili abakie madarakani!!!Kwa sasa Tanzania imeshaanza kuelekea kwenye mkondo huo. Tumeshuhudia Watawala wa CCM wanavyopambana na vyama vya upinzani kwa kuratibu hata mipango ya mauaji ili waendelee kutawala nchi hii milele!(kwa kauli zao wenyewe). Kumbukeni Watanzania wa sasa wameelimika, wamesoma na wanaelewa mambo kwa upana mkubwa kuliko hata baadhi ya Mawaziri.

Karibuni kwenye Baraza jipya la Mawaziri na kazi kwenu.
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Solution iko kwenye rasmu ya katiba mpya. MAWAZIRI WASIWE WABUNGE. Ili rais awe na wigo mpana wa kuchagua mawaziri competent kulingana profesionalism zao.
 

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,642
2,000
Solution iko kwenye rasmu ya katiba mpya. MAWAZIRI WASIWE WABUNGE. Ili rais awe na wigo mpana wa kuchagua mawaziri competent kulingana profesionalism zao.

Bobuk;

Tatizo hapa siyo issue ya Mawaziri kutokana na Wabunge.Tatizo ni mfumo wa uteuzi na uweledi wa maeneo husika.

Hata kama Mawaziri hawatatokana na Wabunge bado haiwezi kusaidia sana. Ukilitazama hili nalo kwa Jicho la Tofauti utakuta kwamba mambo karibu ni yaleyale na watu ni haohao. Suppose Mimi nina uhakika wa kuchukua nchi kama Rais/Chama changu, naweza nikawaambia watu wangu wa karibu kuwa wasigombee Ubunge wasubiri Uwaziri.

Kwa hiyo nikishaingia Ikulu natangaza baraza la Mawaziri kutoka kwenye Timu yangu ambayo haikugombea Ubunge.
Tunachotaka ni professionalism; kama ni Waziri wa Fedha awe ni Mchumi aliyebobea kam kina Prof. Lipumba, kama ni Waziri wa Nishati na Madini awe ni mtu aliyesomea Nishati yenyewe kwa maana ya Umeme(Electrical Engineer) tena mwenye Udaktari. Kama ni Waziri wa Afya, basi awe na elimu ya Udaktari wa Afya( Doctor of Medicine) kwakiwango cha PhD.

Kama ni Waziri wa Mambo ya Ndani, basi tujue ni mtu aliyebobea katika mambo ya Ulinzi na Usalama wa Raia/Sheria au amepitia kwenye Upolisi wenyewe hasa.Kama ni Waziri wa Sheria awe ni Mwanasheria na azijue sheria za Nchi na za Kimataifa. Hali kadhalika kama ni Waziri wa Kilimo awe ni msomi mwenye Elimu ya Kilimo kutoka SUA au chuo kingine chochote kinachotoa Elimu inayofanana n hiyo.Hali kadhalika kwenye Mifugo, Maji, Ujenzi n.k.na hao Mawaziri lazima wafike Site(kwenye maeneo ya kazi zao) ili waone kwa vitendo nini kinafanyika huko site na waelekeze mahali ambapo wataalamu wao walioko chini wanapokosea.

Hatutaki Mawaziri wanaokaa ofisini na kupungwa upepo wa viyoyozi huku kazi zikiharibika.

Namalizakwa kumnukuu Kangi Lugola-MB wa Mwibara-CCM. Alisema hivi,''Mhe.Waziri Mkuu tumekupa usafiri wa Magari na Ving'ora na Ndege masaa 24,Ulikuwa wapi wakti Jeshi na Polisi wakiua Raia na Mifugo kwenye opereshani Tokomeza Ujangiri???''

Swali la Mhe. Lugola lina mantiki sana. Kwamba wakti haya madudu yakifanyika huko porini kwenye zoezi la Operesheni Tokomeza Ujangiri si Pinda,si Emmanuel Nchimbi,si Balozi Kagasheki wala Vuai Nahodha aliefika kwenye matukio kushuhudia kilichokuwa kinafanyika. Hilo ndilo limewagharimu.

They just thought and believed their people under them/their sub ordinates that they gonna deliver what they expected! The poor Ministers were supposed to visit and inspect their respective areas of expertise to see what was exactly happening on the battle field!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom