Somo hili linawahusu wanaume please pitia hapa upate elimu

Llio 002

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,615
2,031
Nawaandikieni nyie waume, maana Mungu amewapa hekima na busara ya kuwa kichwa na kutawala yale yaliyo chini yenu.

Unafahamu kwamba vitu unavyovifanya wakati mwanamke wako anapokua mjamzito vina-influence afya ya mama na mtoto aliye tumboni?

Brothers nisikilizeni hua nashangaa sana mnavyokua mnawasumbua wake zenu wakiwa wajawazito na kushindwa kuendana na mabadiliko wanayopitia.

Ni miezi tisa tu ile wala sio ndio milele watakua vile. Mimba hainunuliwi sokoni, wala sio software kwamba utaipakua kwenye internet. Ile ni mbegu iliyopandwa na wewe. Na lazima awepo mtu wa kuibeba ikue vema na kuweza kuzaa kile kilicho bora. Na wanawake wamepewa uwezo huo wa kuibeba hiyo mbegu

Mimba ni maandalizi ya kumkaribisha member mpya katika familia. Ujauzito ni adventure safari ..iliyojaa furaha, faraja, na kila aina ya disappointment. Wanawake wanatofautiana katika mabadiliko ya mwili na tabia wawapo wajawazito.

■ Kuna kipindi atakuwa ni mlalamikaji sana

■ Kuna kipindi atakuwa akikuomba vitu ambavyo ni vya ajabu mfano chai iliyowekwa nazi au supu ya miguu ya mbuzi.

■ Kuna kipindi atakuwa mvivu kukupikia chakula.

■ Kuna kipindi atatamani umkande miguu na kumbembeleza kama mtoto mdogo.

Tafadhali sana brother msikilize wala usimpotezee...kubeba mtoto sio kazi ndogo eti. Ninauhakika ungehamishiwa ubebe wewe hata kwa siku moja ungeona jinsi ilivyo tabu.

Tafadhali sana, vumilia hiyo hali..hata hivyo mbona ni wakati mzuri sana...hakuna kipindi kizuri kama mwanamke akiwa mjamzito..kadiri utakavyomtunza ndivyo atakavyozidi kuonekana bomba na wa kuvutia

ZINGATIA HAYA.

1. Siku zote observe miguu ya mkeo wakati akiwa mjamzito, mara nyingi miguu huvimba. Tafadhali chukua maji na kitambaa mkande miguu mara kwa mara, ni kitu ambacho wanawake hukipenda sana pindi wawapo wajawazito.

2. Muuluze mara kwa mara anajisikiaje na mtoto tumboni yukoje. Yeye ndie amembeba anafahamu movement za mtoto tumboni.

3. Mueleze ni kwa jinsi gani alivyo mzuri kipindi akiwa na ujauzito..mfano "Honeylove ukiwa na mimba unaonekana mzuri kweli ntakua nakupa mimba kila siku" au "Hivi ni mwanangu ndio anakufanya uonekane mzuri hivi"..kwa vitu vidogo kama hivi mkeo atajisikia faraja sana na atajivunia kukubebea mtoto wako tumboni mwake.

4. Usikasirike pale anapokuamsha usiku wa manane na kumsaidia anavojisikia vibaya. Unatakiwa nawe ujali maumivu yake. Hatakiwi kuugulia maumivu peke yake...ni mtoto wako pia mnatakiwa muumie pamoja.

5. Hakuna sheria inayozuia tendo la ndoa wakati wa ujauzito. Kiufupi ndio kipind ambacho sex ni good kama ukiifanya kwa utaratibu mzuri.

6. Usijisikie fedheha kutoka out na mkeo mjamzito..mpeleke maeneo mazuri ambayo ulikuwa unampeleka kipindi unamfukuzia..she will love you to death...

Muda mwingine nashangaa mambo wanayoyawaza wanaume pindi wake zao wakiwa wajawazito. Kubeba mtoto kwa kpindi cha miezi tisa sio kazi ndogo.

Wanaume wote tuwe karibu na wake zetu pindi wakiwa wajawazito...ni kipindi ambacho wanatuhitaji sanaa.

Heko kubwa kwa wanaume wote ambao wanasimama kidete kuhakikisha mwana member mpya wa familia aliyepo tumboni anahudumiwa vizuri kupitia aliyembeba. Mungu awabariki sana.

“A baby will make love stronger, days shorter, nights longer, bankroll smaller, home happier, clothes shabbier, the past forgotten and the future worth living for.”
 
Kwa hiyo unataka kuniambia mwanamke akipata mimba anaanza kupungukiwa akili?

Maana tabia zote ulizotaja ni za mtu aliyepungukiwa akili
Watakujibu wenyewe mimi nawaheshimu sana wanawake siwezi kuwatukana hivyo hao ni mama zetu pamoja na dada zetu tunatakiwa tuwaheshimu sana na kuwathamini
 
Watu wengi huwa hawajui hata aliyeleta maada najua hajui

Pindi mwanamke anapokua mjamzito ni marufuku kumdekeza kwa maana ndo hapo tabia nyingi alizozificha huonekana lzm usimame kiume umuonye na usimuache kwani ukimwacha tabia utaichixhea mpaka hata kwa watoto

Mfano mwanamke anakuwa mjamzito anampenda mwanaume furani eti asipomwona hajisikii vizuri ukiona hivyo jua huyu anatabia ya uzinzi hata makofi anastahili kabisa
 
Kibongo mwanamke ukifanya hivyo ataitumia fursa hiyo vibaya, unafika getini mtu anakuagiza kitu kinacho patikana kilometa 5 sasa mimba gani hiyo. Mchana alikuwa wapi kukuagiza
 
Nawaandikieni nyie waume, maana Mungu amewapa hekima na busara ya kuwa kichwa na kutawala yale yaliyo chini yenu.

Unafahamu kwamba vitu unavyovifanya wakati mwanamke wako anapokua mjamzito vina-influence afya ya mama na mtoto aliye tumboni?

Brothers nisikilizeni hua nashangaa sana mnavyokua mnawasumbua wake zenu wakiwa wajawazito na kushindwa kuendana na mabadiliko wanayopitia.

Ni miezi tisa tu ile wala sio ndio milele watakua vile. Mimba hainunuliwi sokoni, wala sio software kwamba utaipakua kwenye internet. Ile ni mbegu iliyopandwa na wewe. Na lazima awepo mtu wa kuibeba ikue vema na kuweza kuzaa kile kilicho bora. Na wanawake wamepewa uwezo huo wa kuibeba hiyo mbegu

Mimba ni maandalizi ya kumkaribisha member mpya katika familia. Ujauzito ni adventure safari ..iliyojaa furaha, faraja, na kila aina ya disappointment. Wanawake wanatofautiana katika mabadiliko ya mwili na tabia wawapo wajawazito.

■ Kuna kipindi atakuwa ni mlalamikaji sana

■ Kuna kipindi atakuwa akikuomba vitu ambavyo ni vya ajabu mfano chai iliyowekwa nazi au supu ya miguu ya mbuzi.

■ Kuna kipindi atakuwa mvivu kukupikia chakula.

■ Kuna kipindi atatamani umkande miguu na kumbembeleza kama mtoto mdogo.

Tafadhali sana brother msikilize wala usimpotezee...kubeba mtoto sio kazi ndogo eti. Ninauhakika ungehamishiwa ubebe wewe hata kwa siku moja ungeona jinsi ilivyo tabu.

Tafadhali sana, vumilia hiyo hali..hata hivyo mbona ni wakati mzuri sana...hakuna kipindi kizuri kama mwanamke akiwa mjamzito..kadiri utakavyomtunza ndivyo atakavyozidi kuonekana bomba na wa kuvutia

ZINGATIA HAYA.

1. Siku zote observe miguu ya mkeo wakati akiwa mjamzito, mara nyingi miguu huvimba. Tafadhali chukua maji na kitambaa mkande miguu mara kwa mara, ni kitu ambacho wanawake hukipenda sana pindi wawapo wajawazito.

2. Muuluze mara kwa mara anajisikiaje na mtoto tumboni yukoje. Yeye ndie amembeba anafahamu movement za mtoto tumboni.

3. Mueleze ni kwa jinsi gani alivyo mzuri kipindi akiwa na ujauzito..mfano "Honeylove ukiwa na mimba unaonekana mzuri kweli ntakua nakupa mimba kila siku" au "Hivi ni mwanangu ndio anakufanya uonekane mzuri hivi"..kwa vitu vidogo kama hivi mkeo atajisikia faraja sana na atajivunia kukubebea mtoto wako tumboni mwake.

4. Usikasirike pale anapokuamsha usiku wa manane na kumsaidia anavojisikia vibaya. Unatakiwa nawe ujali maumivu yake. Hatakiwi kuugulia maumivu peke yake...ni mtoto wako pia mnatakiwa muumie pamoja.

5. Hakuna sheria inayozuia tendo la ndoa wakati wa ujauzito. Kiufupi ndio kipind ambacho sex ni good kama ukiifanya kwa utaratibu mzuri.

6. Usijisikie fedheha kutoka out na mkeo mjamzito..mpeleke maeneo mazuri ambayo ulikuwa unampeleka kipindi unamfukuzia..she will love you to death...

Muda mwingine nashangaa mambo wanayoyawaza wanaume pindi wake zao wakiwa wajawazito. Kubeba mtoto kwa kpindi cha miezi tisa sio kazi ndogo.

Wanaume wote tuwe karibu na wake zetu pindi wakiwa wajawazito...ni kipindi ambacho wanatuhitaji sanaa.

Heko kubwa kwa wanaume wote ambao wanasimama kidete kuhakikisha mwana member mpya wa familia aliyepo tumboni anahudumiwa vizuri kupitia aliyembeba. Mungu awabariki sana.

“A baby will make love stronger, days shorter, nights longer, bankroll smaller, home happier, clothes shabbier, the past forgotten and the future worth living for.”

ngoja nijifunze kuqoutes uzi mzima
yaani namanisha nakazia.
 
Wanaume wakuwafanya hayo uliyoyaandika walisepaga na Jesus
 
Back
Top Bottom