Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,942
- 6,860
X-Paster,
Ingekuwa masuala haya yameanzia Somalia, ningekuelewa. Uovu huu umekuwa ukifanyika karibu kila mahali ambapo wametangaza kuongozwa na sharia. Nigeria wamehukumiwa wanawake kwa kupata mimba, Saudi Arabia wamehukumiwa wanawake kwa kubakwa, Pakistani wamehukumiwa wanawake kwa kubakwa, Sudan almanusura mwanamke ahukumiwe kifo kwa kuita doli Mohamed n.k. Wote hawa wamehukumiwa na waislamu wanaodai wanatekeleza yaliyomo kwenye Sharia. Na hakuna mahali ambapo waliotoa hizo hukumu wameadhibiwa kwa kupotosha Sharia.
Baadhi ya askari wa kimarekani (ambamo kwa taarifa yako wako waislamu , wayahudi, wasio na dini n.k.) wametenda uovu mwingi si tu katika maeneo ya vita bali hata kwengine. Wanajeshi hawa wamesemekana kujihusisha na ubakaji hata huko Japani. Lakini matendo haya yalipogundulika, serikali yao imeyalaani na kuchukua hatua dhidi ya wahusika. Kuna kesi zinaendelea hadi hivi sasa. Kuna wanajeshi wamehukumiwa kifungo. Na juu ya yote, serikali ya Marekani si ya kikristu pamoja na kuwa wakristu wengine wangependa iwe hivyo. Hii ni tofauti na nchi ( au majimbo yake ) nilizozitaja hapo awali.
Kusema tuu kuwa vitendo kama hivi si uislamu haitoshi. Itakuwa vyema kama utawa-comfort wanaodhani hivyo kwa kuwafahamisha uislamu unasema nini kwa makosa kama haya. Itakuwa vyema kama mataifa yanayojiita ya kiislamu yakijitokeza na kulaani kwa nguvu zote panapotokea matendo kama haya. Kama nchi za ulaya zenye wakristu wengi zilivyolaani na kuendelea kulaani matendo ya Marekani. Ukimya wenu ndio unaotufanya tudhanie kuwa huu ni uislamu.
Amandla......