Soma mtazamo huu na uchangie; Very interesting!

Soma mtazamo huu na uchangie; Very interesting!

Pia nashindwa kuelewa kwann waislamu walalamike kuwa kuwa kuna mfumo kristo wakati vyuo vya kikristo havibagui wala havikuchagulii mavazi, tofauti na vyuo vya kiislamu, mf.Pale Chuo kikuu cha kiislamu morogoro wakristo hawajichagulii mavazi wote kama ni wasichana wanavaa kama waislamu, pale Songea Muslim pia hivyo hivyo, huo sio unyanyasaji kwa wakristo hawa? Mbona waislamu ktk vyuo vya kikristo wapo huru!!.Hivyo waislamu tusipende kulalamika without doing research.Elimu mbovu mnaipata kutokana na kuangalia udin kuliko kuangalia nan ana uwezo gan.

Ni kweli vyuo vingi vya kikristo havina ubaguzi katika mavazi kama wafanyavyo upande wa pili. Hili mimi nalipinga vikali kwani mavazi hayasaidii kitu kama una akili za wastani.
 
Huyo si muislam na anapretend kua ye ni muislam but si muislam,,....na hajitambui ata kidogo,,.....pumbaless hakuna logic hapo,,....mara nyingine bora uwe kimya kuliko kuongea pumba ambazo ata ukimpa bata hatozila,,....brainless ideas,,....!!

ingekua vizuri ungemjibu kwa hoja ni sio kumdhihaki kama unavyofanya!
 
Hapa umenena, Elimu ni tatizo kwa wengi waislamu na wamekazana kusema mfumo kristo kwa kuwa viongizi wengi walioshikilia serikali na maendeleo ki ujumla ni wakristo.
Kihistoria wakristo walithamini saana elimu hata mababu wa kikristo ndio waliowasomesha watoto wao ambao kwa sasa wengi wao ni viongozi na wenye maendeleo.
Kwa upande wa waislamu mababu zao walikazania saana elimu akhera (madrasa) na kuwa sheikh ndo lengo kuu. Na kwa sasa ndio hawa wanaolalamikia mfumo kristo.
Ukweli utabaki pale pale... Kwa dunia ya sasa bila elimu dunia hufiki popote hasa kwenye upande wa uongozi! Cha msingi ni kubadilika na kukubali kuwa ELIMU ndo kila kitu ifanywe iwe ni lazima kwa kila mtu.
Na siku zoote mtu anayelalamikia mifumo ya kidini kama ndio kikwazo chunguza saaana Elimu na malezi yake yaliyomkuza hutobishana nae.

kweli kabisa adui wa uislamu ni uislamu wenyewe na hapo linakuja suala la kihistoria ambapo ktk uislamu elomu dunia haipewi kipaumbele kama elimu aherA.

nA hiyo haijaanza juzi wala jana ni tangu enzi utawala wa waarabu
 
Familia imara na thabiti ndio msingi wa mambo yote mazuri uyaonayo duniani.unapo zungumzia ELIMU, tambua kuwa inaanza na elimu ya awali halafu msingi,sekondari na hatimae chuo kikuu.ndoa ikivunjika wanao ishia kupata taabu ni watoto.hawapati mahitaji muhimu kama mavazi,malazi, chakula na hata elimu bora.
Binafsi nimepata kufanyia utafiti juu ya matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa mikoa ya LINDI, MTWARA NA PWANI.Matokeo ya utafiti ule yalinishangaza sana.zaidi ya asilimia 95 ya wasichana wote wanao hitimu kidato cha nne hawaendi kidato cha tano.Zaidi ya asilimia 85 ya wavulana wote wanahitimu kidato cha nne hawaendi kidato cha tano.Lakini pia mikoa hii yote kwa pamoja ina shule za sekondari chache kuliko mkoa wa kilimanjaro au Mbeya. hali ikiwa hivyo maana yake ni kwamba wasomi kutoka mikoa hii yenye waislamu wengi itazalisha wasomi wachache kuliko Kilimanjaro au Mbeya.MSINGI WA TATIZO HILI NI KUWA KARIBU ASILIMIA 80 YA WANAFUNZI WOTE WA LINDI, MTWARA NA PWANI wanalelewa na mzazi mmoja au wanakaa na babu zao au nyanya zao!weak familiea means weak or poor upbringing.

pia sababu nyingine ni kuwa na viongozi ambao hawana elimu dunia mf ponda ni wazi kabisa hana maono ya kimaendeleo
 
Mkuu Remote ukiangalia sehem walizopita waarabu kama Tabora, Tanga Pwani na mikoa mingi Tanzania maendeleo yamechelewa kufika kutokana na mafundisho mila na jadi za hawa waarabu.

Tunashuhudia nchi kama Somalia, Misri na nchi za mashariki ya kati zilivyokuwa na vurugu za wao kwa wao japo ya kuwa na uongozi ambao ni 100% mfumo wa uislam na mahakama ya kadhi.

Elimu ya dunia ni kila kitu
 
Last edited by a moderator:
pia sababu nyingine ni kuwa na viongozi ambao hawana elimu dunia mf ponda ni wazi kabisa hana maono ya kimaendeleo

Hilo nalo ni jambo la kweli. Utakuta sheikh anachanguliwa kwa kuwa tu ni msemaji mzuri katika umma bila kujali elimu yake. Unafikiri kama hana elimu ya dunia na hata ya dini nini atakachoongea chenye tija zaidi ya kumislead waumini.

Kimsingi Bakwata ndio wenye jukumu la kusimamia uchaguzi wa viongozi masheikh nk. Lawama kubwa zinatakiwa zitupiwe kwao kwa kutotimiza wajibu wao. Pia utaratibu wa kujenga misikiti unaofanywa na waumini binafsi udhibitiwe na Bakwata kwani ndio chanzo cha kusimamisha masheikh wasio na sifa.
 
Udini udini udini utawasaidia nini hasa mwanzisha huu uzi?
 
Hapa hakuna udini kama unavyoeleza na kujaribu kutuaminisha bwana Shine. Suala ni kubwa ni nini kifanyike ili taifa lisiingie katika mpasuko. Suala la dini huwezi kulikwepa kwani mataifa makubwa yote yana dini wanazoamini. China wana Budhism, India wanaabudu wanyama na miti, UK na US wanaamini katika ukristo.
 
Last edited by a moderator:
Mi nakushaur vitabu hivi kwa kuanzia, huenda kwanza ukajua maana ya neno 'MFUMO' pili utanjua ni namna gani unavyoshuughulikia waislam na uislam ikiwa ni pamoja na kuwatumia haohao waislam kama wew au BAKWATA kuwakandamiza waislam wenzetu hasa watanzania.
1. Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 hadi 1985 by Padre J.C. sivalon.
2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes by Mohamed Said.
3. Muslim and the State in Tanzania by Prof. Njozi, H.M.
4. Mwembechai Killings by Prof. Njozi H.M.
5. Kwa Heri Ukoloni, Kwa Heri Uhuru by Harith Ghassani.

Huenda ukajua nini waislam wanazungumza kama kweli ni mwenye kufikiri lakini.
 
Mi nakushauri ukasome vitabu hivi kwa kuanzia, huenda, kwanza ukajua maana ya neno 'MFUMO' pili utajua ni namna gani unavyoshuughulikia waislam na uislam ikiwa ni pamoja na kuwatumia haohao waislam kama wew au BAKWATA kuwakandamiza waislam wenzetu hasa watanzania.
1. Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 hadi 1985 by Padre J.C. sivalon.
2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes by Mohamed Said.
3. Muslim and the State in Tanzania by Prof. Njozi, H.M.
4. Mwembechai Killings by Prof. Njozi H.M.
5. Kwa Heri Ukoloni, Kwa Heri Uhuru by Harith Ghassani.

Huenda ukajua nini waislam wanazungumza kama kweli ni mwenye kufikiri lakini.
 
Mi nakushaur vitabu hivi kwa kuanzia, huenda kwanza ukajua maana ya neno 'MFUMO' pili utanjua ni namna gani unavyoshuughulikia waislam na uislam ikiwa ni pamoja na kuwatumia haohao waislam kama wew au BAKWATA kuwakandamiza waislam wenzetu hasa watanzania.
1. Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 hadi 1985 by Padre J.C. sivalon.
2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes by Mohamed Said.
3. Muslim and the State in Tanzania by Prof. Njozi, H.M.
4. Mwembechai Killings by Prof. Njozi H.M.
5. Kwa Heri Ukoloni, Kwa Heri Uhuru by Harith Ghassani.

Huenda ukajua nini waislam wanazungumza kama kweli ni mwenye kufikiri lakini.

Kwa kutumia hivyo vitabu vitano vilivyoandikwa na authors mbalimbali ungejibu au ungeshauri kwa hoja kwa kuwa wewe unaonekana umeshavisoma.

Kwa nini usitumie yaliyoandikwa kwenye hivyo vitabu kutoa ushauri au elimu bure kwa waislam walio wengi na si kila muislam kusoma hivyo vitabu.
 
Jambo la kusema tu hapo ni kwamba waislam wameshafanya tafit za kutosha juu ya hayo yote na ndio maana wametambua kuwa adui # 1 ni 'mfumo kristo' na sio wakristo.

Hebu pata picha mfumo wa upumuaji ufanyavyo kazi, yaani punje ya chakula inapojaribu kuingia kwenye tundu la hewa tu bas punje hiyo itaonekana korofi kupita kias na kutupwa mbali na hata mtu kukohoa vibaya mno, na hivyo ndivyo mfumo kristo ufanyavyo kazi ktk Tanzania baada ya kuwekewa misingi imara na babake Makongoro kw kuwa kiungo muhim sana kati ya kanisa na serikali, hivyo kusababisha waislam kuonekana wanalalamika au kuleta fujo baada ya kudai haki zao bila mafanikio kwa muda mrefu na kuchoshwa na hali hiyo kujirudiarudia na vikwazo kuonekana ni vilevile.

Kumbe hawakujua kuwawanuingilia mfumo kristo hasa ktk nafas nyeti kama vile elimu na uchumi hivyo kuonekana kama ile punje ya chakula na ndio maana nchi kwa sasa inakohoa vibaya mno .

Sishangai hali ya sasa hasa baina ya waislam thabiti na mfumo kristo ilivyo, kwan ni matokeo ya juhud za makusudi zilizofanywa na babake Makongoro.
Wakat baba na babu zetu wakihangaika kumpa sapoti ktk kuijenga Tanzania imara kumbe yeye alikuwa akihangaika kuihakikisha kuipa kanisa nafasi nzuri ktk nchi bila waislam, wakristo n.k. walio wengi kutambua.
Huenda ikawa ndio chanzo cha kutoendelea kwa Tanzania kwa kasi iloyotarajiwa na wengi, kumbe miaka 27 yote ilipotea ktk kutengenezea upande moja nafasi nzuri na kubagua upande mwingine.

Maneno yake nje yalikuwa tofauti na matendo yake kindani.

Hakuna amani pasipo na haki.....
 
Mkuu Remote ukiangalia sehem walizopita waarabu kama Tabora, Tanga Pwani na mikoa mingi Tanzania maendeleo yamechelewa kufika kutokana na mafundisho mila na jadi za hawa waarabu.

Tunashuhudia nchi kama Somalia, Misri na nchi za mashariki ya kati zilivyokuwa na vurugu za wao kwa wao japo ya kuwa na uongozi ambao ni 100% mfumo wa uislam na mahakama ya kadhi.

Elimu ya dunia ni kila kitu

Nchi za kiislam zikiachiwa zijitwale kwa sheria za kiislam huwa ni tishio kwa nchi za maghribi, hivyo huanzishiwa chokochoko na propaganda ili hali ya hewa ichafuke then wamagharib wafanye yao.

Mbaya zaid wamagharibi hutmia vyombo vya habari kujitangaza ktk sura nzuri na kuwachafua wengine.

Hivyo kuwashika watu wenye muono mdogo na kutofuatilia taarifa kwtk unalisia wake kama wewe ndugu
 
Last edited by a moderator:
Jambo la kusema tu hapo ni kwamba waislam wameshafanya tafit za kutosha juu ya hayo yote na ndio maana wametambua kuwa adui # 1 ni 'mfumo kristo' na sio wakristo.
Hebu pata picha mfumo wa upumuaji ufanyavyo kazi, yaani punje ya chakula inapojaribu kuingia kwenye tundu la hewa tu bas punje hiyo itaonekana korofi kupita kias na kutupwa mbali na hata mtu kukohoa vibaya mno, na hivyo ndivyo mfumo kristo ufanyavyo kazi ktk Tanzania baada ya kuwekewa misingi imara na babake Makongoro kw kuwa kiungo muhim sana kati ya kanisa na serikali, hivyo kusababisha waislam kuonekana wanalalamika au kuleta fujo baada ya kudai haki zao bila mafanikio kwa muda mrefu na kuchoshwa na hali hiyo kujirudiarudia na vikwazo kuonekana ni vilevile.
Kumbe hawakujua kuwawanuingilia mfumo kristo hasa ktk nafas nyeti kama vile elimu na uchumi hivyo kuonekana kama ile punje ya chakula na ndio maana nchi kwa sasa inakohoa vibaya mno .
Sishangai hali ya sasa hasa baina ya waislam thabiti na mfumo kristo ilivyo, kwan ni matokeo ya juhud za makusudi zilizofanywa na babake Makongoro. Wakat baba na babu zetu wakihangaika kumpa sapoti ktk kuijenga Tanzania imara kumbe yeye alikuwa akihangaika kuihakikisha kuipa kanisa nafasi nzuri ktk nchi bila waislam, wakristo n.k. walio wengi kutambua.
Huenda ikawa ndio chanzo cha kutoendelea kwa Tanzania kwa kasi iloyotarajiwa na wengi, kumbe miaka 27 yote ilipotea ktk kutengenezea upande moja nafasi nzuri na kubagua upande mwingine.
Maneno yake nje yalikuwa tofauti na matendo yake kindani.

Hakuna amani pasipo na haki.....

Bwana SUKAH ngoja nikurejeshe kwenye maelezo ya bwana Mtoi anayeeleza kuwa

"Siuoni mfumo Kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo Kristo, siuoni kwa kuwa hii nchi ni ya Wakristo, Wapagani, Waislamu, Wahindu na dini nyingine.
Siuoni mfumo Kristo kwa kuwa nimeshuhudia watu kama kina Omari Mahita, na Said Mwema wakiwa viongozi wa vyombo ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauaji ya Waislamu wenzetu na ndugu zetu Wakristo.
Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu lakini siuoni mfumo Kristo nikimwangalia JK na Makamu wake. Siuoni mfumo Kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi Shein na Seif Shariff Hamad. Siuoni mfumo kristo nikimwangalia Chande Othman yule jaji mkuu na Othman Rashid, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Si uoni hata nikiungalia kwenye Wizara na Taasisi nyingine za Serikali"

Katika hali ya mtazamo ambao hauhitaji elimu kupambanua mambo unaweza kuona serikali iliyopo madarakani iko katika mfumo wa kiislam kwa kuwa sehem nyeti zote za kimaamuzi zimeshikiliwa na waislam.

Labda pengine sijaelewa hili neno "mfumo kristo" lina maana gani. Bwana SUKAH naomba unijuze nini maana ya mfumo kristo ili tuendelee na mjadala wetu.
 
Last edited by a moderator:
Nchi za kiislam zikiachiwa zijitwale kwa sheria za kiislam huwa ni tishio kwa nchi za maghribi, hivyo huanzishiwa chokochoko na propaganda ili hali ya hewa ichafuke then wamagharib wafanye yao. Mbaya zaid wamagharibi hutmia vyombo vya habari kujitangaza ktk sura nzuri na kuwachafua wengine. Hivyo kuwashika watu wenye muono mdogo na kutofuatilia taarifa kwtk unalisia wake kama wewe ndugu

Tumeshuhudia nchi kama Somalia ikiwa na mfumo wa kiislam kwa asilimia 100% pamoja na mahakama ya kadhi lakini hali ya nchi hiyo sihitaji kukueleza zaidi.

Mataifa ya yaliyoendelea kiuchumi huwa na hofu kubwa kwa kuwa huwa ni chanzo cha mvurugiko wa amani kwa kujitoa mhanga, ugaidi nk. Nchi kama Somalia wamekuwa wanachinjana na kugombana kwa zaidi ya miaka kumi sasa na hawana utajiri wowote wa kuwindwa na mataifa ya kigeni.

Suala linabakia kuwa bila ya kuipa kipaumbele elimu dunia kwa waislam wote huo mnaouita mfumo kristo utabaki kuwepo siku zote.
 
suala mfano la Somalia ni kwamba jamaa wale wamekataa kutawaliwa na kutumika kama dampo na nchi za magharibi kama ambavyo sis tunafanywa, nchi hiz za maghrib zinataka nchi zote dunian ziwanyenyekee hivyo ukienda kinyume tu utatengenezewa kila aina ya propaganda hasa kwa kutumia vyombio vyao vya habari ambapo hivi vyetu hapa tz hukopi na kupesti na ndo hizi habari unazosimamia wew kama hoja zako.

Kwa mfano haukumbuki wale waingereza walokamatwa Iraq wakiua watu huku wakiwa wamefuga ndevu na kuvaa mavazi yavaliwayo humo ili waonekane kuwa ni nchi hiyo.

Kwani haujui wale wairaq waliotekwa na kupandishwa gari lenye mabomu na kwenda kuripuliwa kwenye kundi la watu.
Hivi huajui juu ya meli zimwagazo kemikali za sumu kwenye bahari ya Somalia then baadhi zkikamatwa na wasomali huitwa maharamia?

Hiyo ni mifano michache ambayo hutokea na ukweli kupotoshwa na hivyo vyombo vyao vya habari ambavyo hutegewa maskio na mlio wengi...
 
The Somali Civil War is an ongoing civil war taking place in Somalia. It began in 1991, when a coalition of clan-based armed opposition groups ousted the nation's long-standing military government.

Various factions began competing for influence in the power vacuum that followed, which precipitated an aborted UN peacekeeping attempt in the mid-1990s. A period of decentralization ensued, characterized by a return to customary and religious law in many areas as well as the establishment of autonomous regional governments in the northern part of the country.

The early 2000s saw the creation of fledgling interim federal administrations, culminating in the establishment of the Transitional Federal Government (TFG) in 2004. In 2006, the TFG, assisted by Ethiopian troops, assumed control of most of the nation's southern conflict zones from the newly formed Islamic Courts Union (ICU). The ICU subsequently splintered into more radical groups, notably Al-Shabaab, which have since been fighting the Somali government and its AMISOM allies for control of the region. In 2011, a coordinated military operation between the Somali military and multinational forces began, which is believed to represent one of the final stages in the war's Islamist insurgency. [6]

In November 2010, a new technocratic government was elected to office, which enacted numerous reforms. Among these, in its first 50 days in office, the new administration completed its first monthly payment of stipends to government soldiers, and initiated the implementation of a full biometric register for the security forces within a window of four months. [30]

By August 2011, the new government and its AMISOM allies had managed to capture all of Mogadishu from the Al-Shabaab militants. [31] An ideological rift within Al-Shabaab's leadership also emerged in response to pressure from the recent drought and the assassination of top officials in the organization. [32]

In October 2011, a coordinated operation between the Somali military and the Kenyan military began against the Al-Shabaab group of insurgents in southern Somalia. [33][34] The mission was officially led by the Somali army, with the Kenyan forces providing a support role. [34] In early June 2012, Kenyan forces were formally integrated into AMISOM. [35] Analysts expect the additional AU troop reinforcements to help the Somali authorities gradually expand their territorial control. [36]

The wikipedia
 
Ukisoma vizuri historia ya Somalia utaona kuwa western nations wamekuja kuisaidia Somali baada ya kuona hali ya amani nchini humo imevurugika. Chanzo kikuu cha ugomvi ni wao kwa wao (yaani waislam wenye itikadi kali (radical islamists) na serikali ya Somalia).

Habari za kuwa kuna meli zilimwaga sumu kwenye bahari yao nazitilia mashaka labda ukiweka source ya kuaminika.

Bwana SUKAH hujanielezea maana halisi ya mfumo kristo. Naomba unifafanulie ili tuendelee na mjadala.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu seremi umezungumzia suala la ndoa katika uislam kuwa ndio tatizo kubwa linaloleta matatizo katika uislam. Mimi sikuungi mkono moja kwa moja kwa kuwa wapo waislam waliostaarishwa na elimu na kuamua kuwa na mke mmoja na hivyo kukuza watoto katika malezi bora. Suala la ndoa siku hizi ni janga si kwa waislam tu bali hata kwa wakristo.

Nadhani suala la msingi hapa ni kuweka kipaumbele katika ELIMU tena ile ya dunia na kwa kiasi flani elimu ya dini. Muumini akishaelimika atastaaribika na maisha yake yatakuwa ya kistaarabu.

Katika ulimwengu wa leo tunashuhudia teknolojia ikitawala ulimwengu hivyo hakuna mbadala wa maendeleo zaidi ya elimu. Ukijaribu kuangalia wakristo walio wengi wameelimika ukilinganisha na upande wa pili. Hii ni kutokana na kuweka kipaumbele katika elimu. Sikatai kuona watoto wa kiislam wakienda madrasa hata nyakati za asubuhi badala ya kuwa shule kwa wakati huo bali nakataa hizo juhudi za elimu ya ahera kupewa kipaumbele zaidi ya elimu ya dunia. Ukiangalia wakristo pia wana mafundisho kama kipaimara Komunio lakini hufanywa baada ya wanafunzi kutoka shuleni (shule ya dunia).

Nadhani ndugu zangu waislam ifikie kipindi tukubaliane na ukweli japo ni mchungu kuwa bila kuweka kipaumbele katika elimu dunia na kubakia katika elimu ahera hakika mfumo kristo hautakwisha.

Hapa ndiyo udhaifu wa BAKWATA unapoonekana,Kama chombo cha kiislamu kilipaswa kuandaa mtaala wa elimu ya maarifa ya kiislamu itakayofundishwa kwa watoto wadogo muda wa jioni baada ya watoto kutoka shule,pia ilipaswa kuandaa waalimu kwa ajili hiyo na mtaala huo ungefuatwa na madrasa zote nchini.Badala yake wapo busy kutumika kwa maslahi ya wengine badala ya kusimamia maslahi ya waislamu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom