Somali Bantus walikataliwa Somalia, UN waliomba warudishwe kwao Tanzania

Maswali ya msingi kuulizana hapa ni haya yafuatayo:
1. Nani alikuwa anafanya biashara hiyo ya watumwa ?
2. Kwanini biashara ya utumwa isitawi kwenye jamii ambayo watu wake ni washika dini sana ?

Hakuna biashara ya utumwa iliyofanyika kwa wabantu waliohamia Somalia. Walinunuliwa na nani?

Somalia ina wakazi wengi wenye asili ya kibajuni,wamarca na,mchanganyiko wa wasomali na wareno wanaitwa (Gibilcad).

Kama mtu huna uhakika na unachokiandika bora uulize.
Jimbo la Shabelle Hose mdio makazi ya wabantu wengi wao waliohama kutoka Uzigua na wengine kutoka Lindi na Mtwara.
Mpaka sasa jimbo hilo lina wakazi hao wengi na wanaishi kama wasomali wengine.
 
Hakuna biashara ya utumwa iliyofanyika kwa wabantu waliohamia Somalia. Walinunuliwa na nani?Somalia ina wakazi wengi wenye asili ya kibajuni,wamarca na,mchanganyiko wa wasomali na wareno wanaitwa (Gibilcad).
Kama mtu huna uhakika na unachokiandika bora uulize.
Jimbo la Shabelle Hose mdio makazi ya wabantu wengi wao waliohama kutoka Uzigua na wengine kutoka Lindi na Mtwara.
Mpaka sasa jimbo hilo lina wakazi hao wengi na wanaishi kama wasomali wengine.
Sawa mtaalamu, lakini naomba unisaidie kujibu haya maswali yafuatayo:
1. Hao Wabantu walihamia huko mwaka gani ?
2. Miaka hiyo wanahamia Somalia, eneo hilo lilikuwa linatawaliwa na nani ?
3. Nini kiliwavutia au shughuli ipi ya kiuchumi au kijamii iliwavutia hao Wabantu kuhamia huko Somalia ?
 
Wana miaka zaidi ya 150.Kilichowafanya wahamie ni ardhi ya kulima kwenye eneo hilo la Shabelle Hose.
Wahamiaji hao kiasili ni wakulima na waliingia kama wahamiaji na kukuta eneo hilo lina rutuba na kuweka makazi yao na kuanza kulima.
Wakazi wengine wa Somalia kiasili ni wafugaji.
Ushahidi wa hilo ni kwamba mpaka sasa majority ya wabantu hao wanaishi eneo hilo.
Kuna wengine wamehamia sehemu zingine na kufanya kazi zingine zilizo nje ya kilimo.
Somalia ilipoanza kutawaliwa na Italia wabantu hao walilazimishwa kulima na wakoloni hao wa kitaliani ili kulima mazao yatakayokuwa mali ghafi na pia ndizi mbivu ambazo zilipelekwa Italia.
 
Naona unazunguka mbuyu na hutoi majibu yanayoeleweka, unaruka huku na kule:
1. Kwahiyo hao wabantu walikosa maeneo yenye rutuba huku Tanganyika wakaamua kwenda kulima Somalia ?
2. Halafu una uhakika hao wabantu walifika huko Somalia miaka 150 iliyopita, au umeamua tu kuandika ?
3. Kuhusu kilimo, hao wabantu waliruhusiwa na wenyeji kumiliki ardhi yao binafsi au walikuwa "Mushunguli" (Manamba) ?
 
Tatizo lako unaelezwa jambo unaleta hoja zisizokuwa na msingi.Kwani makabila yaliyohama Ethiopia na Sudan kusini kuja Tanzania enzi hizo walikosa ardhi?
Unataja mushughuli eti ni manamba!!!
Mushughuli ni koo mojawapo katika jamii hiyo ya wabantu.
Ardhi hiyo wameimiliki wenyewe kwa zaidi ya karne moja na walikuwa na Mwalimu wao wa kidini Sheikh Aweys ambaye alikuwa na Markas kubwa eneo hilo.Markas eneo kubwa la kufundishia dini.
Wasomali wengi enzi hizo walikuwa watu wa kuhama hama wasiokuwa na makazi maalum hivyo hakuna suala la kumiliki ardhi.
Jamii hizo zilianza kupata makazi ya kudumu miaka ya karibuni ingawa jamii za wafugaji hasa wa ngamia hazina makazi ya kudumu bali zinahamahama.
 
Naona umekuwa mkali bila kunipa majibu yanayoeleweka.......
1. Wabantu walihamia Somalia miaka gani, kweli walihamia miaka 150 iliyopita ? (Una uhakika na hili)
2. Nani alikuwa anaitawala Somalia kipindi hicho ? kiuweli hao masheikh wako hawakuwa ndiyo watawala wa Somali.
3. Somalia ilikuwa ni nchi ya kikabaila (A Feudal State), nauliza hiyo ardhi ya kulimia hawa wabantu waliipataje ?

NB: Mbona maswali haya ni rahisi tu, nijibu na unipatie vyanzo vya taarifa ili nithibitishe siyo blah blah.....
 
Huu ni uongo wa wazi.Wasomali hawa wenye asili ya Nchi za Tanzania na Msumbiji walikwenda kutafuta makazi kama wahamiaji wengine.Waliondoka Somalia mwaka 1991 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Somalia.
Wasomali hawa hawabaguliwi huko Somalia na wameoana na kuzaa na jamii walizozikuta.
Kuna wapemba walikimbilia Somalia 1992 baada ya vurugu za Zanzibar.Wapo wanaishi mpaka leo na wameoana na wenyeji wa huko .Kwanini hawa wapemba wasibaguliwe.
Wanyamwezi,wanyasa na wamakua waliohamia Zanzibar nao walikuwa watumwa?Au walihamia kutafuta makazi na riziki?Abeid Amani Karume alikuwa mtumwa?Kwani hakuwa na asili ya Zanzibar!
Jiulize kwanini wapemba walikimbilia Mogadishu Somalia na sio Mombasa Kenya?

Nani muongo sasa? Hiyo ni report ya UN HCR wao (UN) ndio waliowaombea hifadhi Tanzania na wengine kuchukuliwa na USA, na ndio walikuwa wanabaguliwa kwa sababu ni Wabantu na ndio maana wakarudishwa Tanzania, sasa ni uongo upi unaousema?
 
Naona umekuwa mkali bila kunipa majibu yanayoeleweka.......
1. Wabantu walihamia Somalia miaka gani, kweli walihamia miaka 150 iliyopita ? (Una uhakika na hili)
2. Nani alikuwa anaitawala Somalia kipindi hicho ? kiuweli hao masheikh wako hawakuwa ndiyo watawala wa Somali.
3. Somalia ilikuwa ni nchi ya kikabaila (A Feudal State), nauliza hiyo ardhi ya kulimia hawa wabantu waliipataje ?

NB: Mbona maswali haya ni rahisi tu, nijibu na unipatie vyanzo vya taarifa ili nithibitishe siyo blah blah.....
Hinnebusch The shungwaya Hypothesis.
Shungwaya Revisited History in Africa 4.
Mkuu mimi nimesoma kuhusu hii jamii kwa mapana sikimbilii hearsay.
 
Nani muongo sasa? Hiyo ni report ya UN HCR wao (UN) ndio waliowaombea hifadhi Tanzania na wengine kuchukuliwa na USA, na ndio walikuwa wanabaguliwa kwa sababu ni Wabantu na ndio maana wakarudishwa Tanzania, sasa ni uongo upi unaousema?
Kuhusu kubaguana wasomali wanabaguana sana kiukoo na kuna koo wanawake wao hawaolewi.
Wengi walitumia fursa ya vita kudai asylum Marekani na Ulaya na sababu rahisi ni kudai ubaguzi.Afadhali ya hata wao wanaoana na wasomali wasio wabantu.
Kuna wasomali wana ukoo unaitwa midgan hawaolewi na wanabaguliwa haswa.Na hao sio wabantu.
Hata vita vya wenyewe kwa wenyewe ni muendelezo wa kubaguana ki ukoo ingawa wote wanafanana kimuonekano , lugha moja ingawa ina lahaja tofauti.
 
Sasa kwa nini walirudishwa Tanzania (Tanga) na siyo Kenya au Uganda ?
 
Hinnebusch The shungwaya Hypothesis.
Shungwaya Revisited History in Africa 4.
Mkuu mimi nimesoma kuhusu hii jamii kwa mapana sikimbilii hearsay.
Kama umesoma kwa mapana kwanini unataka kutuaminisha kilazima kwamba wabantu walienda Somalia kufanya kilimo huku ukikwepa kutaja uwepo wa biashara ya watumwa (The East-African Slave Trade) ambayo iliuza maelfu wa Wayao, Wazaramo na Wazigua. Unataka kutakatisha uovu unaofanywa kupitia mgongo wa dini ?

NB: Hebu wacha hizi, mambo bwana (Do not let religion shape your understanding of history)........
 
Jibu hili swali hao unaosema waliuzwa kwa nani?
Nani aliwanunua na kwa minajili gani?
Watumwa waliouzwa Marekani,Amerika Kusini walipelekwa kulima.Hawa wabantu unaodai waliuuzwa Somalia walinunuliwa na wenyeji?Walipokwenda Somalia walikuwa chini ya nani?
Wacha kusikiliza hearsay bila ushahidi.
Hiyo theory inayodai unavyotaka wewe haina uzito.
Ili kuwe na biashara lazima kuwepo na supply na demand sasa hao wabantu waliuzwa na nani?Walinunuliwa na wasomali wenyeji?Au kuna hao waarabu Somalia?Hiyo angle ya dini wewe ndio unaileta.Wapi nimezungumzia dini?
 
Sasa kwa nini walirudishwa Tanzania (Tanga) na siyo Kenya au Uganda ?
Kwa sababu kiasili walitokea Tanga na Mtwara.Someni theories tofauti na tafuteni ukweli kwenye historia kwenye vyanzo tofauti.Wacheni kukaririshwa kama kasuku.
 
Sasa kwa nini warudishwe kama Somalia ni kwao ? UNHCR wanasema huko Somalia Bantu Somalis wanabaguliwa na kutengwa na ndiyo sababu ya kuwaombea warudi Tanzania, sasa wewe unapingana na UNHCR ?
 
Kwa sababu kiasili walitokea Tanga na Mtwara.Someni theories tofauti na tafuteni ukweli kwenye historia kwenye vyanzo tofauti.Wacheni kukaririshwa kama kasuku.

Hapo chini ni Wabantu- Wasomali wenyewe wanailezea Historian yao, bado unawapinga ?

Hapo imeelezwa wametoka Niger Congo Region na eti karne ya 19 wakaletwa na wafanyabiashara wa kiarabu.
Sasa hawa wa Niger Congo Region ndio hao hao wazigua,wamakua?Hao waarabu waliwatoa wapi.?
Hii historia ni ya mzungu hakuna mbantu msomali anayezunguzia hiyo historia unayoiita "yao".Be critical my friend wacha kulishwa matango pori na wewe unakariri tu!
 
Jibu hili swali hao unaosema waliuzwa kwa nani?
Nani aliwanunua na kwa minajili gani?
Watumwa waliouzwa Marekani,Amerika Kusini walipelekwa kulima.Hawa wabantu unaodai waliuuzwa Somalia walinunuliwa na wenyeji?Walipokwenda Somalia walikuwa chini ya nani?
Wacha kusikiliza hearsay bila ushahidi.
Hiyo theory inayodai unavyotaka wewe haina uzito.
Ili kuwe na biashara lazima kuwepo na supply na demand sasa hao wabantu waliuzwa na nani?Walinunuliwa na wasomali wenyeji?Au kuna hao waarabu Somalia?Hiyo angle ya dini wewe ndio unaileta.Wapi nimezungumzia dini?
Sawa, Wayao walikwenda Somalia kutafuta maisha na kufanya kilimo.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom