Somo kuhusu Mafumbo

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,271
29,879
Mafumbo ni aina ya tungo fupi ambazo huwa na maelezo yanayoishia kwa swali; kisha anayejibu huhitajika kufikiria ili kutambua jibu. Kinyume na vitendawili, majibu ya mafumbo huwa na maelezo marefu.


Sifa za Mafumbo

1. Mafumbo huwa na sehemu mbili – sehemu ya swali na sehemu ya jibu.

2. Huwa baina ya watu wawili – anayefumba na anayefumbua (wanaofumbua)

3. Mafumbo yaliendelezwa wakati maalum.

4. Jibu la fumbo si maalum kwani kinachohitajika ni mantiki katika jibu.

Umuhimu wa Mafumbo

1. Hukuza uwezo wa kufikiri ili kupata jibu.

2. Huimarisha umoja katika jamii kwani watu huja pamoja wanapofumbiana mafumbo.

3. Mafumbo huhifadhi utamaduni –
hupokezanwa kutoka kizazi hadi kizazi

4. Mafumbo hutumika kama burudani

5. Hutumika kupitisha muda.

Mifano ya mafumbo

1. Fumbo: Ajali mbaya ilitokea kati ya mpaka wa Kenya na Tanzania. Je, majeruhi walizikwa wapi?

Jibu: ....................................

2. Fumbo: Upepo ulikuwa unavuma sana kutoka mashariki hadi magharibi.

Nilikuwa nikiliendesha gari la moshi linalotumia umeme kutoka Burundi hadi Malawi.

Je, moshi ulielekea upande gani?

Jibu: ,,..,.,.........................

3. Fumbo: Mimi na ndugu yangu tulinunua fahali mmoja kutoka sokoni.

Baada ya mwaka mmoja alijifungua ndama wawili.

Je kila mtu alipata wangapi?

Jibu: .,......................

4. Fumbo: Juma ana vitu vitatu; mbwa, kuku na mchele anaotaka kuvusha mto.

Mbwa hula kuku na kuku hula mchele.

Kulingana na sheria za kuvuka daraja lile, hauwezi kuvuka ukiwa na zaidi ya vitu viwili.

Je juma atatumia njia gani kuvuka?..........................

Uwe Na Jumapili Njema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom