Soma unafiki wa waziri wa elimu tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma unafiki wa waziri wa elimu tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Oct 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,265
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  Majeruhi wawili Idodi watelekezwa hospitalini  na Francis Godwin, Iringa
  WAKATI chanzo cha moto uliozuka ghafla juzi usiku katika chumba cha darasa kinachotumiwa kama bweni la muda la wavulana kwenye Shule ya Sekondari Idodi kikiendelea kuwavuruga viongozi mkoani Iringa, majeruhi wa moto wa kwanza shuleni hapo wametelekezwa hospitalini bila msaada.

  Katika uchunguzi wa kina uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwapo kwa hali hiyo huku mzazi mmoja wa wanafunzi wawili wanaoendelea kulazwa katika hospitali ya mkoa akitihibitisha kuishi kwenye hali ngumu.

  Majeruhi wawili, Sabrina Abdalahaman, wa kidato cha nne na Veronica Nyamle wa kidato cha tatu ndio wanaoendelea na matibabu katika wodi namba saba ya hospitali hiyo hadi sasa.

  Verotea Ndelwa, mzazi wa Veronica, amelieleza gazeti hili kuwa hivi sasa anaishi kwa taabu wodini hapo pamoja na mgonjwa wake kutokana na kuishiwa fedha za chakula na dawa.

  Alisema, baada ya moto uliozuka Agosti 23 mwaka huu, viongozi wa serikali walifika kuwapa pole ya sh 50,000 kila mmoja na baada ya hapo, kiasi kama hicho kilitolewa wiki mbili zilizofuata na tangu hapo hakuna msaada wowote uliotolewa kwa mgonjwa huyo.

  “Kwa kweli napenda kutumia nafasi hii kwanza kuupongeza uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwani wamekuwa karibu na mgonjwa wangu na hata baadhi ya wauguzi wamekuwa wakinipa msaada wa mahitaji madogo madogo, ila serikali na shule sijaona misaada yao.

  “Mimi hapa namuuguza mwanangu kama baba na mama, kwa kuwa mzazi mwenzangu alishafariki dunia, nilipopata fedha zangu za akiba ya kulimia mashamba nimemaliza kwa matibabu ya mtoto na sipendi kusema nimetelekezwa, ila hali ni kama hii unayoiona hapa, sina hata maji ya kumpa mgonjwa anywe dawa,” alisema mama huyo.

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk. Oscar Gabone, alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri na kuwa mwanafunzi mmoja aliomba kuruhusiwa ili kwenda kufanya mtihani wa kidato cha nne.

  Majeruhi hao wameendelea kuishi katika mazingira magumu hospitalini hapo huku serikali ya mkoa ikiendelea kupokea fedha za rambirambi na pole kutoka kwa wananchi mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi hao.

  Pamoja na kuendelea kupokea fedha hizo, wajumbe wa iliyokuwa tume ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, iliyoundwa kuchunguza moto wa Idodi, ilitoa mapendekezo ya kuweka utaratibu mzuri wa kuratibu misaada inayotolewa kwa ajili ya shule hiyo na kusimamia matumizi yake.

  Pia ilipendekeza ndugu waliopoteza watoto wao kupewa rambirambi zao kwa muda unaofaa na wale wahanga wa tukio hilo kupewa fedha za pole, jambo lililoibua maswali yasiyo na majibu kutokana na kuwapo kwa taarifa kuwa ndugu wa wanafunzi waliofariki dunia kwenye moto huo walipewa pole ya sh 500,000 kila mmoja, fedha ambazo hazijawafikia walengwa.

  Tume hiyo iliundwa na wajumbe sita chini ya uenyekiti wa Paschal Mhongole (mkuu wa wilaya mstaafu), Tasili Mgoda, Rosemary Staki, Rustica Fung’ombe, Augustine Mwadasi na Ally Mbata.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa unafiki wa waziri wa elimu uko wapi hapo?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ishu ya fedha kutowafikia walengwa ni tofauti na pesa kutotolewa... hapo pana shida ya utendaji na siyo waziri anayehusika direct...! Lazima tuweke mipaka waungwana!
   
Loading...