Huyu dada hakukutafuta ila wewe ndio ulimtafuta kwa kumpa ofa ya chakula na bado ukampa namba ya simu. Nadhani kwa kumpa namba ya simu ulitarajia kufanya mawasiliano nae. Mawasiliano ni sehemu ya kufahamiana na wakati mwingine kunasaidia kujifunza kutoka kwa wengine. Kitendo cha wewe kujitangaza kuwa huna mpango nae na kuwa ulimsaidia kwa shida zake ni kutaka sifa. Unapomsaidia mhitaji kwa nia safi Mungu anakuhesabia ukarimu na utapata thawabu. Kumbuka hata maandiko yanatuonya kutokufanya wema ili usifiwe na watu. Baada ya kufanya ulichofanya wewe ungekaa kimya na kama kuna jambo hukulitarajia kwake ulikuwa na nafasi ya kumweleza hivyo na sio jf.