Some lemonade for you madame!

Some lemonade for you madame!

Mmha hii story inakoelekea presha tupu. Thank you money penny saa tatu si mbali. Hope george atapona.
 
Safaree akawazaaaaa wee na kuwazua akaona Zubeda anaweza ku fit kwenye ile mishe anayoiendesa stan na kama atajaribu kuongea na Don Lucifer akakubali, itakuwa bonge la movie maana Zubeda kwa kurubuni waume za watu ni nambari one, akawa anajiuliza atamfanyeje Adrienne mbona mwaminifu ivo kwa mumewake, anaanza kujiskia guilty kitendo cha kumuweka happy pale kumuharibu Adrienne lakini it’s too late atamtoaje pale? Mara simu ikaingia ya Peteroo, boss nataka kuja kukuona, akamwelekeza alipo Peteroo akaenda. Safaree anahitaji gawiwo lake Peteroo hana, Safaree akamwambia umekuja kunitania au? Akamwambia kila kitu kilienda sawa, akamwonyesha picha za kwenye simu lakini zile za video asubuhi naamka siioni camera huenda Doreen aliondoka nazo sasa nafanyaje? Safaree akamwangalia akasema huenda kweli maana nimeshaonyeshwa picha za kwenye simu sidhani kama anadanganya, akamwambia naskia Doreen anaenda bondeni, kuna kazi moja nataka kukupa ya nyumbani kwa Carrie iyo ukiishindwa basi tena me na wewe tunaagana, Peteroo akasema sawa boss amna neno, Safaree akamwambia baada ya wiki 1 kuisha nitakwambia uende Bondeni ukaifanye kwa sasa kata mawasiliano na Doreen hata akikupigia achana nae, Yule Carrie ninataka kumfanyia surprise maana alijidai kimbelembele anakuja na mapolisi kunifunga.



Adrienne nae yupo buzy na kazi, ofisini mara Jeff anakuja kumchungulia anamtania, mara anamtext kwenye simu jana usiku ulikuwa amazing balaa, na leo tena au sio mama twins!? Adrienne hakumjibu akawa akisoma anacheka tu anaendelea na kazi, lunch time Jeff huyoo, nataka kukutoa Lunch, Adrienne akamwambia we Jeff embu niache mbona unakuwa kama mtoto sasa haya mambo yakiendelea tutagundulika utaniletea balaa ofisini sasa haujui kuwa nimeoa, haya mambo tunafanya nje huko sio hapa ndani alafu mimi leo usiku nsafiri nachukua likizo ya wiki 2, naenda Afrika kusini kwahiyo haitawezekana kuonana tena. Jeff kusikia akachoka, eh unaenda na nani? Akamwambia naenda na rafiki yangu watoto wanabaki kwa mama mkwe wa rafiki yangu, Jeff akasema asee na mimi lazima nije weekend moja japo nikupooze si unajua mumeo akija ndio yale yale ya baba jeni bai bai sikuoni tena. Adrienne akawa anacheka tu haya hamna neno tutazidi kuwasiliana whatsapp! Jeff huyoo akasepa zake, Adrienne akaanza kusema eh michepuko mingine classy hata bondeni inagaramia kuja kula papuchi! Du! Kazi ipo akaendelea na kazi hata lunch hakwenda ili atoke mapema aende kujiandaa nasafari.



Doreen nae akatoka mapema akarudi kujiandaa na kuwaangalia watoto na kuwapokea watoto wa Adrienne, akamaliza kila kitu akawa anawasubiri akina Adrienne, baada ya dk 20 akaja Adrienne na team yake, Doreen anashangaa dada wa kazi kama huyo kamtoa wapi? Kha! Shepu kama nyumba ya sanaa?! Akawa anakula tu kwa macho anajisemea moyoni Shawn akija atakutana na balaa kwake sio kwa chura ile! Wakaonyeshwa pa kulala, wakawaaga watoto na maagizo kwa maids na mama mkwe wa Doreen haoo wakapelekwa na body guards wa Lucifer airport. Kufika ndani ya pipa wakaa seat karibu moja sema ndio zile business class ambazo hazibanani kama za kwetu huku economy, kwahiyo wakitaka kuongea inabidi mmoja azunguke, wakaanza kuongea jinsi gani hii vacation imewasevu maana sio kwa malezi yale na upweke ule!

Wakafika bondeni salama wakapokelewa na Carrie, eh Carrie kapungua maana mara ya mwisho alikuwa bongenyanya sijui ndio uzazi lakini sasa hivi kawa potabo acha! Yani kawa mzuri amependeza huenda George matunzo mazuri!



Wakakaribishwa Doreen akasema me nataka kulala na Adrienne maana mambo ya kuwa mpweke hata siwezi, au hauna chumba kikubwa zaidi tulale watatu na Chanel maana dah tuna mengi ya kuongea. Carrie aka arrange chumba kikubwa akawaweka marafiki zake wote 3 walale hapo, wakawa wanatia stori hapo weee utadhani hawajatua le oleo huko bondeni, mume wa Carrie akaja akawasalimia akawaambia namwiba mke wangu usiku umeshaenda mtaongea kesho, wenzake wakamuaga bye Carrie have fun si twalala, lakini hawakulala, Chanel anataka umbea wa Tz, Doreen na Adrienne wanataka umbea wa Chanel, wakaishia kulala saa 8 usiku.



Huko Russia, Shawn akapewa mchongo kwamba KAKARACHA ana kikao cha kugawa mizinga kwahiyo yeye kwakua ana sura ya kirusi kabisa anatakiwa aende akapewa na jina feki la mtu ambae alitakiwa kuwe kwenye kikao lakini walimkamata wakamfunga, wakatengeneza sura kama ya huyo mtu wakamvisha miwani kumbe miwani ina kideo na kila kitu, Shawn akiwa anasikiliza na kuangalia na wao huku nyuma ya pazia wanaona kila kitu. Shawn roho inamdunda anahisi yatamkuta ya kimaro akawa anaomba Mungu. Kufika anaambiw aweka finger prints zako tutajua kama ni wewe unahitajika au la,a akweka finger prints inakubali kumbe waliitengeneza finger print feki ya muhusika! Wakiwa kwenye kikao secretary akawakaribisha akajitambulisha zake, akakaribishwa kubwa la maadui

KAKARACHA: anaongea kirusi ila me naandika kibongo bongo! Akawakaribisha akaendelea na mada, tuna mpango wa kufanya hiki na kile kwa mwaka huu 2012, wamarekani wameshapatwa na mambo yao mwaka jana ya septemba 11 ila sisi hayo hayatuhusu, tunachotaka ni connection kubwa duniani kote ni u control mimi mpaka sasa sijaelewa connection ya Afrika Mashariki anayo nani, akaulizwa muhusika akasimama, Shawn anamwangalia kwa makini na wale wenzake nyuma ya pazia wanaona maajabu, mfanya biashara maarufu Afrika Mashariki ndio gaidi anaeharibu watoto wa watu, wakina Lucifer wakawa wana rekodi, Yule jamaa akaambiwa wataje watu wako, akawataja wote akafika wa Tanzania akataja Kimaro, Safaree, Zubeda, Happy, Peteroo! Lucifer yupo tobaa! KAKARACHA akauliza Kimaro kumbe ni wa kwetu, nimemuua juzi hapa alikuja amevalishwa waya wa ma FBI akauawa na huyu mpenzi wangu, akatokeza Yule dada, ni mwafrica mwembamba, huyu namwita Sungura! Ni karembo kananikumbusha Africa, kametokea Tanzania, akina Lucifer wanasema tobaa, wanashika vichwa! Huyu ni jembe langu anavyopenya Afrika Mashariki hana mpinzani mpaka sasa. Jamaa akaendelea kuwataja wa Kenya na Uganda na Rwanda na Burundi, wengine ma boss zake Lucifer yani mvurugano hatarious! Lucifer akajiambia kweli mtandao wa uhalifu hautaisha! Hadi ma boss wangu sasa nitashtaki kwa nani? Nashukuru niliemwachia urithi wa familia yangu hayupo humu, maana ningezimia.

Wakapanga wee mambo yao kila mtu akapewa jukumu lake kama mwanachama na nini cha kufanya na akiwa na swali wapi pa kuuliza na pesa kiasi gani wanatakiwa walete! Baadae kikao kikaahirishwa kitafanyika tena baada ya miezi miwili New York City! Shawn akatoka zake salama akarudi mpaka kazini kwake wakampongeza; mwenyewe anapumua anajua maji ya shingo yameisha hakujua kuwa mbele kuna bahari inamngojea! Wakwa wanapanga mikakati ya kuwafunga hao watz lakini lazima wawe na evidence wakaendelea kuumiza kichwa!



Kumekucha na wewe, warembo wakaamkia mezani baada ya kujipodoa asubuhi ile, eh chineke, Chanel ananjaa utadhani anaishi Sudani!

Chai ikaisha wakaingia sebuleni kupiga umbea, enhe niambieni wabongo manendeleaje na upweke wa kuchwa na waume zenu huku anacheka, wenzake wakamwambia tumeona jana vitu vyako, mume kaja kukuiba akaondoka na wewe! Tunakutamania, Carrie akapanda bichwa hamna bwana kawaida tu! Wakamsifia pale nyumba yake nzuuri na kuuubwa, baadae wakapanga baada ya maongezi wakaongee na Pastor kanisani kuhusu sadaka ya shukrani na kuzunguka mjini ila Chanel atakaa kwenye gari muda mwingi maana kutembea kwake sio sana.

Doreen akasema kwakweli tukamshukuru tu Mungu maana maisha ninayoishi ni ya aibu, akaanza kusema affair yake na Peteroo na jinsi alivyomrekodi Mungu saidia ile camera ikaanguka wakati anatoka akaiokota, akaanza kuwaonyesha ideo wenzake wakachoka, kweli sadaka ya shukrani imekuja wakati sahihi, enhe na wewe Adrienne tuambie, akasema me namshukuru Mungu kwa yote lakini kibaya ni kama Doreen kuna bwana hana ndoa nzuri ndio nipo nae nikiskia hamu nampigia, anaitwa Jeff king’ang’anizi nahisi ataniharibia ndoa jana nilikuwa nae Hyatt Regency hotel kidogo tubambwe na shemeji yangu Safaree! Nikazuga pale lakini nimemsikia anasema anataka kuja ila simwamini, Carrie na Chanel wakacheka, kwakweli nyie watu mana have a little love affair, sio kwa ku come clean namna hii, dah utadhani mabikira mliotenda dhambi sasa mmekamatwa na bwana Yesu mnaanza kutubu, Chanel akaulizwa we unajikimu vipi maana mimba pia inahitaji dyu dyu, Chanel akasema nipo na bi kidude hapa ni mi stori tu, hataki hata kunipa namba ya Mark aje anibatize anasema anamwogopa Mark basi nimejaa ma upwiru hapa naweza jaza simtank la lita 10,000 ukininyanyua hapa, wenzake wakacheeka maskini Chanel pole bwana bora sie tunaopunguza dhambi zetu kwa majirani Pedeshee akija atapasuka, maana itabidi aogelee tu sasa hehe!

Carrie akasema me sina la kusema yani nikitaka tu hata ofisini namfuata tunajibanza kwenye tainted ya gari tunafungua a/c mambo yanaenda anarudi ofisini me narudi kulea mjamzito hapa, wakamwuliza kwanini hampi Chanel namba ya Mark,a akwa anazuga hataki kusema, Doreen akamnyang’anya Carrie simu akaitafuta namba ya Mark akaipata akachukua simu ya Chanel akaanza kui save! Chanel akawa anacheka tu sasa Doreen unataka Mark aogelee kwenye simtaki we vepee? Wakawa wanacheka baadae hao wakashuka kwenda church kuongea na Pastor kuhusu sadaka ya shukrani.



Kufika kwa Pastor akafungua kwa maombi pale kama traditional ya walokole inavyosema, baadae akaelezwa ujio, akakubali akawapa tarehe, baadae akawashukuru kuwa wamemkumbuka Mungu, akaanza kuwaombea mmoja mmoja, alipofika kwa Carrie akaguna! Mh! Mama naomba uombe sana kuna hatari mbaya mbele yako unaweza ipoteza familia yako yote, omba Mungu akusaidie, akafika kwa Chanel akamwambia utajifungua salama mtoto wa kiume wewe na mumeo mtaishi maisha mazuri sana, ila mumeo haupo nae sasa, jitahidi ukae kwenye uaminifu wa ndoa la sivyo utampoteza for good mumewako, ila mumewako anakupenda sana wewe na mtoto mtarajiwa. Chanel akasema sawa ila me kufunga siwezi labda niombe tu kawaida, Pastor akamwambia sawa vyovyote ilimradi uombe.

Akaja kwa Adrienne akamwambia mumeo ni mtu mzuri na Mungu ameshamponya na hatari mbaya sana, kaa kwa uaminifu kwenye ndoa, usichepuke unaweza pata mimba ingine ikaja kuleta kizaa zaa kwa mumeo, na ikatokea ukapata mimba usiitoe watoto wote ni wa Baraka wanatoka kwa Mungu, akawa anashangaa tu akasema wewe omba maombi ya Shukrani kwa Mungu na ombea familia yako ulinzi wa Mungu.

Akaja kwa DOREEN, eh Pastor akanza kuguna, roho inamuuma, sana sana, akaanza kulia pale warembo wanamshangaa, ikabidi akae tu chini, eh Doreen haelewi huyu Pastor mwanga au psychic?! Pastor akanyamaza akarudi wka Doreen akapiga maombi kama dk 20 warembo wakaamua wakae tu chini maana walisimama, Pastor akamwuliza unampenda mumeo kwa dhati? Doreen akasema ndio. Basi kama atarudi umpokee kama alivyo, kazi anayoifanya ni ngumu sana na itamgharimu maisha yake kutoka lakini maombi ni kila kitu kila siku mwombee mumeo, ukae kwa uaminifu usichepuke atarudi salama kama utakaa kwa uaminifu! Mh Doreen akasema sawa ila akayashika uzuri moyoni maana sio kwa lile chozi la Pastor!



Baadae wakaruhusiwa wakaondoka njiani wanaanza kuulizana ivi mara ya mwisho wenzangu mlifunga lini na masaa mangapi? Maana me nakula kama pipa akasema Carrie, wenzake wakacheka, wakamwambia Doreen usijali bwana yale machozi ya Pastor ni manukato kwa Mungu yataenda kumponya mumeo, wakawa wanamtia moyo pale. Baadae Carrie akamwambia Chanel, umeskia hamna kuchepuka so namba ya Mark ukaifute ivoo! Wakaanza kucheka owte



ITAENDELEA KESHO SAA 6 MCHANA.
Ilibid nirud nione pastor alimwambia nnini carrie Ila wachungaji sio wa kuwadharau
 
Huu msiba umenikumbusha machungu niliyonayo ya kufiwa mtu muhimu sana daah kweli msiba usikie kwa jirani ukikufika unabaki na butwaa kama umepigwa kofi kali sana.
 
Naanza kuichukia hii hadithi carie atapigwa na nani miti mbona kucheleee money penny unatuonea timu George sio kwa miti ile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom