Some women's approach to men is amazing

SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,368
1,131
Hivi karibuni nilisafiri kutoka Dar kwenda mikoa ya kusini. Ndani ya gari nikakuta nimekaa siti moja na mdada mmoja mdogo, umri waweza kuwa kati ya miaka 16-18. Kawaida yangu huwa siyo mzungumzaji sana, labda mpaka mtu mwingine aanzishe mada. Kwa mvao na mwonekano wake alikuwa amependeza vizuri tuu, lakini ikaonekana hakuwa vizuri kiuchumi. Alikuwa ananunua vitu rahisi sana, hata maji alikuwa anauliza kama kuna ya 300.

Tukafika sehemu tukashuka kwa mapumziko ya dk kumi kununua mahitaji na kuchimba dawa. Nikafanya manunuzi ya chakula na vinywaji mara mbili ili nimgawie na yeye. Akafurahi sana na tukajaribu kufahamiana. Nikataka kujua anafanya nini. Akaniambia kuwa aliacha shule akiwa form 2 mwaka jana kwa sababu za kiuchumi, ndo akawa ameenda Dar kutafuta kazi za kuuza duka.

Nikampa pole kwa maswahibu yaliyomkuta. Tulivyokaribia kushuka akaniuliza kuwa nafanya kazi wapi? nikamweleza, akaniomba namba. Tukaachana huku akinishukuru sana kwa msaada wa chakula njiani. Ikawa kila siku usiku ananibip ili nimpigie. kimsingi hakuna hata mada serious za kuzungumza, basi tu kujuliana hali. Baadaye akaanza kunitumia msg za kuniita mpenzi, baby, etc. Akaanza kuniambia ametokea kunipenda, na anataka nimtumie hela na vitu vingine kibao. Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!
 
HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,558
.... Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!

Hapana ndugu yangu, kumsaidia mtu si gear ya kuwa wapenzi kama moyo wako si wa tamaa wala nia mbaya. Kosa nililoliona haraka haraka ni kutoa namba ya simu kwa huyo dada mara baada ya kumnunulia chakula. Kwa kawaida, hata kama nia yako ya kumsaidia ni njema, kitendo cha kutoa namba ya simu ni kuruhusu MAWASILIANO zaidi baada ya kuachana hapo. Na mimi sishangai kabisa yeye kuendelea kukutafuta maana ndiyo kazi halisi ya simu!

Pengine kwa elimu yake na ufahamu wake labda pia na kwa kusukumwa na umaskini, amejikuta akilazimika kukutafuta ili pengine uweze kuwa wake na kumsaidia the same way kama ulivyomsaidia kwenye basi!!!

Najifunza kitu, sisi wazazi ni vyema tukajitahidi kuwalea na kuwasomesha watoto wetu vizuri ili wasije kuchapwa na maisha na kujikuta wakijiingiza kwenye mitego ya namna hii.
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
1,156
Wala usishangae. Mbona tunaona ni kawaida iwapo kama ingekuwa imetokea kwa upande wa pili? Kama wewe ndiye ungeomba namba ya binti na baadaye kuanza kumpigia ukimtaka muwe wapenzi... mbona hiyo tunaona kuwa ni kawaida, kwa nini tushangae inapokuwa vice versa?
 
SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,368
1,131
Nimewasoma wote, ni kweli mnayosema. Ila mimi naona hata kama ni kujikwamua kimaisha amekuja kwa kasi sana. Kwa tamaduni zetu za kiafrika inakuwa tabu sana mwanamke kumsumbua mwanaume kihivyo, ila kwa siku hizi mambo yamebadilika sana.
 
SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,368
1,131
Kiukweli kuna weekend alinisumbua sana akitaka kuja town, sasa nauli 3,000 nimtumie alafu aje town nimgharimie mambo mengine yote, mbaya zaidi sina feelings za kuwa naye kimapenzi, dhamiri yangu hainitumi kwa sababu nitaishiaa kumchapa na kumwacha na pains.
 
UZEE MVI

JF-Expert Member
Feb 6, 2011
231
52
Nimewasoma wote, ni kweli mnayosema. Ila mimi naona hata kama ni kujikwamua kimaisha amekuja kwa kasi sana. Kwa tamaduni zetu za kiafrika inakuwa tabu sana mwanamke kumsumbua mwanaume kihivyo, ila kwa siku hizi mambo yamebadilika sana.

Hamna cha kushangaa. ndipo tulipofikia kimsingi. wewe unasema kwa tamaduni za kiafrika? I ma not sur of your age. lakini miaka michache iliyopita, haikuwa utamaduni wa mwafrika mtoto wa kike au mwanamke kuvaa suluari, haikuwa utamaduni wa muafrika kwa msichana kuongea na mvulana hadharani, hata wachumba tulikuwa tunatafutiwa na wazazi wetu, haikuwa utamaduni wa muafrika kwa msichana na mvulana kukaa benchi moja kanisani. kule shuleni walimu walifanya kazi ya ziada kulazimisha wavulana na wasichana kushare viti na madeski mashuleni. so hilo halishangazi hata kidogo.
 
Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
721
Hivi karibuni nilisafiri kutoka Dar kwenda mikoa ya kusini. Ndani ya gari nikakuta nimekaa siti moja na mdada mmoja mdogo, umri waweza kuwa kati ya miaka 16-18. Kawaida yangu huwa siyo mzungumzaji sana, labda mpaka mtu mwingine aanzishe mada. Kwa mvao na mwonekano wake alikuwa amependeza vizuri tuu, lakini ikaonekana hakuwa vizuri kiuchumi. Alikuwa ananunua vitu rahisi sana, hata maji alikuwa anauliza kama kuna ya 300.

Tukafika sehemu tukashuka kwa mapumziko ya dk kumi kununua mahitaji na kuchimba dawa. Nikafanya manunuzi ya chakula na vinywaji mara mbili ili nimgawie na yeye. Akafurahi sana na tukajaribu kufahamiana. Nikataka kujua anafanya nini. Akaniambia kuwa aliacha shule akiwa form 2 mwaka jana kwa sababu za kiuchumi, ndo akawa ameenda Dar kutafuta kazi za kuuza duka.

Nikampa pole kwa maswahibu yaliyomkuta. Tulivyokaribia kushuka akaniuliza kuwa nafanya kazi wapi? nikamweleza, akaniomba namba. Tukaachana huku akinishukuru sana kwa msaada wa chakula njiani. Ikawa kila siku usiku ananibip ili nimpigie. kimsingi hakuna hata mada serious za kuzungumza, basi tu kujuliana hali. Baadaye akaanza kunitumia msg za kuniita mpenzi, baby, etc. Akaanza kuniambia ametokea kunipenda, na anataka nimtumie hela na vitu vingine kibao. Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!

Huo ni mwanzo wa kuchuna buzi kama hujui.
MAPENZI GANI TENA HAYO!....CHEZEYA WACHUNAJI
 
SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,837
Hebu shangaa na wewe bro ..yaani utoe namba ya simu mwenyewe..halaf uanze kupigiwa simu malalamiko kibao hadi MMU..aaarghhh...This is not fair bwana..Ulitakiwa uwe nunda in the first place..duh!!

....Kosa nililoliona haraka haraka ni kutoa namba ya simu kwa huyo dada mara baada ya kumnunulia chakula. Kwa kawaida, hata kama nia yako ya kumsaidia ni njema, kitendo cha kutoa namba ya simu ni kuruhusu MAWASILIANO zaidi baada ya kuachana hapo. Na mimi sishangai kabisa yeye kuendelea kukutafuta maana ndiyo kazi halisi ya simu!.....
 
Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,854
1,128
Hivi karibuni nilisafiri
kutoka Dar kwenda mikoa ya kusini. Ndani ya gari nikakuta nimekaa siti
moja na mdada mmoja mdogo, umri waweza kuwa kati ya miaka 16-18. Kawaida
yangu huwa siyo mzungumzaji sana, labda mpaka mtu mwingine aanzishe
mada. Kwa mvao na mwonekano wake alikuwa amependeza vizuri tuu, lakini
ikaonekana hakuwa vizuri kiuchumi. Alikuwa ananunua vitu rahisi sana,
hata maji alikuwa anauliza kama kuna ya 300.

Tukafika sehemu tukashuka kwa mapumziko ya dk kumi kununua mahitaji
na kuchimba dawa. Nikafanya manunuzi ya chakula na vinywaji mara mbili
ili nimgawie na yeye. Akafurahi sana na tukajaribu kufahamiana. Nikataka
kujua anafanya nini. Akaniambia kuwa aliacha shule akiwa form 2 mwaka
jana kwa sababu za kiuchumi, ndo akawa ameenda Dar kutafuta kazi za
kuuza duka.

Nikampa pole kwa maswahibu yaliyomkuta. Tulivyokaribia kushuka
akaniuliza kuwa nafanya kazi wapi? nikamweleza, akaniomba namba.
Tukaachana huku akinishukuru sana kwa msaada wa chakula njiani. Ikawa
kila siku usiku ananibip ili nimpigie. kimsingi hakuna hata mada serious
za kuzungumza, basi tu kujuliana hali. Baadaye akaanza kunitumia msg za
kuniita mpenzi, baby, etc. Akaanza kuniambia ametokea kunipenda, na
anataka nimtumie hela na vitu vingine kibao. Jamani, hivi mtu
akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!

Hiyo ndo kusini babu! tuulize sisi!
 
HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,558
Hebu shangaa na wewe bro ..yaani utoe namba ya simu mwenyewe..halaf uanze kupigiwa simu malalamiko kibao hadi MMU..aaarghhh...This is not fair bwana..Ulitakiwa uwe nunda in the first place..duh!!

Halafu namba yenyewe ya simu ameitoa kwa kitoto cha miaka 16-18, imagine! Huyo si mtoto kabisa?! Alitegemea kungea naye nini mtoto kama huyu?
Labda si uzee umeshika kasi tunashindwa kwenda na kasi ya sayansi na teknolojia!!!!
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,611
7,785
.. Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!
Kuna ubaya gani "kumpenda" mtu anayekusaidia katika matatizo? Labda kama issue ni suala la umri.
 
SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,837
Huenda mkuu...manake kuna threads zingine za vijana sizielewagi kabisa hapa....
Mtu anauliza like 'nimempa binti namba yangu ya simu tatizo ananipigia hadi usiku msaada please'....cmon!!
Hili nalo la kuuliza..kweli tunahitaji Katiba mpya hapa MMU!!

Halafu namba yenyewe ya simu ameitoa kwa kitoto cha miaka 16-18, imagine! Huyo si mtoto kabisa?! Alitegemea kungea naye nini mtoto kama huyu?
Labda si uzee umeshika kasi tunashindwa kwenda na kasi ya sayansi na teknolojia!!!!
 
Mahmetkid

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
733
433
Kumsaidia siyo gear ya kumpata kimapenzi,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bejajunior

Senior Member
Sep 19, 2011
192
49
Acha kujifanya innocent wakati unatona number ulijua fika kwamba whats next..na matokeo ndio hayo mengine tunajitakia wenyewe cmoon!
 
UFASHE MLIBHONA

Senior Member
Nov 28, 2012
177
51
ukweli ni kwamba hivyo ndivyo mapenzi yanavyoanza, infact wengine huendelea hadi kufikia kufunga pingu za maisha.. endelea kuwasiliana naye . anaonekana bado mbichi huyo
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,163
50,548
Ni njaa tu ndo inayomsumbua wala sio kwamba we mzuri sana hadi anahitaji kuwa na wewe.

Umejuaje kama jamaa sio hendisamu? Unataka kuniambia girls wanawatokea ma-handsome tu? Au umesahau lile tangazo la 3 types of men lilikuwa linarushwa sana kiss FM...1.Handsome 2.Intelligent 3.Full loaded
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom