Soma tu unaweza ukapata fundisho!!!!

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,999
Bwana Yesu asifiwe....

Asalaam Aleikum....

Tumsifu Yesu Kristu...

Story ya kweli kabisaaaa.....

Iko hivi, kuna mdada mmoja alitoka katika familia ya kifukara sana Usukumani (Bariadi) tumuite "Kija" Kija alikuwa msichana mrembo tu ila hali ya kiuchumi ya nyumbani kwao ilimsababisha aonekana kutokuwa na mvuto... Basi mama mmoja ambaye anatokea Bariadi lakini anaishi Jijini Mwanza tumuite "Mrs. Kombe" alikwenda Bariadi kutafuta msichana wa kazi. Kwa bahati nzuri.akampata Kija...Huyu mama hakuwahi kujaaliwa kupata mtoto hata wa dawa ingawa mumewe alikuwa na mali nyingi....

Wakaja mpaka Jijini Kija akaanza kazi, alifanya kazi kwa bidii sana mpaka Mrs. Kombe akafurahi na kumpenda sana Kija, kwa vile Kija alikuwa ameishia darasa la saba basi Mrs. Kombe akaamua kumsomesha Kija elimu ya Sekondari, alianza kidato cha kwanza mpaka cha nne akiwa "day scholar" anafanya kazi zote za nyumbani kisha anakwenda shule. Yule mama akawa anamuongezea pesa katika mshahara wake ili kulipia ada ya shule mpaka alipomaliza kidato cha nne....

Baada ya kumaliza alifaulu kwa kiwango cha kati na akapangiwa kwenda chuo cha Ualimu. Baada ya kumaliza chuo akapangiwa kufundisha shule fulani ya msingi jijini Mwanza.

Yule mama alimlea Kija kama mwanae wa kuzaa na baada ya muda ile hali ya "U-house girl" ilififia akaonekana kama mwanafamilia ya yule mama. Baada ya kupata elimu hiyo Kija alianza kuichukia familia yake ya kuleee Bariadi na kujiona kama alikosea kuzaliwa katila familia hiyo. Mawasiliano yakawa mabaya baina yake na familia yake ya Bariadi.

Basi baada ya kuanza kazi ya ualimu aliamua kuanza kujitegemea, ndipo akakutana na mkaka flan tumuite "Mabula". Walianza mahusiano hatimaye Mabula akamchumbia Kija....Wakapanga siku ya kwenda kwao Kija...Lahaula lakwata!!!!!! Badala ya Kija kumpeleka kwa mama yake (baba yake alikuwa keshafariki) alimpeleka kwa Mrs. Kombe. Basi siku ya siku Mabula akaieleza familia yake kuwa amepata mchumba na taratibu zote zikafuatia, Wazazi wa Mabula walikwenda kwa Mrs. Kombe kama walivyotambulishwa na Kija kuwa pale ndio kwao taratibu zote za kimila zilifanyika ila mama mzazi wa Kija alipewa taarifa na kuhudhuria kama ndugu tu kutoka kijijini na akawa "treated" kama mgeni.

Mahari ilitolewa na aliyeipokea ni Mrs. Kombe (kama mjuavyoa masikini hana haki) yule mama bila aibu alipokea mali na kumgawia mama mzazi wa Kija kwa kisingizio kuwa yeye ndiye amehusika sana na malezi ya Kija mpaka hapo alipofika. Basi send off iliandaliwa na Mrs. Kombe na aliplay party kama vile mama mzazi (Hapa sisemi kama alikosea, ila kumbuka mama mzazi hakushirikishwa hata kwa mawazo) mwisho akafanyiwa bonge la send off "as usual mama mzazi alikuja kama ndugu tu aliyealikwa"....

Wakati wa utambulisho mama mzazi alitambulishwa kama "mama yangu mwingine" Ilikuwa hivi " Kwanza Napenda kumtambulisha mama yangu (akamsimamisha Mrs. Kombe)" Pili.napenda kumtambulisha mama yangu mwingine (akasimamishwa mama mzazi) u can't believe".......... No way ndo ishakuwa hivyo, maisha yakasonga.

Basi sasa baada ya Ndoa Kija akahamia Shinyanga alipokuwa anaishi Mabula, baada ya muda Kija akapata ujauzito akajifungua watoto mapacha, wale watoto walipokuwa Kija alifunga safari moja kwa moja mpaka kwa Mrs. Kombe kuwapeleka watoto waonwe na bibi yao. "Kimila zaidi" Ingawa ilipaswa wale watoto waonwe na mama mzazi wa Kija. Kisha akarudi zake Shy maisha yakasonga.

Mpaka dakika hii Mabula anafahamu ya kwamba Mrs. Kombe na Mzee. Kombe ndio wazazi wa Kija. Ni miaka miwili na miezi kadhaa imepita...

Najiuliza ilitokea mama mzazi wa Kija afariki dunia Kija ataliaje?

Hivi kuna wanawake wapo duniani wana tabia kama hii?????

NOTE: Majina na mahali sio halisi.....

SAMAHANI KWA STORY NDEFU ILA.UNAWEZA UKAPATA KITU.......

Wasalaam

CL
 
Si angemsema tu mama ake jamani .......

kumleta tu duniani ni kazi kubwa sana...anaweza kudhani ni sawa

lakini in one way or another atakuwa anam hurt mama ake akajihisi kuwa neglegeted.....

I love my mom na haka kastori kamenifanya nimpigie sim sa hivi kumjulia khali yake tu
 
Ama kweli ng'ombe wa maskini hazai.

Mrs na Mr Kombe ni mamburula pamoja na wema wao.

Kija ni Jini mtu.

Baaas.

Mme mtu hakuuliza "mama mwingine" ni nani?

Naye ni bweg.e jinga.
 
Mmmmmmmmmmmh! Malipo hapa hapa duniani! Kija yatamkuta ya huyu Kijana Dullah!

Kijana Dullah alikuwa mtoto wa pekeee, sasa kazi ya kumlea baba yake ikawa inamboa! Baba yake akawa amezeeka sana hajielewi tena! Dullah akawa amempakia kwenye gari akampeleka nyumba ya wazee Dodoma huko! Njiani akamwambia mimi bwana nakupeleka kule coz kama ujuavyo Mungu hakukupa kikazazi kikubwa, tungekuwa wengi tungepokezana, ila coz niko mwenyewe na mke wangu huna budi kunisamehe kwa hili ila sina jinsi. Njia nzima mzee analia anamsihi mwanae asimpeleke!Anamwambia yeye ndo mwanae, na mjuu wake ndo familia yake, sasa kule ataishije? Dullah hana simile. Basi kufika kule akamuacha! Haikupita miezi 2, akapata taarifa Mzee katangulia. Yakaisha maisha yakaendelea.

Dullah, nae akawa na mtoto mmoja tu wa kiume kama mzee wake. Nae ikafika siku yake hapo kazeeka akaambiwa sasa jiandae safari ya Moshi nyumba ya wazee imefika! Tofauti na mzee wake Dulla yeye akawa kimyaaa machozi yanamshuka tu! Nae akaenda kubwagwa!

Kija nae wanae watakua!
 
Insecurity + plus low self esteem at work kwa pair zote 4 kama ifuatavyo:-

Mrs Kombe, hhajawahi pata mtoto, anajifariji Kija ni mwanaye kwa kumpa sapoti ya material things. Kwenye jamii anaonekana kaozesha bintiye kiaina inampa faraja.

Kija, low esteem ya kukubali alikotoka, hii ipo kwa wengi na hutokea kkwa mtindo tofauti. Mfano, kuna watu hudanganya baba angu mkuu wa TRA au sijui nini, mradi tu hakubali alikotoka. Na akina Yahya wamo humu humu, mie nafanya kazi ikulu kumbe hana hata kibanda cha chipsi.

Mama Kija halisi, kutojiamini kunakioisababishwa na umaskini na kukosa upeo. Kaamua anyamaze asiwaumize waliomfikisha mwanae hapo. Ukute anaumia kichini chini na anashinda lalamika, 'coward ways za kusuluhisha mambo'

Mme wa Kija, ana u-bushoke, kama ameshindwa jua hadi sasa mama halisi wa mkewe ni yupi?! Basi hazimtoshi. Na kama amejua na anashindwa kum-advise accordingly basi hajiamini hata tone.

Anyway, majuto yakimfika tujuze pia.
 
Jamani inaumiza huyu kija hana akili nzuri hata baada ya kujifungua hajaweza kujua thamani ya mama? Aliyembeba miezi 9 ? Tujifunze kweli: ila itakuja kumpa shida and it wil be too late
 

nyumba ya wazee dodoma?
hii story ya marekani i guess
 
Mwenye mtihani hapo ni Mabula...wengine wote waliobaki ni wanafiki
 
nyumba ya wazee dodoma?
hii story ya marekani i guess

Iko tena ya serikali! Jirani na nyumba ya vichaa walio recover! Ingine iko Moshi Longuo! Ya wazee na vichaa waliopona ila hawakumbuki ndugu zao.

Bongo kama ULAYA! Sema watu si wachimvi wa kujua!
 

Shost kuna msemo wanasema "Masikini akipata ......... Utamalizia!
 
Ama kweli ng'ombe wa maskini hazai.

Mrs na Mr Kombe ni mamburula pamoja na wema wao.

Kija ni Jini mtu.

Baaas.

Mme mtu hakuuliza "mama mwingine" ni nani?

Naye ni bweg.e jinga.

Mrs. Kombe ni mbulula square, sijui hataki kuonekana kama hakuwahi kuzaa, si Kija peke yake bali aliwale wasichana wengi tu na mwisho wa mwaka huu pia ataozesha... Ngoja nione ya mwaka huu ataifanyaje ntawapa mlisho nyuma!
 

Duh... Umenikumbusha ya marehemu bibi yangu alivyofanyiwa na shangazi mke wa mjombaa angu! Nitaiweka humu siku moja!

Ila kuna watu wana roho za kishetani aiseeee!!!!
 

Hapo kwenye blue nami napasubiri sana tu, ingawa simuombei mabaya....

Mrs. Kombe yaan ndo tabia yake kuchukuamabinti wenye hali ya chini na kuwafanya kama wake....

Kija mashauzi kibao, sema nimebadili kabila make ningepondwa mpaka simu ingepasuka, ila kuna makabila flan hapa nchini kwa mashauzi hawajambo. Hivyo.kusema anatoka familia ya kimasikini ni issue, mpaka wajue kuwa kwao wako vizuri pia kasoma! "You know what i mean"

Mabula hana say kwa Kija....

Mama mzazi wa Kija najua anaumia ila ndo hivyo hana option....
 
Mwenye mtihani hapo ni Mabula...wengine wote waliobaki ni wanafiki

Sijui mwisho wa siku Kija anaanza kumwambia kuwa Mrs. Kombe sio mama yangu mzazi au atauchuna mpaka kifo....

Mabula naye sijui atamchukuliaje mkewe, dah ngumu kumesa!

Hata mama yangu awe mwehu sitokuja kumkana hata siku moja.....
 
Shost kuna msemo wanasema "Masikini akipata ......... Utamalizia!

Siku itafika tu huyo Kija atatambaa kwa magoti kumtafuta mama huku akimiminika machozi kama hatakuja cheka tena maishani.
Ila mama yake nae,ile siku ya kupokea posa alipotambulishwa kama mgeni tu ndio ungekuwa mwisho wake kufika hapo,asingekuja kwenye send off wala siku ya ndoa,huyo bint kama anajua maana ya mama angerudi kijijini kuomba radhi tu
 

Mi nilidhani ujivuni ni tabia ya mtu?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…