Somo kutoka Afrika Kaskazini; JK na CCM wangeshindwa 2010 wangekubali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo kutoka Afrika Kaskazini; JK na CCM wangeshindwa 2010 wangekubali?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ibrah, Feb 18, 2011.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Siasa za Tanzania hazina tofauti sana na siasa za nchi nyingi za Kiafrika, ukiondoa Ghana, Botswana na Afrika Kusini. Chaguzi zetu huwa zinajaa utata mwingi na mara nyingi hazitoi matokeo halisi kulingana na matakwa ya wapiga kura. Kwa maana nyingine ni kuwa huwa kunakuwa na ubakaji mkubwa wa demokrasia na uchakachuaji wa hali ya juu wa matokeo. Katika hali ya kawaida huwa si ajabu mara zote katika nchi nyingi za Kiafrika kura za maoni au maoni ya Waangalizi kuwapa nafasi kubwa ya ushindi Viongozi wanaotawala wakati huo (mfano Uganda kwa sasa).

  Mambo yaliyotokea Tunisia na Misri mwaka huu na yanayoendela sehemu nyingine yamenifanya nitafakari uchaguzi wetu wa mwaka jana 2010 na athari ambazo pengine zingetokea kama matokeo yangeonyesha kuwa Rais Kikwete na CCM wameshindwa. Katika Uchaguzi wa Kenya miaka michache iliyopita mshindi halali hakujulikana; hii ni kwa sababu Tume ya Uchaguzi ya Kenya ama haikujipanga vizuri au ilikubali kutumiwa vibaya na Watawala kiasi kwamba Rais Kibaki akaapishwa haraka haraka akiwa Ikulu!

  Turejee yaliyotokea Misri na Tunisia. Katika chaguzi zilizopita aliyekuwa Rais wa Tunisia Ben Ali alishinda kwa kishindo cha asilimia 99! Vivyo hivyo ailiyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubaraka naye mwaka 2005 alishinda kwa kishindo cha asilimia 88.7, na Chama chake kikapata asilimia 80 katika viti vya Bunge la Misri!

  Kinachonifanya nitafakari hayo ni vishindo vya ushindi wao dhidi ya vishindo vya maanguko yao! Inakuwaje, na inawezekanaje ndani ya miaka 5 tangu chaguzi zifanyike na kupata ushindi mkubwa kiasi hicho wananchi wa nchi hizo washindwa kuvumilia na kusubiri chaguzi zinazofuata? Ben Ali wa Tunisia na Mubarak wa Misri wote, baada ya mbinyo wa Wananchi walitangaza kutogombea kunye chaguzi ambzo zingefuatia; Misri ilikuwa wafanye uchaguzi mwaka huu (sina hakika Tunisia), lakini ajabu ni kuwa Wananchi hawakuwa tayari kusubiri chaguzi hizo! Ina maana gani? Hii inamaanisha kuwa hawakuwa na imani na matokeo ya chaguzi hizo maana haiwezekani ndani ya miaka 5 upate ushindi wa asilima 90 halafu kabla ya muda wa miaka 5 kuisha Wananchi wanakufukuza!

  Uchaguzi uliopita Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni milioni 19! Lakini watu waliojitokeza kupiga kura hawakuzidi milioni 8! Hii inaonyesha kuwa hata Watanzania bado hawaridhiki na mwenendo wa chaguzi zetu, Tume ya Uchaguzi yenye ambayo kwa miaka imelalamikiwa na Wapinzani (na ni kweli haiwezi kwenda kinyume na matakwa ya walioichagua maana si Tume Huru).

  Hibyo si jambo la kushangaza kuona kuwa watu milioni 11 hawaoni sababu ya kupiga kura; hii ni kwa sababu hawana imani kuwa kura zao zinaweza kubadilisha chochote! Na ndio maana Wamisri na Watunisia hawakutaka tena kungojea kupiga kura kwenye chaguzi maana chaguzi zetu huwa ni viini macho;tazama uchaguzi wetu wa 2010. Ilifika wakati wananchi wakachoka kusubiria matokeo wanayoyajua yatangazwe na Tume ya Uchaguzi kwenye ngazi za Udiwani na Ubunge na kuanza kuwashinikiza watendaji wa Tume kutangaza matokeo. Kwangu mimi ni ishara mbaya sana kwa nchi yetu; inamaanisha kuwa Wananchi wamepoteza imani kwa Tume ya Uchaguzi na hata Watendaji waliopewa dhamana kwenye ngazi za Majimbo na Kata.

  Tendo la asilimia 80 ya wapigha kura kutojitokeza kupiga kura inamaanisha kuwa kura zao hazina nguvu ya maamuzi ya kubadilisha Uongozi wa nchi yao (kama Misri na Tunisia ambao hawakutaka kusubiria chaguzi). HII NI ISHARA MBAYA.

  MAONI YANGU
  Serikali yetu isipuuze yaliyotokea Misri na Tunisia na yanaoyoendelea mataifa mengine ya Kiarabu. Tukubali tusikubali tunapoelekea ni huko kama mabadiliko yafuatayo hayatafanyika kabla ya uchaguzi ujao wa 2015:-

  Moja, Ni vema tukapata Katiba mpya kabla hatujaingia kwenye uchaguzi ujao; naamini inawezkekan ikiwa tutalifanya jambo hilo kuwa kipaumbele chetu na kujiweka timeframe- muda wa kuapata Katiba mpya maana Wanasiasa na Watawala wanaweza kuitumia kasoro hiyo ama kuhalalisha ukandamizaji wa demokrasia au kuchochea vurugu.

  Pili; iundwe tume Mpya ya Uchaguzi iliyo huru kabla ya mwaka 2015.

  Kitendo cha Watanzania wengi kutokupiga kura ni ishara kuwa ama hawaridhiki na uendeshaji wa Uchaguzi nchini au wanahisi kura zao haziwezi kuamua ni Kiongozi gani wanamtaka.

  CHONDECHONDE VIONGOZI NA WATANZANIA WENZANGU! Tusitoe nafasi ya amani ya nchi hii kuchezewa, sisi sote tuna dhamana ya kutunza amani yetu. Watawala wasisubiri upepo huu uliotoka Misri na Tunisia kuelekea Ghuba uvume kuelekea kusini mwa Bara letu la Afrika.

  HATUKO SALAMA!
   
 2. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jk na ccm wangeshindwa 2010 wangekubali?

  Sahihisho:jk hakushinda uchaguzi 2010 na alichofanya unakijua!
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawakushinda na kilichotokea wote tunakifahamu
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nanyoosha mikono. "wangeshindwa" wangekubali?
   
Loading...