Somo Kuhusu Programu/Software Bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo Kuhusu Programu/Software Bandia

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jun 1, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yona Fares Maro
  The ICT Pub

  SOMO KUHUSU PROGRAMU/SOFTWARE BANDIA

  Kumekuwa na ulanguzi wa programu/software haswa za kompyuta zinazofanywa na watu mbalimbali haswa kwenye nchi ambazo hazina sheria kali zinazohusiana na masuala haya , Ulanguzi huu umesababisha Serikali kupoteza mapato makubwa , waingizaji wa programu hizi nao kuingia hasara pamoja na hasara za kiusalama kwa watu wanaopatiwa programu hizo .

  Mfano unaweza kupatia programu ya antivirus kwa ajili ya ulinzi wa komputa yako na vifaa vyake , unapounganisha komputa kwenye mtandao ili uweze kufanya updates kadhaa unaambiwa leseni ya antivirus hiyo sio yake labda imeshatumika au ni batili unatakiwa utumie leseni halali .

  Kitu kama hicho kikitokea antivirus hiyo inaweza kuacha kabisa kufanya updates na kuruhusu virus kuingia kwenye komputa yako , nyingine zitaendelea kukukumbusha kuhusu leseni unayotumia si yake au batili lakini itaendelea kukulinda kwa muda fulani tu kisha itaacha kufanya hivyo .

  Tofauti na vitu vingine vinavyouzwa kwenye maduka na sehemu zingine duniani programu zinazoendesha mashine kama komputa na vifaa vyake sio zako wewe unanunua leseni ya kukusaidia kutumia programu hiyo kwa muda fulani kisha unatakiwa kununua leseni nyingine .

  NJIA ZINAZOTUMIWA NA WAHALIFU

  1 - Kama umenunua leseni ya kompyuta moja ni kosa kutumia leseni hiyo kwenye kompyuta nyingine kosa hilo linaweza kukusababishia kifungo au faini kubwa kulingana na ulichofanya na bei za programu hizo na sheria za nchi husika au za kimataifa , unaponunua leseni ya kompyuta moja tumia kwenye kompyuta hiyo hiyo labda kama umenunua leseni ya komputa au kifaa zaidi ya kimoja na unaponunua leseni hiyo unatakiwa usome mkataba wako na mtengenezaji wa programu hiyo itaeleza kwa wazi aina ya leseni na jinsi unavyotakiwa kuitumia .

  Hii ya kuweka leseni moja ya programu kwa komputa nyingi mara nyingi inafanyika kwenye komputa ambazo hazijaunganishwa kwenye mtandao haswa za watu wanaofanya huduma za steshenali mijini wanawekewa antivirus sana , programu za kutengeneza maumbo na aina nyingine ya programu – hili ni kosa .

  Hata kama ulinunua programu ukamuuzia rafiki yako , jirani yako au jamaa yako yoyote leseni hiyo hiyo hili pia ni kosa kuna watu wengi sana wanaotumiana au kupeana programu kwa njia hizi kwa kufikiri ni halali .

  2 – Angalia sana unavyoshusha programu na leseni kwa njia ya mtandao , ni vizuri ukanunua programu hiyo kwenye mtandao na kampuni husika mfano kama ni windows nunua toka Microsoft , kama ni autocad nunua toka autodesk kama ni adobe Photoshop fuata tovuti ya Kampuni husika ingawa kuna Tovuti zinazouza Pia programu hizi angalia sana masuala ya bei na kama kweli wanaushirikiano wowote na kampuni kuu , Na zaidi tembelea maduka ya programu Mji wako wa karibu unaweza kupata kwa urahisi zaidi .
  La Mwisho ni kuangalia tovuti unazotembelea kudownload programu husika kuna tovuti kibao ambazo zinasambaza programu ambazo ni bandia au zimebadilishwa ili zionekane halali wakati sio kweli lakini ni kweli kwamba kuna programu ambazo ni za bure kabisa zinazotolewa kwa sababu maalumu .

  Mfano kumekuwa na watu wanaouza programu ambazo zinatolewa bure na kampuni zilizotengeneza programu hizo lakini wanauza bila maelezo ni vizuri ukawa na mazoea ya kutembelea tovuti za programu husika kujua uhalali wa programu hiyo .

  3 – Kuna kampuni zinazouza au kutoa baadhi ya programu zao kwa ajili ya masoko maalumu haswa ya wanafunzi na kwa bei ndogo kwa ajili ya makundi hayo lakini unaweza kukuta programu hizi zinauzwa kwa bei ghali kuliko yake halisi au zinazuzwa kwa maelezo tofauti mara nyingi angalia makubaliano ya leseni hiyo utaelezwa kila kitu

  4 – Watu wengi sana wanaonunua komputa ambazo zimeshawekwa programu haswa operating system za Microsoft windows , au programu za office kama Office 2003 mpaka 2010 au antivirus wanapoenda kuunganisha kwenye mtandao ndio wanagundua hili haswa wanapotakiwa kuupdate programu hizo au kuzisajili kwa njia ya mtandao , wengi wetu tumezoea kutumia programu zingine kuondoa maonyo tunayopewa kwa programu hii ni bandia unatakiwa kununua na mambo mengine kama hayo .


  MADHARA YA KUTUMIA/WEKA LESENI BANDIA

  1 - Unapofanya mambo hayo hapo juu niliyoyataja unahatarisha usalama wa komputa yako na programu zingine zilizokuwa ndani ya computer hiyo kwa kushambuliwa Na kupata aina nyingine ya matishio kwenye mtandao au yanayoletwa kwa njia ya kuhamisha .

  2 – Hautoweza kuisajili programu hiyo kwahiyo haitoweza kufanya kazi vizuri kama inavyotakiwa mfano mzuri ni programu za ulinzi kama antivirus , internet security na zingine zinazotumika kwa shuguli maalumu .

  3 – Unakosesha Serikali mapato yake kwa njia fulani na unasaidia kupunguza ajira za watu ambao wametumia muda mwingi kutengeneza programu hizo ili kukufanya wewe uweze kufanya kazi zako kwa urahisi zaidi .

  4 – Ni njia nyingine ya Wizi ( Uhalifu ) wewe unayetumia na aliyekuuzia akikamatwa anaweza kufunguliwa mashitaka akafungwa au kulipishwa faini kubwa .

  5 – Kama umenunua programu kutoka kwenye tovuti ambayo ni bandia inawezekana ukatoa taarifa kuhusu kadi yako ya benki , wahalifu wanaweza kutumia kadi hiyo kwa ajili ya uhalifu mwingine au kuhamisha hela toka kwenye kadi hiyo , uwe unaangalia taarifa kuhusu anuani ya tovuti hiyo kabla ya kuamua kufanyanao biashara .


  ONYO KWA WAFANYAKAZI

  Kampuni na mashirika mengi hayana miongozo kuhusu Matumizi ya programu haswa na kompyuta na vifaa vingine vya mawasiliano na hata kama zipo basi hawaweki miongozo inayohusu programu kwahiyo ni rahisi kukuta wafanyakazi wakichukuwa programu za nje kwenda nazo makazini na kupeana na wafanyakazi wengine au kuingiza kwenye kompyuta zao kwa ajili ya kazi , Ni vizuri kampuni na mashirika kuwa na miongozo na sheria zingine zinazohusu programu na matumizi yake kwa ajili ya ulinzi na usalama wa masuala yao huko mbeleni .

  ONYO KWA WAZAZI

  Watoto wenu na vijana wenu wengine wanapenda kupeana programu hizi kwa njia nyingi tu mnatakiwa muwe makini haswa na komputa zenu za nyumbani zenye taarifa na vitu vyenu vingine endapo mtoto akaja kuweka programu kama hizi ambazo zinaweza kumwezesha mhalifu kuingilia komputa yako na kuhamisha taarifa au kupandikiza programu zingine , kumbuka kuweka programu za kudhibiti matumizi ya komputa kwa watoto wadogo .

  Yona Fares Maro
  The ICT Pub
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hapo penye bluu mkuu ndipo penye msiba wa taifa.......utawezaje kugundua mara moja pale unaponunua?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mfano micrsoft office unaweza kuuziwa cd yake tofauti kama unahitaji ila inakuwa na version ambayo unahitaji kuifanyia activation wengi huwa wanatoa version hiyo na kukuwekea yakwao ambayo ni pirated kwa mteja kujua au bila kujua vile vile na antivirus ntaeleza uzuri kwenye mada ya kesho

  usiku mwema
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  SOMO KUHUSU PROGRAMU/SOFTWARE BANDIA

  MADHARA YA KUTUMIA/WEKA LESENI BANDIA
  Mashambuliz ya kwenye mtandao hayabagui uwe na pirate au uwe na umeweka program amabyo si pirated THREAT ni zile zile

  Hii unaweza kuchukua update kwa offline sio lazima kufanya online update kwa software . lakini hata ukifanya online labda kama unatumia ENTERPISE EDITION program lakini home program hata iwe MS office au MS XP au Kapersky sijawa kusikia kuna tu kashindwa kufanya updat sababu ni pirated.

  Serikali gani inakosa mapatao kutokana na pirated Windows XP Antivirus ??? Mapatao ya Billgates au Warusi hayatuhusu na zaidi ya yote uwezo wetu mdogo ndio maana hawawezi kufuatilia sana huku kwetu.

  Huo sio wizi ni watu wanaamua kushare haya mambo ya licence ndio WIZI. wewe ukiambiwa leo hii nguo uliyonunua dukani ina licence moja huruhusiwi kuigawa wala kumpa mtu wingine kuvaa si utakuwa wizi. XYZ kanunua Norton kihalali kaamua kutoa kopy kuwapa ndugu na jamaa iweje umuite mwizi?


  Hili ni kweli kabisa lakini tovuti nyingi zinazotoa au kushare pirated software na keys kama piratebay.org au demonoid.com hawauzi ni bure tu unahitaji bandwidth ya kudowload tu.


  Mkuu nadhani cha msisitizo nikuweka wazi kuwa hizi piraets software ni kwa watumiaji wa nyumbani home user zina umuhimu sana wawe watumiaji wawe makini msanii asimuuize antivirus/software kwa bei kubwa sana wakati software yenyewe ni pirated.

  Msisitizo mwingine kama una uwezo nenda kanunue halali na kama hauna uwezo usiogope sana hizi pirated software ni salama 80% tena
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Microsoft Genuine Advantage Program Information

  On This Page
  Program Overview
  Windows Genuine Advantage (WGA) for Windows Vista
  Windows Genuine Advantage for Windows XP
  Program Overview

  What is the Windows Genuine Advantage Program?
  Microsoft Genuine Advantage programs, including Windows Genuine Advantage, help you determine whether or not your copy of Windows is genuine. Genuine Windows software is published by Microsoft, properly licensed, and supported by Microsoft or an authorized partner, giving you full capabilities, access to all the latest updates, and confidence that you are getting the experience you expect. Microsoft continues to invest in education, engineering, and enforcement in order to more effectively combat software piracy. It’s part of Microsoft’s commitment to help protect its intellectual property and to help you avoid problems before they happen.

  Why you should care that your computer is running genuine Windows
  In today’s world, you rely on your computer to work for you and to run your business. You store thousands of photos, music collections, and important documents; you make purchases, enter personal information, and search the Web. Imagine what it would be like to lose all your favorite family photos, or have your financial data stolen as a result of malicious or unwanted software running on your computer. Market research firm IDC reported in a recent study (English only) that obtaining and using pirated software can pose a serious security threat to organizations and individuals. Often, counterfeit software is bundled with malicious and unwanted software that can lead to a corrupted system, a loss of data, and even identity theft. The risk of running counterfeit software is real. Windows is the operating system and the brain behind everything you do on your computer; you can help protect your data by installing only genuine Windows.

  How software piracy impacts local businesses and global economies
  Software piracy is an industry-wide problem that has significant impact on the global economy, and affects legitimate businesses that have to compete with those selling counterfeit software. The Business Software Alliance and market research firm IDC reported in The Global Software Piracy Study (English only) that software piracy contributed to nearly $40 billion in global losses. Consumers spend millions of dollars each year on counterfeit copies, financing scammers who threaten the integrity of the software industry and the security of home and business computers. Software piracy puts everyone at risk. Microsoft and its customers can work together to stop it.

  What Microsoft is doing to help protect you and the Windows ecosystem
  As an industry leader, Microsoft has an obligation to help level the playing field for its partners and to help the broader computing ecosystem by doing all it can to address software piracy. Microsoft continually invests in technologies and programs that make piracy harder, make it easier for you to recognize counterfeited software, and help you if you have been a victim of it. Microsoft’s anti-piracy efforts are organized under an umbrella initiative called the Microsoft Genuine Software Initiative, Learn more about Microsoft’s Genuine Software Initiative. The Windows Genuine Advantage (WGA) program provides technologies that help you determine whether your copy of Windows is genuine, including product activation and validation. Both help you ensure that your copy of Windows is genuine and properly licensed. You can find out if you’re running genuine by clicking Validate Windows on Genuine Microsoft Software. Microsoft values your privacy and does not use any information collected to contact you or identify you. Read the Windows Genuine Advantage Privacy Statement.

  What Microsoft is doing to help you get genuine
  If your copy of Windows is not genuine, Microsoft can help you to quickly fix the problem and get genuine. Customers can contact Microsoft Support or visit the Microsoft Genuine Advantage support page to resolve the problem. Microsoft also offers several options to help victims of counterfeit software obtain a legal copy of Windows, including a complimentary offer for victims who were deceived into buying high-quality counterfeit copies. Read the Frequently Asked Questions to learn more about genuine Windows offers.

  Top of page
  Windows Genuine Advantage (WGA) for Windows Vista

  Windows Vista has built in anti-piracy technology that enables Microsoft to combat piracy more effectively. This new technology is a part of the Windows Genuine Advantage program. It changes how Windows Vista activates, validates, and behaves when attempts are made to tamper with the activation or validation requirements of the operating system. This helps to make piracy harder and provides a better experience for customers running genuine Windows. Using genuine Windows Vista helps customers enjoy the full functionality of Windows while helping to avoid viruses, tampered files, and other malicious software often associated with counterfeit copies. Windows product activation and validation are the experiences customers see when using WGA.

  Windows Product Activation
  Activation is an anti-piracy technology designed to make sure that the proper product key is being properly used with the software license associated with it. All editions and distributions of Windows Vista, including those obtained through a volume license program, are required to complete activation within the first 30 days of using Windows Vista. Because activation is required, failure to activate will result in the system being placed in a reduced functionality mode. Learn more about reduced functionality mode by visiting the Frequently Asked Questions.

  Windows Validation
  Validation helps confirm that a copy of Windows Vista is activated and properly licensed. Users may be asked to validate their copy of Windows when they download content that is reserved for users of genuine Windows from the Microsoft Download Center. Validation can also occur as part of an update from Windows Update. In some instances, a computer that has previously passed validation may fail the validation process. This may happen because Microsoft constantly discovers new forms of piracy. As new forms of piracy are discovered, Microsoft updates the anti-piracy components to help disable the emerging threats and therefore, a copy of Windows that previously passed validation may fail a later validation check. Copies of Windows Vista that are unable to validate as genuine may need to activate and validate again in order to maintain full functionality.

  Designed to give you a great experience
  Microsoft is strengthening its commitment in the fight against software piracy by building new anti-piracy technology right in to Microsoft software products. As Microsoft leverages new technology, a key goal is to maintain a great experience for customers using genuine software. Overall, Microsoft would like customers to expect fairness, great service, and a positive experience in the implementation of our anti-piracy measures, and Microsoft has taken steps to make it easy and convenient for victims of counterfeit to get a genuine copy of Windows Vista.

  Top of page
  Windows Genuine Advantage for Windows XP

  The Windows Genuine Advantage program for Windows XP uses Windows product activation, validation, and notifications to verify that your copy of Windows is genuine. Using genuine Windows delivers better performance and lets you access all downloads in the Microsoft Download Center, while helping to protect you from the risks of counterfeit software. Learn about Microsoft Genuine Advantage programs.

  Activation is an anti-piracy technology designed to make sure that your copy of Windows XP is properly licensed. It works by verifying that the product key is valid and is only being used on the number of computers permitted by the software license. Activation uses a simple and fast process to protect your copy and ensure that you paid for the right thing.

  Validation is a quick process that allows you to find out if the product key you activated is counterfeit or has been misused. For example, you may have accidentally received a product key that was reported as lost or stolen by its original owner. Sometimes, during a repair or reinstall, an invalid product key is used if the original product key is not handy. Microsoft values your privacy and does not use information collected during the validation process to identify you or contact you.1

  Notifications helps Microsoft to fight software piracy and helps to you validate that the copy of Microsoft Windows XP that's installed on your computer is genuine and properly licensed. It reminds you that your copy of Windows XP did not pass validation and provides resources that help you to easily fix the problem online. Get more information about WGA Notifications.

  By confirming that your copy of Windows XP is genuine, you can take advantage of all the capabilities, support, and continuous improvements—as well as the peace of mind—that come with using genuine Windows.
  Genuine Microsoft Software
   
 6. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  @SHY,
  Acha kukatisha tamaa wabongo, kwa sent za kibongo utaweza vipi kununua kila software unayohitaji? hata hapa mjini wanunuzi wa software ni wale wale wasiojua kuzitumia ndo wanatishika na hizo habari kwamba ukitumia genuine itakulinda zaidi. Uliza wa-Chinese mpaka serikalini wanadunda nazo tuu.
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Jun 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hayo ni maoni yako na mimi nilitoa yangu mwanzo kwahiyo ni shauri ya mtu mwenyewe kuamua kuwajibika
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Copy and Paste @ Work - Shy as usual!
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tena hawa jamaa wangebadilisha jina na kujiita sharingbay


  Sweeden is one of the most developed countries yet kuna watu wakaona uuhimu wa kufanya sharing. Iweje mtu wa nchi tena kama Tanzania .uwe mwepesi kuona ubaya wa sharing.

  Kama site imo kwenye 100 popular site duniani unelewa nini?? hakuna threat kubwa kivile kama watu wanavyosema kwenye kutumia prirated.

  Kwa kazi ambazo chanzo chake sio tanzania nadhani twende kwa style ya copy left.
  Kwa tanzania badala ya kuongelea piracy ya software tushirikiane kutokomeza piracy ya kazi za wasanii wetu. kwa hilo tuko pamoja.


  .
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hao majamaa wa Pirate Bay wote wamehukumiwa mwaka mmoja jela na fine ya 30 million Krona so mfano si mzuri huo. Kutumia software au kazi yoyote yenye haki miliki bila license ni wizi, tusitake kuhalalisha.

  Kwa bongo software ni unaffordable kwa majority ya watu so tuhamie Open Source au Freeware, watu wanakimbilia kupirate wakati alternative za bure zipo.Pia watengeneza software waje na special pricing for third world countries.

  Risk zake ni kwa wale ambao ujuzi wao mdogo wa kompyuta, kama unajua unalofanya hakuna cha risk.
   
 11. kidadari

  kidadari JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2018 at 2:48 PM
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 2,348
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  RIP Yona
   
Loading...